Andrew Tate
JF-Expert Member
- Jun 28, 2020
- 4,503
- 6,861
What would you do if hutopata kazi?Mi nina kauli mbiu yangu kuwa"kuwa na elimu ni jambo la Kwanza,la pili lazima na ni lazima uitumie elimu uliyonayo to the maximum huwez nambia una masters afu unachowaza kichwani ni udereva bajaji na umeridhika kabisa haya ni matumizi mabaya ya elimu"
mimi kama cheti changu ninacho nitapambana kama nilivyopambana kusoma nipate kazi sio huo udereva
Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
Are you trying to say hao wote waliibuka tu kutoka kwenye makochi ya wazazi wao au shemeji then boom wanamiliki company au business kubwa?Kujiajiri ni kama walivyofanya kina Mendes wa KopaGas, MakJuice, Wasafi media, Maxence Melo wa JF.
Ni kampuni sustainable, ambazo unaweza kujua kabisa zitaajiri watu, kukuza kipato na kuvutia uwekezaji hata kama ni kupitia DSE.
Sasa yeye biashara ya Bajaj, akilala na yenyewe inalala.
Swali zuri kwa waliopata kazi baada ya kumaliza chuo na kufikiri wanaongaika kwa muda mrefu bila kupata ajira hawana akili !😎What would you do if hutopata kazi?
Ntapambana kimyakimya bila kujisifia magazetini sababu ntakua sijatimiza malengo ya elimu yangu , siku nikitoboa sasa nimejiajiri kwenye fani yangu ndo natoka sasa kuwainspire vijana wa kada yangu na kuwaaajiri pia.What would you do if hutopata kazi?
Mkuu are you even serious.yani kesho kutwa awe na bajaji kumi???acha ulongo field sio kwepesi kiasi hicho ni ngumu na itachukua muda
Ni kujisifia ujinga ujinga tu, Hivi kwa kiwango cha elimu alichofikia alipaswa kuwa dereva wa bajaji? Au ni changamoto ya maisha ndio yamesababisha kujiingiza kwenye kazi ambayo haindani na fani yake? Elimu aliyosoma haijamsaidia chochote bali kumfilisi tu , so mnataka kutuambia si ni bora asingesoma na kuanza kuwa dereva wa bajaji?.View attachment 1660302
Tofauti na mawazo ya wengi kuwa ukisoma hadi chuo kikuu lazima uajiriwe, Mwasu Mavere ameonyesha upande mwingine wa shilingi, kwamba unaweza kujiajiri na kufanikiwa zaidi. Licha ya kuwa na shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), yeye ameamua kuwa dereva wa pikipiki ya miguu mitatu (bajaji) akisafirisha abiria katikati ya makao makuu ya nchi, Dodoma.
Dada Mwasu anasema wasomi wengi wanatembea na bahasha miaka hadi mitatu bila kupata kazi, kumbe wangeuza hata karanga zingewaingizia kipato badala ya kuzunguka na vyeti. Hata hivyo, anasema mfanyabiashara msomi ni tofauti na asiyesoma, kwa kuwa ile elimu aliyonayo msomi anaitumia kufanya vizuri kwenye biashara zake. “Kuna wasomi wengi wanaendesha bajaji na bodaboda na wapo wengine wengi mtaani wanatafuta kazi, hawajajua kuwa kuna kazi ya kuendesha bajaji na kujipatia fedha kama walioajiriwa, hivyo niwatake waache kuchagua kazi,” alisema Mwasu alipozungumza na Mwananchi.
Mwasu alianza shughuli za usafirishaji abiria Desemba 2018 katika eneo la eneo la Royal Village, Dodoma lakini baada ya muda alihamia katikati ya mji ili kupata abiria wa pande zote. Anasema wasomi wengi wanatembea na bahasha miaka hadi mitatu bila kupata kazi, kumbe wangeuza hata karanga zingewaingizia kipato badala ya kuzunguka na vyeti.
Hata hivyo, anasema mfanyabiashara msomi ni tofauti na asiyesoma, kwa kuwa ile elimu aliyonayo msomi anaitumia kufanya vizuri kwenye biashara zake. “Kuna wasomi wengi wanaendesha bajaji na bodaboda na wapo wengine wengi mtaani wanatafuta kazi, hawajajua kuwa kuna kazi ya kuendesha bajaji na kujipatia fedha kama walioajiriwa, hivyo niwatake waache kuchagua kazi,” alisema Mwasu alipozungumza na Mwananchi.
