Watafsiri na wabobezi wa ndoto naomba mniambie hii inamaanisha nini?

Kwa kifupi umetumikia kifungo usichokijua hadi kimeisha... Bahati mbaya ulizalishwa ujinini ndio maana ulifuatwa uraiani ukaambiwa ufuate mtoto wako 🤣🤣... Sauti ya mshana
 
Asante kwa mwangaza, nimerudia kusoma mara kadhaa na nitaendelea kutafakari.

Ushauri nimeuchukua, shukrani sana!
Usiumie Sana akili sababu haya mambo ukiyapotezea yanakimbia mana yanaona hayapo sehemu sahihi lakini lazima utagombana Na ndugu Kwa maana utakuwa umeukana ukoo kimtindo.

Ila ikumbuke ahadi hiyo ndio ambayo itakusumbua itekeleze ili ufanye mambo mengine Kwa Amani.

Siunajua mtoto ukimtelekeza lazima atakusumbua Kwa simanzi Yake 😂😂😂 Rudi umfate mtoto wako
 
misituni anasema urudi umeacha mtoto wako huko. Yule mtu aliyenishika mkono naye alikua hana sura haionekani.
Nafsi yako imetekwa kuzimu
Huyo mtoto uliyenaye ni wa huko kuzimu
Na mchakato wa kujaribu kutoka nje ya geti ni inaonyesha nafsi yako ikihangaika kutafuta uhuru

Cha kufanya
Ombea Nafsi yako ikombolewa
Jitoe kwenye vifungo vya nafsi
 
Shida kuokoka hamtaki.. ndoto ya namna hii ni ngumu sana kuishughulikia kikamilifu kama hujaokoka kwa sababu kuna vitu utashindwa kuvielewa, yani kuna namna ukielezewa hapa itakuwa ni ngumu sana ww kuelewa sababu unakuwa huna uelewa wa kiMungu.
Mpe Yesu kwanza maisha yako ili akusaidie kwenye matatizo kama haya
 
Kwa kifupi umetumikia kifungo usichokijua hadi kimeisha... Bahati mbaya ulizalishwa ujinini ndio maana ulifuatwa uraiani ukaambiwa ufuate mtoto wako 🤣🤣... Sauti ya mshana
Kutumikia kifungo nikiwa mtoto?

Na kama nilizalishwa, mtoto wa ujinini si anabakia huko huko au?
 
Binadamu ana vitu vitatu vinavyomkamilisha yupo mara tatu yaani katika sehemu kuu tatu ambazo zote kwapamoja zinamkamilisha.
Sehemu ya kwanza ni MWILI huu wa damu na nyama,ambao utakufa na kuharibika ,

Sehemu ya pili ni Nafsi(ufahamu utashi) ambao kumbukumbu akili ufahamu conscious,subconscious ..hii hudumu milele haifutiki.MEMORY au AKILI.

Sehemu ya tatu ni ROHO ambayo ni pumzi ya uhai haifi.
Mwili ambao asili yake ni uharibifu na MAUTI hufa..huwa unazeeka,kuugua,kuchoka n.k. LAKINI

ROHO always ni kijana au mtoto kama teenage ROHO HAIZEEEKI iko vile vile ,sio mrefu sio mfupi,ni kijana muda wote,.kama ulivyo jiona ,ulivo ota uko teenage ndotoni..ndio binadamu wote ni vijana katika ulimwengu wa Roho ,haizeeki ,haifi.

MWILI+NAFSI+ROHO=MWANADAMU

SO HAYO ULIYO OTA na ulivyojiona ndio wewe ulivyo katika ulimwengu wa ROHO.

NDOTO ZOTE ZINA MAANA ,PIA NDOTO ZOTE NI HALI HALISI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.
Hasa ndoto unayoiota ukakosa amani,ina maana unatakiwa uchukue hatua ya haraka ,mana Yanayodhihirika kutokea katika ulimwengu wa MWILI huanza kwanza kutokea katika ulimwengu wa Roho.
Kabla kitu hakijatokea machoni huanza kwanza kufanyika katika ulimwengu wa ndoto halafu kinakuja kutokea LIVE baade au unakuta ndio hali halisi unayoipitia kiroho kwa wakati huo.

