Ume copy na paste maneno sijui yametoka wapi!?
Katika uislam Allah hakutufundisha kueneza dini kwa mapigano,bali katuhimiza KUITETEA DINI YAKE.
Ukisema kueneza dini kwa Upanga inamaana ni sawa na kulazimisha dini.
Na ARTICLE YOTE ULOLETA inapingana na Qur'an 2;256.
View attachment 2998930
Jihad maana yake ni kufanya jitihada eidha kwa nguvu au pesa.
Na katika jihad kuna jihad ya mali na vita.
Na sheria za Jihad ya vita ni zifuatazo;
1)Hakuna kuua wanawake,watoto na wazee.
2)Hakuna kuharibu mji.
3)Hakuna kuharibu mali,mazao,miti.
4)Hakuna kupigana na asiyeshika silaha.
Asa unaposema dini imeenezwa kwa Upanga inamaana kila mtu alishikiwa panga na kuulizwa kama amekubali uislam au laaah,huo ni uongo.
Jiulize maswali haya mawili ana ulete majibu;
1)Kama uislam umeenezwa kwa upanga kwanini Muhammad aliruhusu mkataba na wayahudi??
2)Kama uislam umeenezwa kwa upanga kwanini Muhammad aliweka mikataba na WARUMI(ROMAN EMPIRE)?
3)Kama uislam ulienezwa kwa upanga kwanini kipindi waislam wanateswa Mecca Mungu aliwakataza wasipigane ila aliwaamuru wahame??
Endeleeni kuokota articles za uongo.