Waswahili bwana yaani Treni ya SGR Dar hadi Moro ni masaa 2 na dakika 20 mnafurahi na kushangilia!

Waswahili bwana yaani Treni ya SGR Dar hadi Moro ni masaa 2 na dakika 20 mnafurahi na kushangilia!

Walikwisha jaribu mara ya kwanza bila abiria hii ni mara ya pili.
Ili chombo kiende kasi ni lazima kiwe na umbile (mchongoko) litakalokiwezesha kupenya kwenye upepo bila msuguano mkubwa, kichwa cha treni ya jana kinapingana na upepo na kusababisha msukumo mkubwa unaopelekea nguvu kubwa kutumika na kusababisha umeme mwingi kutumika.
I agree [emoji817]
 
Walikwisha jaribu mara ya kwanza bila abiria hii ni mara ya pili.
Ili chombo kiende kasi ni lazima kiwe na umbile (mchongoko) litakalokiwezesha kupenya kwenye upepo bila msuguano mkubwa, kichwa cha treni ya jana kinapingana na upepo na kusababisha msukumo mkubwa unaopelekea nguvu kubwa kutumika na kusababisha umeme mwingi kutumika.
Hii si lazima. Ferrari limechongoka?
Pikipiki cc 750 imechongoka?

Tuangalie na ubora wa dereva,njia,nk
 
Nikajua watu wa JF wana uelewa mkubwa kumbe nao kama wa mtaani kwangu tu nacheka comment tu ,au ndio kawaida ya wabongo kila kitu wanajua
 
nimepanda treni mara nyingi sana nchi za mbele, tena zenye speed kama hii ya kwetu 160kmh. though zipo hadi zenye 300kmh lakini kama hii ya kwetu zipo. wengi wanaojadili hapa, ndio wanaanza kuiona treni ya aina hii leo na wanaongea kwelikweli.
Treni zipo huko nje,U- Bahn mjerumani masaa 8 ye matatu mshafika
Iinakimbia km new force au sauli na halisimami popote ni mji kwa mji tu.
 
Nasubiri wabadili jina jina kama mradi wa mabasi toka mabasi ya mwendo kasi hadi mabasi yaendayo haraka
 
Kwa umbali huo muda ulitakiwa uwe ni dakika 60 au 75 tu kama ambavyo inafanyika katika Mataifa mengine makubwa ya watu wenye akili na yaliyoendelea...
Kwa mwendo huo, Mwanza litafika saa moja au saa mbili usiku. Bora kupanda bus tu.

Halafu nauli pendekezwa Morogoro ilikuwa 27,000 na ushee. Bora kukomaa na Abood kwa maana hiyo.
 
Kwa umbali huo muda ulitakiwa uwe ni dakika 60 au 75 tu kama ambavyo inafanyika katika Mataifa mengine makubwa ya watu wenye akili na yaliyoendelea...
Mkuu huo muda wa SGR wa masaa mawili dar-moro ulitumiwa na mabasi ya enzi 90s tena mengine yakifika msamvu masaa mawili kasoro,sasa hizi drama za kushangilia mawili+ tena katika zama hizi ambazo technolojia ikò juu ni uzwazwa.Waliowahi kusafiri na matema, zainabu, masia, tawaqal, Ilangamoto, luckstar, kiswele....wanawashangaa.
 
umbali wa reli au barabara? hapo ndipo mnapochanganya. pili, kama basi linachukua masaa 3.5 hadi moro, treni ikichukua 2.20 si mshukuru? hata hapo mnashindwa kujipongeza kweli?
Kivip kwa hiyo jam na speed governor zimewekwa kwa ajili ya kiki za kisiasa?hatutashangilia huo ujinga kama mshangiliavyo misafara ya watawala.
 
Kuwa lengo lenu Kuu la hii Treni yenu ya SGR ni Kusafirisha hasa Mizigo na Abiria ni kama Bonus tu ya Huduma.

Halafu nikiwadharau mnanichukia!!!
 
kamwulize kadogosa mzee, unatuuliza sisi kwani ndio wakandarasi tulioijenga, upande wetu sisi tunafurahi tu kwamba kumbe tunaweza kusafiri hadi moro kwa 2:20 hours badala 3 t0 4 hours za mabasi, tena mabasi yenyewe ujue yanakimbia mno kwa muda huo. binafsi nafurahi, ninachopinga ni value for money, mabehewa hayo sio ya kisasa kabisa, na yawezekana yalitupwa huko walikochukua. hata south korea walikochukua hawatumii kama hayo. kwa lugha nyingine hili ni ngalangala linalokimbia, sio treni ya kisasa hata tukiwa nje ya nchi kwa wenye treni wakisema wenye treni za kisasa hatutakiwi kunyoosha mkono kabisa.
Sawa kabisa. Haya yote kamweleze Kadogosa mzee.
 
Kwa speed hiyo kama ni kweli, huu utakuwa ni mradi uliofeli kabla haujaanza kufanya kazi....
Itoshe tu kusema nyie watz ni watu wapumbavu sana sana........yaani linater moja likileta taarifa zake mnadandiadandia tu hovyo hovyo. Sasa kitu ni majaribio mkitakaje?!!!
 
Hilo treni la umeme linabugia umeme mwingi mpaka mwanza na kurudi dar trc wataweza kulipa hizo gharama ikiwa nauli itakuwa ndogo? Na nauli ikiwa kubwa wasafiri itabidi waendele na mabasi tu
 
Back
Top Bottom