Wataalamu wa lugha ya Kiswahili naomba mnisaidie katika hili 👇.

Wataalamu wa lugha ya Kiswahili naomba mnisaidie katika hili 👇.

Ni sawa na wale huwa wanasema taja majina yako as if majina ya wazazi yote ni ya kwako.
 
Namba ya simu kwa sababu simu ni moja na namba yake inaweza kuwa na dijiti kadhaa...." Namba ya simu ni sawa zaidi, hata tukichukulia simu kama laini bado namba itakayotajwa bila kujali dijiti zake ni namba ya laini ileile moja labda ziwe laini au simu mbili ndipo tunaweza kusema namba za simu au laini.
 
Tarakimu/digits ni tofauti na namba/number. 1,000,000 hii namba moja inayoitwa milioni yenye tarakimu saba. Kinachounda namba ni tarakimu.
Nimeelawa na Uzi unapaswa kufungwa.
 
''Hebu'' naomba namba zako za simu,

Hapa neno hebu halikukaa kiungwana,ilitakiwa iwe unaweza kunipatia namba yako ya simu kama hutojali?

''Nipe namba yako ya simu''
Kauli hii sio ombi bali ni amri,haikukaa kiungwana,


Nikirudi kwenye mada,

Namba za simu maana yake ni namba zaidi ya moja,
Namba ya simu,maana yake ni contact yako moja,

Mfano mtu hawezi kukwambia ''Nipe namba zako za size ya viatu'' kisa size yako ni 42,haiwezi kuitwa namba za viatu kisa kuna tarakimu za namba mbili,yani namba 4 na 2 hiyo ni size moja,

So,kwa contact moja itaitwa namba ya simu.
 
Back
Top Bottom