Mwasu alianza shughuli za usafirishaji abiria Desemba 2018 katika eneo la eneo la Royal Village, Dodoma lakini baada ya muda alihamia katikati ya mji ili kupata abiria wa pande zote. “Elimu yangu ni masters, lakini mshahara mdogo niliokuwa nalipwa ndio uliosababisha nikaamua kuacha kazi na kujishughulisha na biashara mbalimbali ikiwemo kuuza nguo na hatimaye nikaanza kuendesha bajaji,” anasema.
Mwasu, mama wa watoto wawili anasema mshahara aliokuwa analipwa ambao haukukidhi mahitaji yake wala kuendana na kiwango chake cha elimu, ulisababisha akaichukia ajira akaamua kujiajiri mwenyewe.Alisema mwaka 2009 alihitimu shahada ya sociology and political science nchini Kenya na baada ya hapo alirudi nchini na kufanya kazi katika NGOs mbalimbali.
Ilifopika mwaka 2011 aliamua kujiendeleza katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) huku akiendelea kufanya kazi. Alihitimu mwaka 2013 shahada ya uzamili katika utawa (Masters of public adminstration). Alisema wakati anafanya kazi kwenye shirika lisilo la kiserikali la Afnet alikuwa programme officer na field officer baada ya muda akahamia katika shirika jingine la Ngonedo ambapo alikuwa monitoring and evaluation officer (ufuatiliaji na tathmini).
Mwasu alisema katika kipindi alichofanya kazi hakuwa na mshahara uliokuwa unazidi Sh390,000 kwa mwezi, ambao amesema haukuwa unakidhi mahitaji yake. Alisema kipindi hicho anafanya kazi alikuwa na mtoto mdogo, hivyo kutokana na mahitaji yake kuwa mengi na mshahara mdogo alipomaliza shahada ya uzamili aliamua kuacha kazi na kuanzisha biashara mbalimbali ikiwemo kuuza nguo. “Hela hiyo haikuwa inakidhi mahitaji yangu, mwisho wa siku nikaona ili nisiingie kwenye vishawishi vya kuiba fedha ofisini ili kukidhi mahitaji, bora niache kazi, niliona ni bora kujiajiri mwenyewe kuliko kuajiriwa kwani nilichokuwa ninalipwa hakilingani na elimu yangu.
“Wakati huo nafanya kazi, nilikuwa nakusanya hela kidogo kidogo na kuna siku nilienda field, pesa niliyolipwa na zile akiba zangu nikaamua kuanzisha biashara kwa mtaji wa Sh400,000. Nilikwenda Kariakoo (Dar es Salaam na kuchukua mzigo wa nguo na kuja kuuza Dodoma.” Alisema Mwasu, biashara yake ilikuwa vizuri na alikuwa anaingiza fedha kuliko zile alizokuwa analipwa wakati ameajiriwa.
Biashara hiyo aliifanya kwa muda mrefu hadi akawa anasafiri kwenda China pamoja na wafanyabiashara wengine kuchukua mzingo wa nguo na kuuza nchini. “Katika biashara kuna kuinuka, lakini pia unaweza kushuka. Biashara yangu ilikuja kuwa mbovu nikawa napata hasara, si kila siku ni kupata faida, hasara kwa mfanyabiashara haikwepeki nawakati huo tayari nilikuwa nishapata mtoto wa pili. “Licha ya hasara hiyo, sikukata tamaa badala yake nikaamua kubadilisha kazi ya kufanya. Niliamua kuachana na biashara kabisa na kuwa dereva bajaj,” alisema.
Endelea kufahamu Kilichomfanya aendeshe bajaji na Manufaa yake pamoja na Changamoto aipatayo kupitia link >>> Mwasu, dereva wa bajaj mwenye shahada mbili
View attachment 1660415
That's good mkuu.Ntapambana kimyakimya bila kujisifia magazetini sababu ntakua sijatimiza malengo ya elimu yangu , siku nikitoboa sasa nimejiajiri kwenye fani yangu ndo natoka sasa kuwainspire vijana wa kada yangu na kuwaaajiri pia.
