Watafsiri na wabobezi wa ndoto naomba mniambie hii inamaanisha nini?

Sikua nimerealize hilo.
We unafikiri ni mambo gani?
Ndoto inawahusu zaidi wazazi wako kuliko wewe so kama wapo nenda ukaongee nao, wakupe historia mbili tatu za wewe hadi 13 yrs...

Ndoto imekaa zaidi kimakubaliano baina ya watu wawili ila hayakutekelezwa (agano) na inaonekana bado lipo so unakumbushwa na yule Babu wa msituni kwamba kuna mtoto wako umemuacha kule😂😂😂 (code).
 
Ndoto inawahusu zaidi wazazi wako kuliko wewe so kama wapo nenda ukaongee nao, wakupe historia mbili tatu za wewe hadi 13 yrs...
Wapo, sasa nikaongee nao nini? niwasimulie ndoto au nifanye nini. Asubuhi tayari nilimsimulia mama akasema tuombe tu!
Ndoto imekaa zaidi kimakubaliano baina ya watu wawili ila hayakutekelezwa (agano) na inaonekana bado lipo so unakumbushwa na yule Babu wa msituni kwamba kuna mtoto wako umemuacha kule😂😂😂 (code).
So inamaanisha huyo mtoto ndiyo hilo agano, au?
 
Wapo, sasa nikaongee nao nini? niwasimulie ndoto au nifanye nini. Asubuhi tayari nilimsimulia mama akasema tuombe tu!

So inamaanisha huyo mtoto ndiyo hilo agano, au?
Tuombe tu! It seems kuna kitu anakijua😅😅😅, waulize tu kama kuna agano lolote waliwahi kuingia wakati unazaliwa or before haujazaliwa...

Anyways, achana na hiyo ndoto, ipotezee kwasababu kwanza sio mbaya, so usichukulie serious haya maneno yangu mkuu (tuendelee kuzogoa, au hii sio mada ya kuzogoa kwa voice yako mwenyewe😂)
 
Kama ni kweli ina maana hiyo ndoto sio ya kawaida hata kidogo.

Possibly kuna jambo lilikutokea kipindi unavunja ungo, ikiwemo kuanza kwa tabia mpya kabisa ambayo pengine hukuwa nayo. Pengine ume stack kwenye jambo fulani kwa muda mrefu na hujaweza ku move on.
Lakin pia kuna uwezekano fate yako ipo controlled na spirits zenye uhalali kabisa na maisha yako.
Either kwa wazazi wako au wewe kufanya maagano kwa kujua ama bila kujua.

Kama unamuamini Mungu, jitahidi umuombe akusaidie uvuke. Ila ukitaka kulala kwa amani kabisa ikiwa una wasiwasi play gospel music uache zikiimba wakati umelala, hasa zile za kusifu na kuabudu
 
Hii ndoto Ina laana ndani Yake.

Sauti zisizoelewaka maana Yake ni malumbando katika ukoo wenu.

Msituni ni kifungo cha laana

Binti aliyekuja kukusaidia ni roho ya Nguvu yaani unalindwa na kuna mara unatenda wema bila kutarajia utalipwa Sasa huyo binti ndio malipo

Geti ni vizuizi vya kimaisha lakini ukatoka.

Babu anakwambia umeacha mtoto.
Kuna ahadi uliyosemaga utaifanya na bado hujaifanya kwahiyo tekeleza ahadi hiyo mambo haya kauondoke.
Hii ipo Kwa upande wa baba yako maana ndio ukoo wako.

Ushauri zidisha Sala Na maombi maana hii vita pia haupo peke yako Hao Wadada mliofungwa pamoja nao wanapitia Msoto kama wako lakini vipindi tofauti.

Zidisha kutoa Sadaka Kwa nahitaji.

Msitu kwenye ndoto humaanisha vikwazo katika Maisha.

Bila Shaka utakuwa umepata mwangaza kidogo WA ndoto yako
 
Tuombe tu! It seems kuna kitu anakijua😅😅😅, waulize tu kama kuna agano lolote waliwahi kuingia wakati unazaliwa or before haujazaliwa...
Sawa nitawauliza.
Anyways, achana na hiyo ndoto, ipotezee kwasababu kwanza sio mbaya, so usichukulie serious haya maneno yangu mkuu (tuendelee kuzogoa, au hii sio mada ya kuzogoa kwa voice yako mwenyewe😂)
Haya tuzogoe, lete sasa mada ya zogo 😂
 
Sawa nimechukua ushauri, asante sana 🙏🏽
 
Asante kwa mwangaza, nimerudia kusoma mara kadhaa na nitaendelea kutafakari.

Ushauri nimeuchukua, shukrani sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…