Wasomi jifunzeni kwa dada Mwasu, dereva wa bajaji msomi mwenye shahada mbili

Tulisema tu hiki chuo cha UDOM kitatutolea takataka ona Sasa. Eti mtu ana MASTAZ dereva bajaj. Jinga kabisa. UDOM ni janga jamani.
[emoji1][emoji23][emoji23]wasomi mmepagawa
 
Anayejiyonga kwa kukosa ajira na anaendesha bajaji yupi bora?
Hivi kwenye kuendesha bajaji mnajua anakutana na watu wangapi? Mnajua niuzoefu gani anaupata?
Siku akipanua mradi bajaji zikawa 10 kuna dereva atamdanganya mapato,vifaa vinavyoharibika Mara kwa Mara,kuiba spea.
Aisee huyo Dada yupo katika shule moja kubwa sana, shule ya vitendo, huyo Dada ametupita wengi humu hata uelewa wa how to get customers.Huyo Dada hata akitaka kuandika kitabu anacho cha kuzungumza, nyinyi mtaandika hisia "not reality"
Ktk ujasiliamali kuna mstari unasema " How to sell" .
Heshimuni watu wanaofanya, experience is very important in life not theory. Mmekazana kuchangia utopolo humu,elimu elimu ikaenda ikarudi wewe umebuni nini na elimu yako ili huyo Dada aje ajifunze kwako jinsi kutumia elimu?
 
Hongera kubwa Tangantika !Jipongeze kwa soda hapo ulipo kati ya hizo pichani.
 
Bajaji unajifun..how to sell haha siunakaa kwa foleni tu na kusubiri abiria
 
Bajaji inabeba watu wanne ambapo total ni sh 2000 , ili upate 30,000/= inabidi uende safari 15 kwa siku, assume unafanya kazi masaa 15 (sa12 asubuhi hadi sa3 usiku) manake kila ndani ya saa moja ujaze abiria utembee , na hapo ujue kijiweni haupo peke yako kuna foleni kama bajaji 10 hivi.
Toa hela ya mafuta
Mzee hiyo 30,000 utaondoka nayo mara chache sana ndai ya mwezi.
Ni biashara nzuri lakn sio mteremko kama unavyoielezea
 
Mambo mengine ni vichekesho kabisa hawa wasomi wa siku hizi wamekuwa na hoja dhaifu sana yaani mtu anarudi mtaani kufanya kazi aliyokuwa anaifanya mzazi au mlezi wake kwa taabu ili amsomeshe chuo halafu wanasema kajiongeza?

Kama ni hivyo kumbe hata anaeishia darasa la saba au form four halafu akaenda kutafuta maisha yake anajiongeza basi.

Huko sio kujiongeza ni mgangaji tu kama wangangaji wengine. minadhani ingekuwa amejiongeza kama angekuwa ametengeneza bajaji yake kwa ubunifu wake halafu ndio anaiendesha hapo sawa. Yaani kuwa dereva bajaji wa kawaida iwe inshu pengine hata bajaji sio yake anapeleka hesabu?! No! no! no! Ieleweke tu kwamba ameamua kuwa dereva wa bajaji kama kazi aliyoamua na si vinginevyo kuwaambia watu waige mfano wake eti kajiongeza. Kulikuwa na haja gani ya kusoma kote huko halafu uje kuendesha bajaji za watu angetengeneza yakwake tuone elimu ilivyo msaidia sio kwa hilo hapana bana.
 
Ubarikiwe kwa shuhuda wako hapa Mersen na kufahamu mpambanaji dada Mwasu dereva mwenzako wa bajaji msomi mwenye shahada mbili mlioko Dodoma.
 
Kituo chenu kiko wapi Mersen hapo mjini ?
 
Hamna chakujifunza hapo ,huo ni upungufu wa akili huwezi kuwa na Masters halafu ukaendesha Bajaji ,
 
Kuna la kujifunza kwenye hii comment yako mkuu inabidi kutafakari sana.
 
Ukifuatilia vizuri story ya huyu dada ni tofauti kabisa na ya huyu mwendasha bajaji, yeye ametengeneza system kabisa ambayo anawafanyakazi na haitaji tena yy kuwepo ili iendelee, na pia kuna nyingine ya dada muuza miguu ya kuku na yy katengeneza mfumo ambao hamuitaji yy kuwepo. Bottom line: ni matumizi mabaya ya elimu kuendesha bajaji kwa level ya master huo ndio ukweli mchungu ila watu lazima waambiwe hiyo ni level ya kuunda biashara zinazojitegemea
 
Asante kwa maoni yako Nicklaus
 
Shukrani Mersen kwa maelezo
 
Hapo uenda ana nyumba yake.
Na vimradi vingine hatuwezi jua.
Ila kwa siku kuingiza elfu 50.
Ni hela nyingi sana.ni zaidi ya kuajiriwa.
Kama atakuwa na hivyo vitu ulivyotaja tayari basi si haha maisha yaenda murua kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…