Usiumie Sana akili sababu haya mambo ukiyapotezea yanakimbia mana yanaona hayapo sehemu sahihi lakini lazima utagombana Na ndugu Kwa maana utakuwa umeukana ukoo kimtindo.Asante kwa mwangaza, nimerudia kusoma mara kadhaa na nitaendelea kutafakari.
Ushauri nimeuchukua, shukrani sana!
Nafsi yako imetekwa kuzimumisituni anasema urudi umeacha mtoto wako huko. Yule mtu aliyenishika mkono naye alikua hana sura haionekani.
HatariHamna mtaalamu!
I wish hata ingekua ni ndoto ya kuliwa 🍑, hapo ningeelewa ni upwiru tu unanisumbua 😅
Nina moyo wa shukrani kwa ajili ya huyo ndugu.Ulikuwa unakufa lakini kuna mtu katika ndugu zenu kakukuokoa na hiyo mauti.
Sawa, hatutawadharau 🫠Msidharau walokole siku nyingine
Nimejihami tu, maana hawashindwi kuja kusema nilikua nimelewa 😅Kuhusisha Gambe kwenye mambo yasiyo ya lazima
Kunakera zaidi ya jambo lenyewe
Kutumikia kifungo nikiwa mtoto?Kwa kifupi umetumikia kifungo usichokijua hadi kimeisha... Bahati mbaya ulizalishwa ujinini ndio maana ulifuatwa uraiani ukaambiwa ufuate mtoto wako 🤣🤣... Sauti ya mshana
Wewe, nitakutupia kwenye ignore list ushangae 🤣🤣🤣Sijasoma mada ila nimesikitika sana hasa hapo uliposema walikuua 😭
Huwezi, Mm ndo utamu wako 😋Wewe, nitakutupia kwenye ignore list ushangae 🤣🤣🤣
Ukiota unafanya mapenzi ndotoni🤣🤣🤣 haya nikiota nakojoznitakushirikisha mtaalamu 😅
Nayapotezea tu, maana hata sijui cha kuhangaika nacho hapo ni nini!Usiumie Sana akili sababu haya mambo ukiyapotezea yanakimbia mana yanaona hayapo sehemu sahihi lakini lazima utagombana Na ndugu Kwa maana utakuwa umeukana ukoo kimtindo.
Nitajaribu kukumbuka kama kuna ahadi nilitoa ambayo sijaitimiza.Ila ikumbuke ahadi hiyo ndio ambayo itakusumbua itekeleze ili ufanye mambo mengine Kwa Amani.
I hope mtoto unamaanisha hiyo ahadi na si mtoto kweli!Si unajua mtoto ukimtelekeza lazima atakusumbua Kwa simanzi Yake 😂😂😂 Rudi umfate mtoto wako
Kifungo cha huko unaweza kufungwa hata ukiwa kwenye pumbu za mzazi 😁😁... Mtoto wa ujinini ana damu yako hivyo wakihitaji kukusumbua watakatumaKutumikia kifungo nikiwa mtoto?
Na kama nilizalishwa, mtoto wa ujinini si anabakia huko huko au?
AmenBinadamu ana vitu vitatu vinavyomkamilisha yupo mara tatu yaani katika segemu kuu tatu ambazo zote kwapamoja zinamkamilisha.
Sehemu ya kwanza ni MWILI huu wa damu na nyama,ambao utakufa na kuharibika ,
Sehemu ya pili ni Nafsi(ufahamu utashi) ambao kumbukumbu akili udahamu conscious,subconscious ..hii hudumu milele haifutiki.
Sehemu ya tatu ni ROHO ambayo ni pumzi ya uhai haifi.
Mwili ambao asili yake ni uharibifu na MAUTI hufa..huwa unazeeka,kuugua,kuchoka n.k.
