Waswahili bwana yaani Treni ya SGR Dar hadi Moro ni masaa 2 na dakika 20 mnafurahi na kushangilia!

Waswahili bwana yaani Treni ya SGR Dar hadi Moro ni masaa 2 na dakika 20 mnafurahi na kushangilia!

Mimi nilikuwepo jana tulitumia dk 90
Kwahiyo Waandishi wa Habari wote ( Media ) zote na hata Magazeti ya Leo yaliyosema / yaliyoripoti kuwa Safari ya Majaribio ya Treni ya SGR jana kutoka Dar hadi Moro ni Saa 2 na Dakika 20 Wametudanganya na tukuamini Juha Mwandamizi Mmoja Wewe?
 
shida ndio inaanzia hapo, tupo sisi wengine ambao tumeishi na huo ndio umekuwa usafiri wetu kwa miaka mingi tu, na mpo ninyi kama wewe ambao mnajifunzia kwenye internet. ndio maana mnaongea ujinga mtupu. hizo treni zipo za speed tofauti hata huko ulaya, chukua mfano tu Ujerumani, Ufaransa, Italia ambako ni nchi kubwa kubwa na zina usafiri huo sana, zipo treni zinaanzia 155kmh, na zipo zingine zimefika hadi 300kmh. yaani kwa lugha nyingine, hii aina ya treni tuliyonayo sisi hapa hata ulaya zipo na bado zinatumika kwenye SGR zao. sasa shida ni pale mnataka watuletee 300kmh train wakati hata hiyo ya speed ndogo hamjawahi kuwa nayo. kwani shida ni nini? kama tayari miundombinu ya reli mmeshajenga, si jambo la kununua tu za speed mnayotaka? hiyo reli ni barabara ya train kama hujui, za speed zote zitapita kama mtakuwa na hela kununua za speed hizo. kwahiyo kwenye barabara la lami toka dsm hadi moro ikipita lori la speed 80kmh haiwezi pitisha V8 la speed 200kmh?
1709027321556.png

Source: Fastest Train In Africa: Lagos Is Number One - Politics - Nigeria
 
Kwa umbali huo muda ulitakiwa uwe ni dakika 60 au 75 tu kama ambavyo inafanyika katika Mataifa mengine makubwa ya watu wenye akili na yaliyoendelea.

Yaani Dar hadi Moro zimetumika Saa 2 na dakika 20 halafu mazuzu tokea jana na leo inashangilia tu wakati kwa wenye hizo Treni za SGR katika Mataifa mengine wanaotumia Saa 3 tu kwa umbali wa mfano wa kutoka Dar es Salaam hadi Singida wanatucheka na kutudharau mno.

GENTAMYCINE nikisikia au niliambiwa Treni ya SGR itatumia saa 2 na dakika 30 au hata na dakika 45 kidogo nitaona imefanikiwa ila hili la kutoka Dar hadi Moro kutumia Saa 2 na dakika 20 naona ni Kufeli kwa Mradi na Mpango kwa Maendeleo ya Taifa, Muda na Uimarishwaji wa Uchumi wa Tanzania na Watanzania.

Haya Team Kusifu Upuuzi na Wanafiki karibuni sana katika Kunipinga ili mlipwe Buku Saba Saba zenu, mlambe Uteuzi na Maisha yaendelee ila wenye Akili Kubwa na tusiopenda Upuuzi na Unafiki ndiyo tumeshafunguka.
Wewe kenge ndo mana walisema hayo ni majaribio na wakaweka na mabehewa machache kuona je kilichojengwa kinaendana.
 
SGR sio zile train za mwendo kasi kama bullet train ya japan, train à grande vitesse (TGV) ya ufaransa au zile train za mwendo kasi za china. Hizo ni train za speed kali 300 km/saa au zaidi. Hii yetu ni reli ya SGR. Mwendo wa juu kabisa ni kama 160 km/ saa. Kwa kulinganisha utalinganisha na ile SGR ya kenya. Speed zitapitana kutegemea na mtengenezaji wa engine labda na mabehewa.
Sijui ni lini Wapumbavu mtaisha Tanzania.
 
Ukitaka kujua hii project imevamiwa na majitu yasiyo na exposure ya Maisha ya kisasa yaliyopo serikalini jiulize tokea lini bullet train ikawa na Hostess (wahudumu wa kike) on board?

Sehemu ya kwenda dakika 60 hadi 75 ina haja gani ya wahudumu, hiyo si ni kuongeza tu gharama za uendeshaji wa kampuni na kuibia serikali?

Bullet train [emoji583] ya kisasa yenye mwendo usiopungua 350km/h kutoka hapa Dar hadi hapo Morogoro ni sawa na abiria wa daladala ya kawaida kutoka tegeta kwenda posta so sidhani kwa muda huo na kasi hiyo unahitaji kuwa na wahudumu wa vinywaji, chakula sijui na vitu gani maana hata chooni kwenyewe unaweza sikilizia kwenda.

Hebu tuwe tunatazama wenzetu wenye hii mifumo wanaishi vipi ndipo tutaweza kuona hawa wanaojinasibu kuwa wamepiga kazi hakuna ambalo wamefanya.
GENTAMYCINE napenda sana kukutana na Great and Critical Thinkers wa aina yako hapa JamiiForums ila kwa bahati mbaya mno hampo wengi ila Mijuha ( Mipumbavu ) ndiyo imejazana na Kutwa tu Kazi yao ni Kusifu na Kupamba.
 
Hapa tunazungumzia ni majaribio...Hauwezi kimbia kwa speed inayotakiwa kwenye sehemu ambayo haujafanyia majaribio kuona je kila kitu kiko sawa hasa hayo mataluma na hizo waya za umeme.
Wahaya ( Watani zangu Wakubwa Mzanaki Mimi ) huwa wana Akili ( Werevu ), Wewe ni Mhaya gani Juha ( Fool ) kiasi cha Kusikitisha hivi?
 
Back
Top Bottom