Watanganyika ajira za TRA 1574 Wazanzibar wametengewa 21%

Watanganyika ajira za TRA 1574 Wazanzibar wametengewa 21%

Heshima sana wanajamvi.

TRA wametangaza ajira mpya 1,574.

Hili ni jamba zuri sana vijana wetu watapata ajira za uhakika zenye mishahara mizuri na nafasi kubwa ya kutengeneza kipata cha ziada kupitia urefu wa kamba zao.

Kitu wasichakijua WATANGANYIKA katika ajira hizo WAZANZIBAR wametengewa nafasi 331 huku WATANGANYIKA MACHOGO wakitengewa 1243 tu.

Idadi ya watu TANGANYIKA ni zaidi ya 64 Million idadi ya watu ZANZIBAR ni 836,000.
Hizi hesabu nimejaribu kuzipiga,kugawanya,kuzidisha nimetoka kapa.

Huu upuuzi uliletwa na Mchengerwa katika bunge hili linalomaliza muda wake WABUNGE wetu hawakuhoji,hawakudadisi,hawakuuliza waligonga meza kama kawaida yao.

Wakati LISSU akishangaa idadi ya wabunge wa ZANZIBAR kuchanguliwa na wastani wa watu 11,000 tu wakati wabunge wa TANGANYIKA wanachaguliwa na idadi ya watu 300,000 na kuendelea angejiuliza na kudadi inakuwaje WAZANZIBAR wanatengewa nafasi 331 katika taasisi moja tu.Siku BOT wakitangaza ajira utaratibu ni huo huo.

Lissu badala ya kutazama nafasi za kisiasa pekee yake angetazama pia suala zima la ajira katika hii JMT.
CCM hawaitendei haki Tanganyika kwa kuendelea kumuendekeza Samia
 
Ninavyo fahamu Wizara ya Uchukuzi sio ya Muungano.

Kwahiyo hao Wazanzibar hawakupaswa wahusishwe na hizo ajira za SGR

Hata kama wangeruhusiwa, ilipaswa iwe ni asilimia 4 tu

Kwahiyo asilimia 4 ya ajira 1574 zilipaswa ziwe ajira 63 tu kwaajili ya Wazanzibar na ajira 1511 zibaki Kwa Watanganyika

By the way Kwa kuwa hakuna anayesemea hayo mambo, zaidi ya Tundu Lissu basi wacha tuendelee kuliwa hadi akili ziturudie 🙌
 
Kumbe ni udini?
Mnaogopa mpaka jina?
Yusufu wako wengi sana mbeya na bara yote
Mkuu umekula lunch ?..maana njaa ikiwa inauma akili haifanyagi kazi, kwanini umeniandikia vitu ulivyoandika hapa wakati mimi nlikuwa na co-sign alichosema jamaa kuwa CG ni mtu wa mbeya na mimi nikamtaja yes jamaa sio mpemba sababu kina mwenda ni watu wa iringa, njombe na mbeya. Bwana mkubwa tatizo lake nini?
 
Vipi ZRA watanganyika ni % ngapi? Watu wachangamkie fursa huko kisiwani?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Je, nyie Wazenji mna uwezo wa kubeba gharama zote za uendeshaji wa JMT kwa 50/50?!
Au mnavizia tu ulaji halafu mnadai hiyo 50/50?
Sasa mie hayo hayanihusu, wewe ndie ulitaka ubia, gharama ni zako zote, ni sawa tu na kujenga nyumba za ubia,

We umeona wapi mwenye eneo akatoa mchango, zigo lote ni la mbia aliyekuja, yaani hapa salama yenu ni muiachie tu zenji na mambo yake
 
Back
Top Bottom