Wataalamu wa lugha ya Kiswahili naomba mnisaidie katika hili 👇.

Wataalamu wa lugha ya Kiswahili naomba mnisaidie katika hili 👇.

Hata mimi ninawaza hivyo hivyo. Huenda wanasema "namba ya...", Kwa kuzichukilia zile tarakimu 10 kama kitu kimoja.
Ndivyo ilivyo, hizo tarakimu 10 za namba ya simu n moja hvy n namba ya simu na sio namba za simu.

Hata nida tunasema namba ya nida na sio namba za nida.
 
Namba ya simu ni mkusanyiko wa namba/tarakimu kadhaa zinazompa mtumiaji uwezekano wa kuwasiliana kutumia kifaa simu. Kwa hivyo mkusanyiko huo kama ulivyo ni "namba" moja. Mfano pia unaweza kuwa kwenye namba ya usajili ya gari na mambo mengine kadhaa.
 
namba ya simu (maana ni namba moja )
namba za simu (maana yake mpe zote za mitandao yote uliyo nayo)

zote zi sahihi kulingana na unataka namba 1 (ya) ama mitandao yote/nyingi/tofauti (za)
Lakini laini moja ya simu inatarakimu (namba) zaidi ya Moja mkuu.
 
Namba ya simu ni mkusanyiko wa namba/tarakimu kadhaa zinazompa mtumiaji uwezekano wa kuwasiliana kutumia kifaa simu. Kwa hivyo mkusanyiko huo kama ulivyo ni "namba" moja. Mfano pia unaweza kuwa kwenye namba ya usajili ya gari na mambo mengine kadhaa.
Ufafanuzi murua huu.
 
Back
Top Bottom