Wasomi jifunzeni kwa dada Mwasu, dereva wa bajaji msomi mwenye shahada mbili

Je ! Ni wasomi wangapi wana vyeti vizuri vya elimu juu, lakini wanapata taabu sana baada ya kukosa ajira na hata pesa ya kununua wembe nk ?
Na ndiyo point yangu mkuu. Tunahimiza kundi kubwa lichukue taaluma fulani wakati mahitaji ya wenye taaluma hiyo ni madogo.
Mwisho wa siku una miaka 24 na cheti chako, af unaambiwa start small, wakati ungeanza small ukiwa na miaka 13 sa hivi ungekuwa sugu wa kitaa.
 

Elimu ya Tanzania kwa sasa imebadilika.
Yaani kwa sasa ni kusoma kuongeza elimu tu(Kua na vyeti vingi).
Kuhusu swala la ajira kwa sasa ni kujikita kwenye fani tu.
Yaa inatakiwa ukisoma ualimu jiandae kuwa muuza mafuta sheli.
 
Na hili gazeti la mwananchi wanafeli sana, badala ya kutuletea emerging youth billionaires watu wawe inspired, tunarudishana kwenye udereva wa bajaji
Au kutuletea emerging innovations in Tz..! Magazeti yetu ya bongo yanatuangusha sana!!
 
Huyo kaamua kuwa kioja kwenye jamii.

Aingie kwenye fani ya vioja na vituko huko bongo movie atapiga hela
 
Haikuwa na maana kupoteza muda na fedha kugharamia elimu mpk shahada mbili af uishie kuwa dereva Bajaji,sbb ata bila elimu hyo angeweza kuendesha. Nafikir kaz hyo sio ndoto yke ila anafanya 2 ili kukidh mahtaji,Hvo si mfano wa kuigwa coz ukimuiga huyu unaiga hasara kwa familia.
 
Huwezi jua kwa nini anangangania Biashara ya Bajaji, mengine hawezi sema...




Cc: mahondaw
 
Kuajiriwa Tanzania ni sawa na kupata mkopo 100% wa chuo kutoka bodi ya mikopo helsb
 
Maoni tumeyasoma. Asante !
 
Ujiajiri kupitia taaluma yako mbona changamoto ni nyingi?

Si akafungue hta tuition basi hapo kitaa!!

Mie nlipomaliza chuo nilijiajiri ila kupitia taaluma yangu nikawa nafundisha wanachuo wapya, naandika tafiti, naandaa business plans, docx za negotiation n.k so bado nilikua eneo langu nililosomea.

Sasa imagine mimi na Msc ya Uchumi niendeshe bajaj, Y nilienda shule?
 
Hivi katika dunia ya utandawazi unalaumu mfumo wa elimu huku utandawazi unakupa chance ya kujifunza chochote kilicho kosekana kwetu? .
Good sababu siongei as an individual bali kwa ajili ya majority.

Nadhani unapoongelea utandawazi unaamanisha internet ambayo yote yaliyokesana kwenye elimu yetu yapo huko.
Mimi ninayo access.

Question: now can you tell wanafunzi wangapi wa kitanzania wana access ya internet?
Namaanisha wanafunzi wote Tanzania haijarishi ni primary, secondary ngazi za juu kabisa.

Ukiacha wasio na access wenye access hawatumii huo utandawazi kujifunza bali kujiharibu bila kujua.


halafu to a mbadala elimu iboreshwe nini sio lawama tu.
Lawama ni dalili ya kushindwa.
Mkuu mbadala wa elimu nishatoa sana.


Pia nina imani hiyo serikali inajua inachokifanya kama itaamua kubadilisha mfumo.
Hivi umetafiti kuwa mfumo wa elimu yetu haufanani na nchi zingine?
Unadhani mfumo tunaoutumia sisi unafanana na nchi zote?
 
Aisee ni naona sio kitu cha kujivunia ila ni ufinyu wa upana wa elimu yetu.
Masters then unaendesha bajaj ni sawa kwa ajili ya kipato ila sio kujivunia na kuwa front page.
 
Si akafungue hta tuition basi hapo kitaa!!
Mkuu unadhani kila binadamu ana mipango sawa na mwingine kwenye maisha yao?
Unajuaje kwamba hana idea kubwa ya kufanya kitu kikubwa baada ya kuwekeza?
Sasa imagine mimi na Msc ya Uchumi niendeshe bajaj, Y nilienda shule
Mkuu unajua kuhusu chimbuko la Facebook?

Mkuu hakuna kitu simple yaani unaibuka tu tayari una company.
Mie nlipomaliza chuo nilijiajiri ila kupitia taaluma yangu nikawa nafundisha wanachuo wapya, naandika tafiti, naandaa business plans, docx za negotiation n.k so bado nilikua eneo langu nililosomea.
That's why nikakuuliza unadhani kila binadamu ana mipango au ndoto sawa na mwingine?

Unajuaje kama anataka kufungua company mfano wa uber ile yeye anatumia bajaj instead sababu bajaj inatumika zaidi maeneo ya mitaani.
Unajuaje hana hiyo idea?

Ungemuona sahihi kumiliki company ya bajaj ila chimbuko lake hulijui na akikwambia chimbuko lake utakataa?
 
Hata Rais John Magufuli wakati anasoma, hakuwa na ndoto ya urais kama wengine ... ! Alichukua PhD kuongeza elimu si kipato.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…