Binti wa zamani
Platinum Member
- Nov 19, 2011
- 15,052
- 36,866
Mara nyingi usiku nikilala huwa sipati kabisa ndoto au nikiota asubuhi nakua nimesahau nilichoota.
Ila jana usiku nimeota ndoto ambayo imenitisha na naikumbuka kwa sehemu kubwa, siku nzima nimejaribu kuwa bize ili kuisahau ila imegoma kabisa kutoka kichwani na kuna kitu kinanisukuma niisimulie.
******💭🛌
Nimeota ni binti mdogo miaka kama 13 -15 hivi niko na wazazi tunatembea, mara tukaanza kusikia sauti ambazo hazieleweki kama watu wanapiga mayowe, wengine wanalia, tukasimama. Ghalfla tunaona watu hawaonekani sura wanatujia huku wanakimbia na sisi tukaanza kukimbia tukielekea uelekeo mwingine. Baada ya umbali kidogo mimi nikadondoka na wale watu wakanikamata.
Nikapelekwa mahali sipajui, nikakaa huko muda mrefu (miaka kadhaa) na wakaletwa watoto wengine ambao sikua nawafahamu.
Siku moja nikajaribu kutoroka, nikatoka kwenye chumba cha kulala, nikaanza kukimbia sijui naenda wapi, nakumbuka kuna wakati nilikimbia sehemu yenye mteremko mrefu na baada ya kukimbia sana nikakuta kibanda, nikajificha hapo. Kulipokucha nikajikuta bado niko msituni ila mbele yangu nikaona kuna geti kubwa na kama nasikia sauti za watu na pikipiki na magari.
Nikaendelea kukaa pale nilipojiificha huku nimejawa woga, baada ya muda akapita mmoja kati ya wasichana ambao tulikua tumefungiwa nao kule msituni, akafungua lile geti na funguo halafu akatoka nje, nikasubiria kuona kama atarudi, baada ya muda mchache akarudi, basi nikapiga kelele “naomba na mimi unifungulie” akaniangalia usoni, akatabasamu, akafungua na kuacha geti wazi, akaondoka. Nikasimama na kutoka pale nilipojificha huku nakimbia, nikafanikiwa kutoka nje ya lile geti.
Cha kushangaza nilivyotoka tu ndani ya lile geti, hakukua tena na misitu wala mashamba, bali makazi ya kawaida ya watu, yani mtaani pa kawaida, mazingira ya mjini, nilivyoangalia tena pale nilipotokea naona kuna duka, na hakuna geti.
Sikumbuki tena sehemu nyingine ya ndoto ila nakumbuka imeendelea nimekua mtu mzima sana, nikarudi lile eneo na ghafla wakati natembea mtu akanishika mkono, akasema yule mzee wa misituni anasema urudi umeacha mtoto wako huko. Yule mtu aliyenishika mkono naye alikua hana sura haionekani.
Nikaamka moyo unadunda, nikasali!
Je, kuna mtu ameshawahi kupata ndoto kama hiyo ambayo inagoma kutoka kichwani na ni ya kuogopesha?