Waswahili bwana yaani Treni ya SGR Dar hadi Moro ni masaa 2 na dakika 20 mnafurahi na kushangilia!

Waswahili bwana yaani Treni ya SGR Dar hadi Moro ni masaa 2 na dakika 20 mnafurahi na kushangilia!

SGR sio zile train za mwendo kasi kama bullet train ya japan, train à grande vitesse (TGV) ya ufaransa au zile train za mwendo kasi za china. Hizo ni train za speed kali 300 km/saa au zaidi. Hii yetu ni reli ya SGR. Mwendo wa juu kabisa ni kama 160 km/ saa. Kwa kulinganisha utalinganisha na ile SGR ya kenya. Speed zitapitana kutegemea na mtengenezaji wa engine labda na mabehewa.
Kama treni inatumia masaa 2:30 na basi masaa 2 au 2:30 si bora upande gari tu.
Umeme wenyewe wa mgao
😀😀😀😀😀
Labda bei iwe ndogo kuliko za mabasi
 
Kweli lazima wasifie ,Nakumbuka Maulid Kitenge alituonyesha Treni ya umeme alivyokuwa nchi za watu huko dashboard ilikuwa inasoma around 420Km/hr ,hii ya kwetu mwendo wa kobe.
Hizo zinaitwa express train hazisimami simami ni kama ndege za direct flight

Train zone za mwendo kasi zaweza kuwa na hizo spidi lakini kama ina vituo vingi vya kusimama huwezi kwenda kwa spidi hiyo
 
Nigeria, morocco na misri wanazo za mwendo kasi sana. na miundo yake ni ile ile ya majuu, ila hii 3rd class ya kadogosa sijui ameokota wapi, hadi aibu.
Tatizo kubwa litakuwa kwenye uendeshaji wenye ufanisi kwenye hilo shirika. Mchwa ni wengi sana, yaani baada ya miaka 10 tutakuwa hoi bin taabani, tutabaki kulipia mikopo yenye hasara tupu.
 
Hizo zinaitwa express train hazisimami simami ni kama ndege za direct flight

Train zone za mwendo kasi zaweza kuwa na hizo spidi lakini kama ina vituo vingi vya kusimama huwezi kwenda kwa spidi hiyo
Na ndio maana huwa kuna kuwa na Express yaani ni Dar to Moro non stop (bei juu), halafu inakuwepo ya akina sisi kila kituo ni breki (bei chini)
 
Kwa umbali huo muda ulitakiwa uwe ni dakika 60 au 75 tu kama ambavyo inafanyika katika Mataifa mengine makubwa ya watu wenye akili na yaliyoendelea.

Yaani Dar hadi Moro zimetumika Saa 2 na dakika 20 halafu mazuzu tokea jana na leo inashangilia tu wakati kwa wenye hizo Treni za SGR katika Mataifa mengine wanaotumia Saa 3 tu kwa umbali wa mfano wa kutoka Dar es Salaam hadi Singida wanatucheka na kutudharau mno.

GENTAMYCINE nikisikia au niliambiwa Treni ya SGR itatumia saa 2 na dakika 30 au hata na dakika 45 kidogo nitaona imefanikiwa ila hili la kutoka Dar hadi Moro kutumia Saa 2 na dakika 20 naona ni Kufeli kwa Mradi na Mpango kwa Maendeleo ya Taifa, Muda na Uimarishwaji wa Uchumi wa Tanzania na Watanzania.

Haya Team Kusifu Upuuzi na Wanafiki karibuni sana katika Kunipinga ili mlipwe Buku Saba Saba zenu, mlambe Uteuzi na Maisha yaendelee ila wenye Akili Kubwa na tusiopenda Upuuzi na Unafiki ndiyo tumeshafunguka.
Wengine tulitegemea kuhamia moto sababu tunavijumba huko ili asubuhi tuwahi mishe zetu Dar sasa kama sehemu fupi hivyo masaa mawili si balaa hiyo?tunarudi tena kwenye stone age
 
Kwa umbali huo muda ulitakiwa uwe ni dakika 60 au 75 tu kama ambavyo inafanyika katika Mataifa mengine makubwa ya watu wenye akili na yaliyoendelea
Mataifa mengine Makubwa! STOP! Taifa letu nalo ni kubwa? Asante sana kwa kutupaisha.

Issue ya Marehemu Nkono na mwanae Rea ilinifanya mimi niache kusoma kabisa matoleo ya GENTAMYCINE, hasa pale ambapo yule mzee mstaafu wa CCM alipotoa maelezo. Mzee alisema, kuchelewa kuletwa mwili wa Marehemu Nkono toka USA mpaka Tanzania ni sababu za usafirishaji na document tu na si kama mitandaoni (aka Gentamycine) inavyoelezwa.

Leo, nimejikwaa kupitia andiko lake.... Hata hivyo sina coment.
 
wabongo mnalalamika hatari.

Shida mnataka train kama za Japan wakati kodi zenyewe mnakimbia kulipa.
Ukiwaeleza watoe TOZO, hata barabarani watakwenda. Nyie ni watu gani? Wabongo achana nao tu, wamezoea vya bure. Ndio maana wanasema MATAIFA MAKUBWA......
 
Tanzania hyperloop completes first test runs, pushing ahead in race for ultra-fast land transport. Pod travels at 50km/h (31mph) through vacuum
 
Yaani treni itembee kwa speed ya 160/170 km/h kwenye reli hizi ambazo wabongo hawachelewi kuvusha ng'ombe na mbuzi....si unataka kusababisha maafa?
 
Mimi sio mshabiki wa vyama vya siasa ila tu wale wakosoaji sijui kama wanafahamu maana ya neno majaribio.TRC walitoa taarifa yao hapo jana kuwa walikuwa wakifanya majaribio zaidi ya Nane katika treni hiyo na bado wanaendelea kufanya majaribio kwa kila kifaa kitakacholetwa kwa ajili ya treni hii mpaka pale watakapojiridhisha kuwa mradi upo salama kwa usafirishaji wa watu na mali zao.
 
Back
Top Bottom