Wasomi wa karne hii ni vilaza, wanabebwa na vyeti vya chabo kuliko taaluma halisia

Wasomi wa karne hii ni vilaza, wanabebwa na vyeti vya chabo kuliko taaluma halisia

Habarini wana JF,

Nipo kazini katika office mojawapo hapa duniani.

Bhasi hivi karibuni wamekuja watoto wa field katika vyuo fulani vikubwa sana hapa Tanzania.

Vijana ni warembo na watanashati. Basi katika kuwaweka katika vitengo husika ili wajifunze utendaji, niliogopa vijana wa degree wanashindwa kuwasha computer, graduate hajui kutumia mouse ya computer au mouse ya laptop.

Graduate hajue MS Word, Excel vitu ambavyo ni rare na ni common kujua

Graduate awezi ku-type kitu na ku-save vizuri.

kuanda tu CV au kutuma application online ni kazi sana

Hali ni mbaya sana na sasa hivi interview kama za mabenki huwa mnafanya online kwa muda maalumu then una submit matokeo unapata. Hapo hapo je mtawezana na technolojia?

Naomba tuimbe wimbo wa taifa ubeti wa kwanza.
Mkuu mim nimesoma IT lakin cha ajabu nilijua kuiwasha kompyuta kipindi nipo chuo hii ilitokana na familia niliyotoka mkuu kwaiyo usishangae sana.
 
Ki Ukweli kabisa, Ukweli kabisa, hii nchi tunahitaji Mjadala wa Hatma ya Elimu yetu kama alivyowahi kuusia Big Ben. Hali ni mbaya mno huku mtaani, tena mbaya zaidi na huu uandishi wao wa 'x badala ya s'. Wanachokijua sana ni kubana sarawili zao na kuvaa viatu vya kung'aa
 
BADILISHA EDUCATION SYSTEM.

well huwezi kujua kitu ambacho hukijui.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Zabron amem 'mock' mtoa mada, OP ndiyo aliyeandika 'mouth', mtoa mada aka edit fasta, japo bado ipo kwenye quote
Na nilijua atafanya editing ndio maana nikafanya kuquote ili asijejikuta Newton. Anaponda wsdiojua kutumia computer wakati yeye kuandika hajui.
 
kama computer yenyewe ni Fiji mnategemea nini unaweza kudhani unawasha kumbe unaongeza sauti
 
Nilikuwa nasikiliza katibu kiongozi akisoma majina ya walioteuliwa uwaziri na manaibu wao. Nilichoka ule mvurugano wa majina aliyokuwa akisoma. Wengine kama Jafo, alitaja jina la kwanza Selemani na kuishia la mwisho. Ila wengine akaanza la mwisho mfano Pinda anaishia la mwanzo Mizengo. Na mvurugano uliendelea hivyo hivyo, ikitokea mtu unajua ndio nafuu, la sivyo ni mpaka uchambue hapa jina la kwanza ni lipi na la ukoo ni lipi?
Nilijiuliza huu utovu wa umakini wa kila jambo katika nchi hii una dawa kweli?
 
Hoja yako haijakaa vizuri. Ndo mana ata vyuo vinatoa miez miwili adi mitatu wanafunz waende kijifunza waliyosoma kwa vitendo(field).

Mwanafunz aliyetoka chuo ambaye ajawa experience ya kaz ndo Mara ya kwanza kuwa ofisn kwanza atakuwa na uwoga flan kazin kabla hajazoea, kingine hawez kujua kila kitu kinavofanyika ndo mana hupuwa msimamiz wake(instructor), ambaye kazi yake kumwelekeza na kumsaidia anapokwama au akiwa na shida.

Field ni kwajili ya kujifunza na kupata uzoefu wa kazi. Ungefanya jambo la maana kama ungewasaidi pale wanapokwama..
soma uzi vizuri wewe umebase kwenye field tu
 
Mkuu mim nimesoma IT lakin cha ajabu nilijua kuiwasha kompyuta kipindi nipo chuo hii ilitokana na familia niliyotoka mkuu kwaiyo usishangae sana.
iyo IT uliyo soma imekusaidia nini
 
Ki Ukweli kabisa, Ukweli kabisa, hii nchi tunahitaji Mjadala wa Hatma ya Elimu yetu kama alivyowahi kuusia Big Ben. Hali ni mbaya mno huku mtaani, tena mbaya zaidi na huu uandishi wao wa 'x badala ya s'. Wanachokijua sana ni kubana sarawili zao na kuvaa viatu vya kung'aa
well
 
Back
Top Bottom