Mungu aliye mkamilifu, asiye fananishwa na kitu, Alfa na Omega; hapa anatamkwa namna hii?
Ama kuna namna ilimaanishwa na Mwandishi wa Wakorinto?
View attachment 2853435
Excel, hapa tatizo lipo katika udhaifu wa kutafsiri kwenda Kiswahili, na pia kuelewa maana ya andiko. Mungu hana upumbavu wala ujinga, na ni hatari sana kumfikiria Mungu katika muktadha huo kwa sababu unaweza ukafanya kufuru au dhambi isiyosameheka kwa sababu ya utakatifu wake.
Maneno yaha ya Paulo katika andiko hili katika lugha sanifu ya Kiswahili yanapaswa kusomeka hivi, "Kwa sababu kitu kipumbavu cha Mungu ni chenye hekima kuliko wanadamu, na kitu dhaifu cha Mungu ni chenye nguvu kuliko wanadamu."
Sasa nini maana ya andiko hili? Ni wazi Mungu aliumba vitu vyenye complexity tofauti tofauti, na kama ni katika suala la design, basi utasema kuna uumbaji wa Mungu ni wa design iliyotumia akili ya juu sana. Kwa mfano, fikiria alivyoumba ubongo wa mwanadamu, ambao ni wa kipekee kuliko compyuta zenye nguvu sana. Lakini pia fikiria kiumbe rahisi sana alichoumba Mungu, kama earthworm. Katika macho ya kibinadamu, unaweza kuona kiumbe kama earthworm ni cha kipumbavu, au mwingine akaona Mungu kuumba vitu kama nzi halikuwa jambo la hekima.
Lakini sasa, ndio Paulo anawakumbusha watu, kwamba katika mtazamo wa kibinadamu, kile tunachoona kuwa cha " kipumbavu au kitu dhaifu" ni chenye hekima kuliko hao wanadamu ambao mara nyingine wanakosa kabisa hekima ya kuwa wameumbwa na Mungu. Hebu mlinganishe mtu anaemnajisi mtoto wa miaka mitatu, je, katika uumbaji wa Mungu, si utaona nzi ni kiumbe wa maana kuliko mtu kama huyo?
Na unaweza kuona kama kiumbe kama mbu anaeeneza malaria, ni namna ya udhaifu katika uumbaji wa Mungu, au kwa mfano funza (maggots) ambao utaona ni disgusting. Waliumbwa kwa sababu nzuri tu zinazomfaa binadamu, hawakufanywa wawepo ili kueneza magonjwa au kufanya uharibifu, kama vile tu simba hakuumbwa ili awinde wanyama na kuwala. Haya ni matokeo ya uasi wa shetani ibilisi. Kwa hiyo andiko hilo lipo katika context hiyo. Hivyo hata katika hali hizi, usiviangalie vitu katika context ya kuona ni kitu cha kipumbavu au udhaifu cha Mungu.
Lakini pia kuna suala ambalo linahusu amri za Mungu, ambazo wewe unawza kuona ni za kijinga au ni udhaifu kuzifuata. Akishasema usifanye hivi, hata kama unaona ni udhaifu, ni ujinga, watu hawatakuelewa, ujue kwamba yeye kama Mungu anaona mbali sana kuliko wewe kama mwanadamu. Fuata. Usichukue position ya kutaka kumshauri Mungu, au kuona kama alikosea, au hakufikiria mbali alipotoa agizo fulani. Kuna mtu anaona ni udhaifu kuomba msamaha pale ambapo unajua hujafanya kosa, lakini Mungu anasema wewe fanya hivyo hata kama unajua sio kosa lako, ili ulete amani na mtu mliekorofishana.
Vitu kama hivi muwe mnawatafuta mashahidi wa Yehova wawafafanulie. Nimejifunza mengi sana toka kwao, pamoja na hili. Huu sio ujuzi wangu, bali ni ufafanuzi wao.