Wataalam wa kilimo naomba kujua madhara ya dawa ya kuua magugu shambani

Wataalam wa kilimo naomba kujua madhara ya dawa ya kuua magugu shambani

Kwahiyo kama nimeshapanda zao siwezi kutumia dawa hii?
Kama umeshapanda unatumia isipokuwa mpaka upate ushauri wa kitaalamu dukani utakapoenda kununua dawa hiyo kwa kutaha zao ulilokwisha lipanda.

Dawa hizo kwa palizi zimegawanyika katika aina mbili, tena usiwe umechanganya mazao kwenye shamba moja.

Kama ni mpunga ama mahindi, zipo zinazoua magugu jamii ya kunde(dico'...) na kama umepanda karanga ama kunde, zipo za kuua magugu jamii ya nyasi (monoco'...).

Cha msingi uwe na bomba la kunyunyuzia lenye ujazo wa ltrs 16-20, utamaliza kazi fasta.

Wahi mkuu, madawa hayo yamejazana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo kila sehemu.
 
Uku tunalima maemari ya ufuta ni mwendo wa kupuliza tu. Tena tunachanganya na mbolea ili kupata matokeo mazuri
 
Kama umeshapanda unatumia isipokuwa mpaka upate ushauri wa kitaalamu dukani utakapoenda kununua dawa hiyo kwa kutaha zao ulilokwisha lipanda.

Dawa hizo kwa palizi zimegawanyika katika aina mbili, tena usiwe umechanganya mazao kwenye shamba moja.

Kama ni mpunga ama mahindi, zipo zinazoua magugu jamii ya kunde(dico'...) na kama umepanda karanga ama kunde, zipo za kuua magugu jamii ya nyasi (monoco'...).

Cha msingi uwe na bomba la kunyunyuzia lenye ujazo wa ltrs 16-20, utamaliza kazi fasta.

Wahi mkuu, madawa hayo yamejazana kwenye maduka ya pembejeo za kilimo kila sehemu.

Asante sana mkuu.
 
Nachojua ni kwamba Kuna Baadhi ya dawa zinakaa shambani mwaka mzima so Huwa ni hatari kwenye crop rotation eg dawa za palizi ya zao y linaweza UA zao K msimu mwingine
Kama dawa zipi ? Maana dawa zote zina class na zinatumika wapi hivyo ndo nachoelewa pia THPH ndo wanaruhusu hilo . Kuna dawa zipo kwenye matumizi ya makampuni tu uwezi zikuta maduka ya kawaida
 
Side effects za pesticides zipo. Lakini kwa kilimo cha sasa, hasa large scale au commercial farming, matumizi yake hayaepukiki. Huwezi kulima ekari kwa mfano 30 au 50 za mahindi au mpumga usitumie madawa ya magugu, mbolea nk
Majuu super markets kuna bidhaa products ambazo zimelimwa bila chemicals na bei yake ipo juu zaidi.
 
Kama dawa zipi ? Maana dawa zote zina class na zinatumika wapi hivyo ndo nachoelewa pia THPH ndo wanaruhusu hilo . Kuna dawa zipo kwenye matumizi ya makampuni tu uwezi zikuta maduka ya kawaida
Dawa ya graphosate inakaa mwaka mzima na ni kiboko ya magugu,Kwa crop rotation haifai
 
Hapo kwenye kununua, lazima ueleze aina ya mazao uliyolenga kwenda kupulizia.

Nyingi sasa hivi ni fake, ukipuliza zinababua tu haziui majani.

Ila ukipata og, ni nzuri sana.
Lt1 unapulizia eka1.

Katika upuliziaji inatakiwa timing ya umande na mvua, ni kwamba ukishapuliza haitakiwi kunyeshewa na mvua muda wa masaa6, pia pasiwe na umande mwingi unapunguza nguvu ya dawa.

Mi nishasahau kung'olea mpunga majani.

Zinasaidia sana kupunguza gharama kwa kweli.
MIMI SHAMBA LANGU NI LA MICHUNGWA KUNA NYASI NYINGI NNAWEZA KUTUMIA DAWA GANI YA KUKAUSHA HAYO MANYASI MAANA EKARI 6 KUZILIMIA HELA SINA KWA SASA
 
MIMI SHAMBA LANGU NI LA MICHUNGWA KUNA NYASI NYINGI NNAWEZA KUTUMIA DAWA GANI YA KUKAUSHA HAYO MANYASI MAANA EKARI 6 KUZILIMIA HELA SINA KWA SASA
'Dawa ya magugu isiyobagua'.
Zina majina mengi, lakini ukifika duka lolote la pembejeo ukitoa statment hiyo muuzaji atakuelewa bila shida.

Inategenea na mkoa, haizidi Tsh12,000@lt na maelekezo ya matumizi wameambatisha kwenye chupa.

Hivyo eka 6 zinahitajika lt6 kila eka1 huwa ni lt1 kuangamiza vioto.

Unatakiwa upige pasiwe na ukungu, umande wala mvua isinyeshe kwa muda wa masaa6 kulinda concentration ifanye kazi sawa sawa.

Wakati wa kupiga utaangalia hali ya anga, kama kuna dalili za mvua, sitisha zoezi.

Dumu la mgongoni ni muhimu kuwa nalo kwa kazi hiyo.
 
Ndio ,zinatumika sana kweymazao ya mda mrefu japo kama huna Mpango wa kuweka mazao mengine anytime soon wewe piga ni nzuri.

Kiambata ni graphosate.
Naijua ila glyphosate aikai mda huo wote ni miezi miwili mwisho dawa inayokaa sana ni lifenuron ambayo iko na athari zaidi kwenye hii industry ya kilimo niko mda mrefu , tembelea makampuni ya viuatilifu watakujulisha mfano hii glyphosate ya madukani aiwezi kukausha shamba la chai labda uweke mil 1000 kwenye lita 20 , mfano mwingine paraquat inatumika palizi hasa kwenye mashamba ya migomba, mahindi yaliyozidi magotini , kuna location mbeya sitapenda kupataja wakulima uitumia kukausha maharage hasa ya kipindi cha mvua too risk for consumer ili wayawahishe sokoni n.k
 
Hivi unajua matumizi ya herufi kubwa kenge wewe?
KUWA NA HESHIMA USIFIKIRI KILA UNAECHAT NAE HUMU UMRI WAKO MIMI NNA ANDIKA KWA MAANDISHI MAKUBWA SABABU YA UWEZO WANGU WA KUONA KWAHYO USIKURUPUKE KUTUKANA WATU NDIO MAANA JF WA ZAMANI WOTE HUMU WAMEBAKI WATAZAMAJI HAWAANZISHI MADA WALA KUCHANGIA MADA MAANA HUCHELEWI KUTUKANWA NA MTU UNAEWEZA KUMZAA.
 
BASI NISAMEHE MKUU WANGU
 
Back
Top Bottom