ROHO always ni kijana au mtoto kama teenage ROHO HAIZEEEKI iko vile vile ,sio mrefu sio mfupi,ni kijana..kama ulivyo ota uko teenage..ndio binadamu wote ni vijana katika ulimwengu wa Roho ,haizeeki ,haifi.
MWILI+NAFSI+ROHO=MWANADAMU
SO HAYO ULIYO OTA na ulivyojiona ndio wewe ulivyobkatika ulimwengu wa ROHO.
NDOTO ZOTE ZINA MAANA ,PIA NDOTO ZOTE NI HALI HALISI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.
Hasa ndoto unayoiota ukakosa amani,ina maana unatakiwa uchukue hatua ya haraka ,mana Yanayodhihirika kutokea katika ulimwengu wa MWILI huanza kwanza kutokea katika ulimwengu wa Roho.
Kabla kitu hakijatokea machoni huanza kwanza kufanyika katika ulimwengu wa ndoto halafu kinakuja kutokea LIVE baade au unakuta ndio hali halisi unayoipitia kiroho kwa wakati huo.
2.KUOTA UNAKIMBIZWA Mana yake kuna Roho za giza zinazokufuatilia maisha yako..au nguvu za giza kama wachawi,mizimu ya ukoo,mapepo,n.k
3.KUona watu miguu lakini sura hiwaoni...HIYO ni kawaida ya watu wabaya au roho za giza ambazo ni adui hutumia njia ya kujifunika sura/kujificha utambulisho wao wasionekane..WACHAWI huwa wanajificha SURA wasitambulike,LAH wasipojificha sura usiwatambue basi watavaa SURA ya mtu wa wa karibu yako unayfahamu kama ndugu yako, kaka,dada,wazazi wako ili kukufarakanisha ja jamaa zako(MCHAWI HATAKIWI KUTAMBULIKA)..na endapo ukamuona sura kwenye ndoto na ukamtambua hata yeye atajua umemtambua hata kesho ukimsalimia hataitika mana atajua ulimuona kwenye ndoto na ukamtambua,Usipomuona sura na kumtambua kama hivyo ,hivyo ndivyo wanavyopenda.
KUOTA UPO KIFUNGONI/UMEFUNGIWA KWENYE CHUMBA..Mana yake umefungwa katika ufahamu mana upo mjini lakini wewe ukiwa ndani ya kifungo hata mji hu uoni ila unaona upo poroni au kwenye kijumba.
UKIWA KIFUNGONI mana yake MAMBO YAKO MENGI YAMEFUNGWA..hata vision yako,na mambo yako kadhaa maeneo fulani yatakua yamefungwa ..
KITOKEWA TENA na mtu mbaya aliyenificha sura na kukutaka URUDI PORINI kwa vile kule una mtoto wako..
Maana yake bado kuna ROHO ZA ADUI nguvu za giza zinakufuatilia na una maagano nazo,pengine uliingizwa kwwnye maagano bila kujua labda na MIZIMUYA UKOO,ama na wachawi kupitia vitu mbalimbali au hata ndotoni au mapepo ndotoni na yanasema una mtoto kule porini,huenda una mtoto wa kiroho na hayo maroho ya giza,.MIKATABA mikataba mingine ni ya damu ya ukoo toka enzi za mababu na mabibi.hata kabla hujazaliwa.
NINI CHA KUFANYA SULUHISHO.
YESU PEKEE ndiye anayeweza kumuokoa mwanadamu kutoka katika nguvu za giza akamuhamisha na kumuongiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake..
VUNJA ROHO ZA MAAGANO na kataa roho zinazokufuatilia zikemee kwa jina la Yesu,
OMBA SALI,
FUNGA maombi ya kufunga na kuomba yana manibu ya haraka na yana nguvu kubwa.
Lakini umeridhika na tafsiri yangu?Nina moyo wa shukrani kwa ajili ya huyo ndugu.
