Wataalamu wa Sheria mje hapa, mueleze hii kesi atashinda nani

Wataalamu wa Sheria mje hapa, mueleze hii kesi atashinda nani

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,387
Reaction score
44,030
Kuna kijana mpigapicha nchi jirani kaipeleka mahakamani kampuni kubwa ya kuuza maji kwa kutumia picha aliyoipiga bila ridhaa yake.

Picha yenyewe ni ya mtu anakunywa maji yanayotengenezwa na hiyo kampuni. Kuna watu wanasema kampuni haina kesi kwa sababu mpigapicha alipiga kinywaji chao bila ridhaa ya kampuni.

Chanzo cha yote ni baada ya picha kwenda viral. Ilitapakaa sana mtandaoni. Kijana kaona kuna haki zake pale. Je, kijana atashinda au kampuni itashinda?
 
Kampuni itashinda mana kuna brand yao iliyosajiliwa kwenye hiyo picha hvy itaonekana wao ndo wamiliki Sahihi wa hiyo picha.

Jamaa atashindwa mana hakuna chcht cha kuthibitisha hiyo picha n mali yake na hata hvy itaonekana ametumia brand ya kampuni kinyume na utaratibu wa kampuni.

Tena hy kampuni wakikaza, jamaa ndo anatakiwa kuwalipa hiyo kampuni.

Anyway, tungeona picha na sisi
 
Kuna kijana mpigapicha nchi jirani kaipeleka mahakamani kampuni kubwa ya kuuza maji kwa kutumia picha aliyoipiga bila ridhaa yake.

Picha yenyewe ni ya mtu anakunywa maji yanayotengenezwa na hiyo kampuni. Kuna watu wanasema kampuni haina kesi kwa sababu mpigapicha alipiga kinywaji chao bila ridhaa ya kampuni.

Chanzo cha yote ni baada ya picha kwenda viral. Ilitapakaa sana mtandaoni. Kijana kaona kuna haki zake pale. Je, kijana atashinda au kampuni itashinda?
Hiyo picha ni image ya huyo mpigapicha au ya mtu mwingine (mteja wake)?
 

View: https://m.youtube.com/watch?v=fXQZj2sS340&pp=0gcJCcQBo7VqN5tD

Led to👇


View: https://m.youtube.com/watch?v=0KbiBl0r4Q4

Led to 👇
IMG_8201.jpeg


Picha ni intellectual property ya mpigaji uwezi kuitumia bila ya ridhaa yake, na hata huyo aliyepo kwenye picha nae inabidi alipwe.
 
Back
Top Bottom