Unadhani lengo la elimu ni nini?Ni kujisifia ujinga ujinga tu, Hivi kwa kiwango cha elimu alichofikia alipaswa kuwa dereva wa bajaji?
Imagine wewe ni masikini then uwe na elimu kubwa na ushamaliza chuo considering una plans za kumiliki company.Kweli mkuu, mtu amesoma shahada ya kwanza hola ya pili anakuwa dereva bajaji.
Hana cha kuwa mtu wa mfano.
What would happen if kila mtu angeajiriwa?Kilaza tu huyo...ajira zinatangazwa na Utumishi kila day..kama ana uwezo angepata kazi za utumishi. Huo ndio ukweli
Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Wewe kama kweli elimu uliyosoma imekuelimisha basi jibu hilo swali.Ujinga huu nao niwakujivunia?? Master unaenda kuendesha bajaji?? Kweli? Elimu yetu ni ya hovyo sana, badala ya kwenda kutatua changamoto za kijamii na kuja na kitu kipya kama msomi, unakwenda kuendesha bajaji na na yule wa shule msingi atafanya kazi gani?
Unakurupuka. Mimi sina tatizo mtu kujiajiri.What would happen if kila mtu angeajiriwa?
We'll seeUnakurupuka
Nukuu sehemu inayosema huyo dada amekosa ajira?Ila alivosema amekosa ajira na ana masters hapo ndo nikataka kucomment
Tuliza mshono. Nimeona video interviewWe'll see
Nukuu sehemu inayosema huyo dada amekosa ajira?
Kumtangaza magazetini isha mpa popularity, anaweza pata wateja wengi zaidi.Hata ikitokea kazi hutaweza kupambana nae, tayari ana confidence.Kufahamika kuna faida zaidi kuliko hasara.Ntapambana kimyakimya bila kujisifia magazetini sababu ntakua sijatimiza malengo ya elimu yangu , siku nikitoboa sasa nimejiajiri kwenye fani yangu ndo natoka sasa kuwainspire vijana wa kada yangu na kuwaaajiri pia.
Nisipotoboa nikaishia kwenye bajaji nakaa kimya ili nisiwavunje moyo vijana wengine wakaona elimu haina maana.
[emoji1][emoji1][emoji23]Anaendesha Bajaj Kama Dereva mwenye Masters au Kama seven B leaver?
Atumie Elimu Vizuri.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Tujifunze nini sasa? Toa ujinga hapa.
Hatukusomea kuendesha bajaji sisi.
Au nasema uongo ndugu zangu?
[emoji23][emoji23]Vitu vingine sio vya msomi kujivunia kufanya
Hivi umetafiti kuwa mfumo wa elimu yetu haufanani na nchi zingine? Kozi za sociology hazijatungwa ulaya kwel? Political science!! Unataka afundishwe nii ambacho PS haijamfundisha.Ukitaka kujua mfumo wetu wa elimu ni mbovu na unazalisha wajinga ni hizi comments za humu.
Siungi mkono kuendesha bajaj ila kwa masikini hata uwe na PhD huwezi kuanzisha au kufanya vitu vikubwa bila pesa ya kutosha.
Hivyo ni lazima uanzie chini no matter what kama una nia ya kufanya vikubwa au nenda kaajiriwe kama mfumo mbovu wa elimu na jamii kama humu zinavyosema.
Mnajua ana plan gani au ana wekeza nini kwenye hicho anachokifanya?
Kama wewe ni masikini au kwenu hamjiwezi na wewe una elimu kubwa pia una ndoto za kumiliki vitu vikubwa na hutaki kuanzia chini.
Basi endelea kubaki hapo kwa wazazi au shemeji na uendelee kuota hizo ndoto au uendelee kusubiri ajira huku unazeeka.
Kama mnayoandika haya mmesoma basi elimu zenu ni useless pia mfumo wa elimu ubadilishwe mara moja sababu unatengeneza watu ambao ni dreamers, delusional and useless sababu hakuna execution katika chochote wanachosema.
If everything is that easy as you think then you shouldn't be where you are right now.