Watu kama wewe ndio mnanifanya niachane na ku-post vitu JF. Najiona kama napoteza muda kujibizana na watu ambao hawajui vitu, na hawajui kwamba hawajui, halafu wanajifanya wanajua. Na badala ya kujibu hoja ili kuendeleza mazungumzo, wanakuja na kashfa. Ni dalili za matataizo ya afya ya akili.
Hata hivyo, kwa mfano, umewahi kujiuliza kwa nini mwanadamu ana apendix katika tumbo? Ni kwa sababu hata mwanadamu hakuumbwa ale nyama. Suala la kula nyama likikuja baadae sana, baada ya Gharika ya Nuhu. Ni akili kufikiri hapo ndipo wanyama nao walianza kula nyama, maana la sivyo ndani ya Gharika ingekuwa ni vurugu tupu.
Lakini sasa, ona kwamba kwa kuwa suala la ulaji nyama halikuwa katika mpango wa Mungu, Mungu anaporejesha hali ya amani, zile hali zilizokuwapo katika Eden zinarejeshwa tena. Angalia andiko la Isaya 65:25; "Mbwa mwitu na mwanakondoo watalisha pamoja, Simba atakula majani kama ng’ombe dume, na chakula cha nyoka kitakuwa mavumbi. Hawatadhuru wala kusababisha uharibifu wowote katika mlima wangu wote mtakatifu,” asema BWANA.
Sasa japo Biblia inasema Mungu aliumba wanyama wa porini na kufugwa, hakuna mahali inasema simba na fisi nk walikula nyama. Na japo Biblia haisemi wazi kwamba simba hakula nyama, inference za mwanadamu kuruhusiwa kula nyama baada ya Gharika, na Mungu kuongelea simba kula majani, ni wazi amani katika bustani ya Eden ilikuwapo pia kati ya wanyama kwa wanyama, na wanadamu kwa wanyama. Hawakuuana kwa ajili ya chakula.
Na suala la kusema wadudu kuleta magonjwa, Mungu aliwaumba wa nini? Swali nzuri, lakini Mungu hakuwaumba ili walete magonjwa. Usisahau wadudu kama nzi na funza (maggots) wana sehemu yao. Na sikatai kabisa kwamba simba walikula nyama katika bustani ya Eden, labda walikula mizogo bila ya kuwaua wanyama, kwa sababu katika bustani ya Eden wanyama walikuwa wakifa, na hatutarajii kwamba Adamu alifanya kazi ya kumzika kila mnyama aliekufa.