Wasomi jifunzeni kwa dada Mwasu, dereva wa bajaji msomi mwenye shahada mbili

Si akafungue hta tuition basi hapo kitaa!!
Can you tell kipi bora kati ya kufungua tuition na kumiliki company ya bajaj mfano wa uber?

Unadhani how much atatengeza kutoka kwenye company hiyo ambayo itakuwa inafanya kazi Tanzania nzima?

6 million per day or 50 million per day tsh?

Now kati ya yeye na wewe nani ungemuona yupo sahihi?
 
Mkuu tusitafute justification.... Wote waliotoboa walifanya vitu vilivyopo kwa namna tofauti.

Mfano angeingia dili say na wasafi ili waziite ''Wasafi Xpress'' so bajaji zake zinakua na brand kubwa na zingesafirisha mpka A list.

Ssa kuona mtu ana masters alafu anaendesha biashara kwa style ile ile iliopo na doubt elimu yake.

Huyo kma ana M.A basi ni zile za kubebwa ila content hana kichwani. Anatudhalilisha wasomi
 
"UDOM ni chuo cha vilaza"....in Magu's voice.
Kwa kweli mkulu hakukosea kuwaita vilaza Kama output za chuo hicho ndo type hii ya kina Mwasu
 
Afungue UBER wakati bajaj anayotumia hta rangi tu no kma zilizopo mtaani? Ameshindwa hta customization na product differentiation ndio aweze franchising kma UBER?

Mimi niliwahi fungua biashara huko nyuma ila kwakuwa sikua na mtaji nkaongea na superstar mmoja yye akawa ndio kma mmiliki ila mwisho wa siku alikua kivuli tu. So yye akawa kma ananiletea wateja mie naingiza pesa. Hapo ndio unaona elimu ilifanya kazi sio upuuzi wa kuendesha bajaji!!

Hvi tunaelewa Masters ni nini? Ada tu million 6-8 alafu ukaendeshe bajaj? Matatizo ya taaluma yake yote yana ufumbuzi?

NB: Kina zuckeberg unaowatolea mfano walijiajiri kupitia Taaluma zao. Sio zuckeberg alisomea IT alafu akaendeshe malori ni upuuzi
 
Mkuu tusitafute justification.... Wote waliotoboa walifanya vitu vilivyopo kwa namna tofauti.
Sitafuti justification bali ni ukweli.

Kwamba kama mtu ni masikini basi huwezi kufika popote bila kuanzia chini.

That's why kuna wapenda shortcut au wote wanakimbilia ajira.
Ssa kuona mtu ana masters alafu anaendesha biashara kwa style ile ile iliopo na doubt elimu yake.
Unaweza ukaniambia kuna wasomi wangapi Tanzania walio apply elimu zao ukiondoa waliopata ajira.

If hujui wangapi mention majina yao then uangalie chimbuko lao.
 
Naomba namba yake awe anakuja kunichukua huku Koromije na kunipeleka Dom wakati wa mikutano ya bunge.
 
Mie nawafahamu wawili ni wasomi wa M.A mmoja Godwin mwingine Winnie. Hawajaajiriwa ila wame design products mwingine App mpya kabisa sokoni. Na wana progress nzuri.

Hao ndio ilipaswa mwananchi iwahoji maana wamejiajiri kusolve matatizo ya sekta zao sio kuendesha bajaji. Ni kudhalilisha elimu ya Masters

UDOM wamfutie hyo award.... Haiwezekani shida za sociology na administration hazijaisha alafu anaendesha bajaji!!!
 
Huu upumbavu inabidi tuuache mwaka huu 2020 huko tuendako tutaanza kuwazaba makofi mtu yoyote anaewaambia wasomi kuwa wakajiajiri.

Hivi mtu asome miaka yote zaidi ya 15 halafu uje umletee upuuzi wa kuwa ajiajiri, hiyo taaluma alisomea ya kazi gani?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Afungue UBER wakati bajaj anayotumia hta rangi tu no kma zilizopo mtaani? Ameshindwa hta customization na product differentiation ndio aweze franchising kma UBER
Unadhani kwanini asiweze?
Mkuu wewe hautoshi kujitolea mfano ndani ya graduates karibu mill 6 hauwezi fika hata asilimia .05.

