Watafsiri na wabobezi wa ndoto naomba mniambie hii inamaanisha nini?

Watafsiri na wabobezi wa ndoto naomba mniambie hii inamaanisha nini?

Wenzio tunaota tuko maabara tuna design engines za kutufikisha sayari ya Mars.wewe mwenzetu unaota ujinga?
Pathetic
 
Mara nyingi usiku nikilala huwa sipati kabisa ndoto au nikiota asubuhi nakua nimesahau nilichoota.

Ila jana usiku nimeota ndoto ambayo imenitisha na naikumbuka kwa sehemu kubwa, siku nzima nimejaribu kuwa bize ili kuisahau ila imegoma kabisa kutoka kichwani na kuna kitu kinanisukuma niisimulie.

******💭🛌
Nimeota ni binti mdogo miaka kama 13 -15 hivi niko na wazazi tunatembea, mara tukaanza kusikia sauti ambazo hazieleweki kama watu wanapiga mayowe, wengine wanalia, tukasimama. Ghalfla tunaona watu hawaonekani sura wanatujia huku wanakimbia na sisi tukaanza kukimbia tukielekea uelekeo mwingine. Baada ya umbali kidogo mimi nikadondoka na wale watu wakanikamata.

Nikapelekwa mahali sipajui, nikakaa huko muda mrefu (miaka kadhaa) na wakaletwa watoto wengine ambao sikua nawafahamu.

Siku moja nikajaribu kutoroka, nikatoka kwenye chumba cha kulala, nikaanza kukimbia sijui naenda wapi, nakumbuka kuna wakati nilikimbia sehemu yenye mteremko mrefu na baada ya kukimbia sana nikakuta kibanda, nikajificha hapo. Kulipokucha nikajikuta bado niko msituni ila mbele yangu nikaona kuna geti kubwa na kama nasikia sauti za watu na pikipiki na magari.

Nikaendelea kukaa pale nilipojiificha huku nimejawa woga, baada ya muda akapita mmoja kati ya wasichana ambao tulikua tumefungiwa nao kule msituni, akafungua lile geti na funguo halafu akatoka nje, nikasubiria kuona kama atarudi, baada ya muda mchache akarudi, basi nikapiga kelele “naomba na mimi unifungulie” akaniangalia usoni, akatabasamu, akafungua na kuacha geti wazi, akaondoka. Nikasimama na kutoka pale nilipojificha huku nakimbia, nikafanikiwa kutoka nje ya lile geti.

Cha kushangaza nilivyotoka tu ndani ya lile geti, hakukua tena na misitu wala mashamba, bali makazi ya kawaida ya watu, yani mtaani pa kawaida, mazingira ya mjini, nilivyoangalia tena pale nilipotokea naona kuna duka, na hakuna geti.

Sikumbuki tena sehemu nyingine ya ndoto ila nakumbuka imeendelea nimekua mtu mzima sana, nikarudi lile eneo na ghafla wakati natembea mtu akanishika mkono, akasema yule mzee wa misituni anasema urudi umeacha mtoto wako huko. Yule mtu aliyenishika mkono naye alikua hana sura haionekani.

Nikaamka moyo unadunda, nikasali!

Je, kuna mtu ameshawahi kupata ndoto kama hiyo ambayo inagoma kutoka kichwani na ni ya kuogopesha?
Epuka kushiba sana usiku
 
Ok.Rudi kwenye ule uzi wa kutafuta rafiki wa hivi majuzi(Nadhani nilicomment) nenda delete then ghairi ule mpango wa kutafuta Rafiki wa kiume wa kusafiri nae na mambo kama hayo utakuja Nashukuru.Ila kwakuwa wanadamu tumeumbiwa try and error jaribu pia utanikumbuka.📌
 
Ndoto ni maono ambayo unaonyeshwa mambo ambayo yanatokea au yatakuja kukutokea baadae.

Unapoota ndoto kwnz unapaswa ujuwe muda na saa ya ndoto yenyewe.
Ukiota ndoto kuanzia saa Saba usiku hadi saa Tisa na nusu ,
Hyo ndoto 99% ni kweli jambo hilo linafanyika au litafanyika.

Ukiota ndoto unafukuzwa na watu au mnyama na ukakamatwa au ukang'atwa na mnyama ,,
maana yake upo kwenye shida kubwa na wameshakuroga tayari.

Kitendo cha kuota umetoroka na kukimbia maana yake ni kwamba umefanikiwa kukimbia ubaya .

Na kitendo cha kukamatwa mkono tena maana yake ni kwamba bado wabaya wanakuwinda ingawa ulifanikiwa kutoroka huko msituni.

Fanya sana maombi mkuu,ipo vita ya kichawi mbele yako..
 
Wazazi = Ulinzi
Watu wasio onekana = stress, msongo, vikwazo
Kufungwa miaka = usimbe, joblessness
Watoto mateka = friends cycle ambao mnashea mitizamo
Kutoroka/kukimbia = self development, self love, kujikwamua
Kutoka nnje = mwisho mzuri
Kuacha mtoto = kuto kamilisha malengo, talent,
Kurudi = second chance to get your shit together
Kushikwa mkono = wasiwasi, kutokujiamini
Conclusion : baada ya kutoka kwa wazazi na kwenda kuishi kivyako mambo mengi yametokea, so life journey ina mengi, Ila grab it by the horns and ride it. Keep dreaming.
Asante kwa kuchukua muda wako na kushare tafsiri, nimeipokea.
Hii conclusion yako itaishi na mimi, shukrani!
 
Pole sana mamy.
Asante sana mamie 💕
Uko kwenye vita Kali iliyotoka kizazi kimoja kwenda kingine,,, mizimu ya mama yako iko na wewe na inapambana

1. Unaweza kusali kwa Imani yako kwa dhamira na Imani kuu kuombea hiyo vita

2. Ukiweza katembelee makaburi ya kwenu safisha na uombe kwa Imani yako

3. Unaweza kutumia mafuta ya mzeituni kupaka kwani hufukuza vitu vibaya vya kila aina.
Nitayafanya haya yote, shukrani sana!
 
Most likely nyumba ina wachawi au walikuja wachawi...
Hebu nenda hotel nzuri hivi kama Una hela kidogo ...lala hapo uone utaota ndogo gani
Mbona nalala kila siku hapa nyumbani na sijawahi kuota ndoto kama hizi?
Na hata jana na leo sijaota tena, sidhani kama itakua ni wachawi.
 
Back
Top Bottom