Sawa, hatutawadharau 🫠
Ndoto yako ni njema. Ni muongozo unaotakiwa kuufuata. Ndoto imekukumbusha maisha yako ya nyuma na namna ulivyokwepa viunzi kadhaa katika maisha yako kwa msaada usioutarajia. Mwisho ndoto inakukumbusha ni wakati sahihi kukumbuka malengo yako uliyowahi kuyafikiria na kwa wakati huu unaweza kuyatimiza kwa kuwa tiyari unafahamu kuna nguvu inayokuongoza na kukulinda.Mara nyingi usiku nikilala huwa sipati kabisa ndoto au nikiota asubuhi nakua nimesahau nilichoota.
Ila jana usiku nimeota ndoto ambayo imenitisha na naikumbuka kwa sehemu kubwa, siku nzima nimejaribu kuwa bize ili kuisahau ila imegoma kabisa kutoka kichwani na kuna kitu kinanisukuma niisimulie.
******💭🛌
Nimeota ni binti mdogo miaka kama 13 -15 hivi niko na wazazi tunatembea, mara tukaanza kusikia sauti ambazo hazieleweki kama watu wanapiga mayowe, wengine wanalia, tukasimama. Ghalfla tunaona watu hawaonekani sura wanatujia huku wanakimbia na sisi tukaanza kukimbia tukielekea uelekeo mwingine. Baada ya umbali kidogo mimi nikadondoka na wale watu wakanikamata.
Nikapelekwa mahali sipajui, nikakaa huko muda mrefu (miaka kadhaa) na wakaletwa watoto wengine ambao sikua nawafahamu.
Siku moja nikajaribu kutoroka, nikatoka kwenye chumba cha kulala, nikaanza kukimbia sijui naenda wapi, nakumbuka kuna wakati nilikimbia sehemu yenye mteremko mrefu na baada ya kukimbia sana nikakuta kibanda, nikajificha hapo. Kulipokucha nikajikuta bado niko msituni ila mbele yangu nikaona kuna geti kubwa na kama nasikia sauti za watu na pikipiki na magari.
Nikaendelea kukaa pale nilipojiificha huku nimejawa woga, baada ya muda akapita mmoja kati ya wasichana ambao tulikua tumefungiwa nao kule msituni, akafungua lile geti na funguo halafu akatoka nje, nikasubiria kuona kama atarudi, baada ya muda mchache akarudi, basi nikapiga kelele “naomba na mimi unifungulie” akaniangalia usoni, akatabasamu, akafungua na kuacha geti wazi, akaondoka. Nikasimama na kutoka pale nilipojificha huku nakimbia, nikafanikiwa kutoka nje ya lile geti.
Cha kushangaza nilivyotoka tu ndani ya lile geti, hakukua tena na misitu wala mashamba, bali makazi ya kawaida ya watu, yani mtaani pa kawaida, mazingira ya mjini, nilivyoangalia tena pale nilipotokea naona kuna duka, na hakuna geti.
Sikumbuki tena sehemu nyingine ya ndoto ila nakumbuka imeendelea nimekua mtu mzima sana, nikarudi lile eneo na ghafla wakati natembea mtu akanishika mkono, akasema yule mzee wa misituni anasema urudi umeacha mtoto wako huko. Yule mtu aliyenishika mkono naye alikua hana sura haionekani.
Nikaamka moyo unadunda, nikasali!
Je, kuna mtu ameshawahi kupata ndoto kama hiyo ambayo inagoma kutoka kichwani na ni ya kuogopesha?
Sawa, nitafikiria hili swala la kuokoka.Shida kuokoka hamtaki.. ndoto ya namna hii ni ngumu sana kuishughulikia kikamilifu kama hujaokoka kwa sababu kuna vitu utashindwa kuvielewa, yani kuna namna ukielezewa hapa itakuwa ni ngumu sana ww kuelewa sababu unakuwa huna uelewa wa kiMungu.
Mpe Yesu kwanza maisha yako ili akusaidie kwenye matatizo kama haya