Still narudia hamuwezi kufanana mipango na mwingine hata kama muwe na elimu sawa au elimu ya shule ilifundisha kuongea na superstars kama hauna mtaji?
Kina zuckeberg unaowatolea mfano walijiajiri kupitia Taaluma zao. Sio zuckeberg alisomea IT alafu akaendeshe malori ni upuuzi
Yeah ila Zuckerberg hakuibuka tu na company from nowhere.

And nani amekwambia Zuckerberg amesomea IT
Wakati hata chuo hakumaliza?
 
Mie nawafahamu wawili ni wasomi wa M.A mmoja Godwin mwingine Winnie. Hawajaajiriwa ila wame design products mwingine App mpya kabisa sokoni. Na wana progress nzuri.
Would you tell me walianzaje bila mtaji?

Let me ask you a question.

Imagine wewe ni mtoto wa masikini au ni masikini as huyo dada pia umemaliza chuo na elimu yako let say una economics degree na una plans za kumiliki company kubwa ya usafiri.

Wewe ungefanya nini kwenye situation kama hiyo?
 
Mawazo ya kijinga kabisa, hivi hiyo bajaji ndicho alichosomea??? Kwa nini anaingilia kazi za watu???? Hivi tofauti ya aliyesoma na asiyesoma ni kitu gani??? Kwa nini asingetafuta namna ya kutatua changamoto za jamii kulingana na alichosomea???? Idiot kabisa huyu msomi. Vyuo vinahitaji kujitransform toka kutoa digrii za makaratasi mpaka problem solver kuliko hawa wanaokariri eti kuuza karanga ni kujiajiri.
 
Tujifunze nini sasa? Toa ujinga hapa.
Hatukusomea kuendesha bajaji sisi.
Yeah Hukusomea kufungua company.

Like mwenye uber hakusomea udereva taksi just like you.

Now unajua yuko wapi?
No you don't yeye aliona miaka kadhaa mbele.

Bila shaka wakati anaanza ungekuwa una mmock just like this.
 
Mkuu unadhani mmiliki halali wa uber alisomea udereva taksi?
 
Mwisho wa siku Ni kuwa na pesa haijalishi background yako Ni ipi

Kama unaingiza pesa kwangu Mimi is okey sijali unaingizia juani au kwenye AC
 
Mkuu unadhani mmiliki halali wa uber alisomea udereva taksi?
Yeye alileta suluhisho la upatikanaji wa usafiri kwa bei nafuu na pahala popote, na huo ndiyo usomi, na usomi wa kuelewa namna ya kutatua changamoto haijalishi umesomea kitu gani. Hivyo huyu mdada na li bajaji lake hajatatua tatizo la jamii zaidi ya kuwa sawa na wale hawajaenda shule, afikirie mara nyingi contribution ya elimu yake kwa jamii.
 
Wewe unafanya kazi ?

Serikali inaweza kukusomesha lakini haikupi guarantee ya kazi

Kama ndio unafanya kazi ukifukuzwa hapo unaweza survive hata mwaka mzima ?

kumtukana mtu anayeingiza Senti zake kihalali Ni ujuha

Ukitaka aende kudanga? na kujidhalilisha ?

Mpe moyo anaweza kua kiuchumi na kesho na kesho anaanzisha big business

'started from the bottom"-drake

[emoji123][emoji123][emoji123]
 
Ameajiri wangapi baada ya yeye kujiajiri?
 
So unadhani aliibuka tu from nowhere na company kubwa namna vile?

Unajua company ya uber ilipoanzia?
usomi wa kuelewa namna ya kutatua changamoto haijalishi umesomea kitu gani
Mkuu dk chache nyuma uliandika hivi
Mawazo ya kijinga kabisa, hivi hiyo bajaji ndicho alichosomea??? Kwa nini anaingilia kazi za watu???? Hivi tofauti ya aliyesoma na asiyesoma ni kitu gani??? Kwa nini asingetafuta namna ya kutatua changamoto za jamii kulingana na alichosomea????
Kwamba anafanya kitu ambacho hakusomea now unajicontradict mwenyewe kwamba kutatua changamoto za jamii haijarishi umesomea nini.

Ina maana huna uhakika na unachokiandika?

That's why nimekuuliza kwani mmiliki wa uber alisomea udereva taksi?

Na je huyo mmiliki wa uber aliibuka tu na hiyo huge company from nowhere?

Je unajua uber ilivyoanza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…