2.KUOTA UNAKIMBIZWA Mana yake kuna Roho za giza zinazokufuatilia maisha yako..au nguvu za giza kama wachawi,mizimu ya ukoo,mapepo,n.k

3.KUona watu miguu lakini sura hiwaoni...HIYO ni kawaida ya watu wabaya au roho za giza ambazo ni adui hutumia njia ya kujifunika sura/kujificha utambulisho wao wasionekane..WACHAWI huwa wanajificha SURA wasitambulike,LAH wasipojificha sura usiwatambue basi watavaa SURA ya mtu wa wa karibu yako unayfahamu kama ndugu yako, kaka,dada,wazazi wako ili kukufarakanisha ja jamaa zako(MCHAWI HATAKIWI KUTAMBULIKA)..na endapo ukamuona sura kwenye ndoto na ukamtambua hata yeye atajua umemtambua hata kesho ukimsalimia hataitika mana atajua ulimuona kwenye ndoto na ukamtambua,Usipomuona sura na kumtambua kama hivyo ,hivyo ndivyo wanavyopenda.

KUOTA UPO KIFUNGONI/UMEFUNGIWA KWENYE CHUMBA..Mana yake umefungwa katika ufahamu( NAFSI)mana kama kwa uhakisia upo mjini lakini wewe ukiwa ndani ya kifungo hata mji hu wenyewe huoni ila unaona upo porini au kwenye kijumba.(vision imefungwa)
UKIWA KIFUNGONI mana yake MAMBO YAKO MENGI YAMEFUNGWA..hata vision yako,na mambo yako kadhaa maeneo fulani yatakua yamefungwa ..
KUTOKEWA TENA na mtu mbaya aliyejificha sura na kukutaka URUDI PORINI kwa vile kule una mtoto wako..
Maana yake bado kuna ROHO ZA ADUI nguvu za giza zinakufuatilia na una maagano nazo,pengine uliingizwa kwenye maagano bila wewe kujua labda na MIZIMU YA UKOO,ama na wachawi kupitia vitu mbalimbali au hata ndotoni umeingia mikataba au mapepo ndotoni,au waganga wa kienyeji kama si wewe au ukoo,
na YANASEMA una mtoto kule porini,huenda una mtoto wa kiroho na hayo maroho ya giza,.MIKATABA mikataba mingine ni ya damu ya ukoo toka enzi za mababu na mabibi.hata kabla ya wewe hujazaliwa.

NINI CHA KUFANYA SULUHISHO.
YESU PEKEE ndiye anayeweza kumuokoa mwanadamu kutoka katika nguvu za giza akamuhamisha na kumuingiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake..
VUNJA ROHO ZA MAAGANO na kataa roho zinazokufuatilia zikemee kwa jina la YESU
OMBA SALI,
FUNGA maombi ya KUFUNGA NA KUOMBA yana MAJIBU YA HARAKA na yana NGUVU KUBWA SANA NI MOTO MKALI SANA UNAUNGUZA NGUVU ZOTE ZA GIZA .
 
Usiumie Sana akili sababu haya mambo ukiyapotezea yanakimbia mana yanaona hayapo sehemu sahihi lakini lazima utagombana Na ndugu Kwa maana utakuwa umeukana ukoo kimtindo.
Nayapotezea tu, maana hata sijui cha kuhangaika nacho hapo ni nini!
Ila ikumbuke ahadi hiyo ndio ambayo itakusumbua itekeleze ili ufanye mambo mengine Kwa Amani.
Nitajaribu kukumbuka kama kuna ahadi nilitoa ambayo sijaitimiza.
Si unajua mtoto ukimtelekeza lazima atakusumbua Kwa simanzi Yake 😂😂😂 Rudi umfate mtoto wako
I hope mtoto unamaanisha hiyo ahadi na si mtoto kweli!
 
Amen
 
Ndoto yako ni njema. Ni muongozo unaotakiwa kuufuata. Ndoto imekukumbusha maisha yako ya nyuma na namna ulivyokwepa viunzi kadhaa katika maisha yako kwa msaada usioutarajia. Mwisho ndoto inakukumbusha ni wakati sahihi kukumbuka malengo yako uliyowahi kuyafikiria na kwa wakati huu unaweza kuyatimiza kwa kuwa tiyari unafahamu kuna nguvu inayokuongoza na kukulinda.

Kila la heri haujachelewa nenda katimize ndoto zako.
 
Sawa, nitafikiria hili swala la kuokoka.

Ila umesema haya ni matatizo, kwa uelewa wako wa kiimani, tatizo kubwa la hii ndoto ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…