Kama mkataba uwe halali unahitaji idhini ya UAE, si kuna umuhimu wa hiyo idhini iwe sehemu ya mkataba na isiwe tu assumption kuwa idhini ilitolewa?
Mkataba wenyewe tumeupata kwa kuvuja, hatujaupata kwa njia rasmi.
Unajuaje kwamba tumeupata wote?
Unajuaje hiyo idhini haijatolewa sema tu haijawa sehemu ya mkataba iliyovuja?
Ukiangalia mkataba niliouweka hapa utaona kuwa hata instruments of full powers za Dubai tu zimewekwa kama atachment ambayo haipo katika numbered pages za mkataba. Angalia attachment (IGA) nimeiweka post #17.
Pages zote za mkataba zina margin ya kijani, instruments of full powers ya Dubai haina margin ya kijani, ina maana imeletwa separately. Unajuaje kwamba idhini ya UAE haipo separate pia?
Sasa utajua vipi idhini ya UAE haipo, ila haijawa leaked tu, labda aliyeleak mkataba hakuwa nayo, au hakuwa na uda wa kuiscan alikuwa anaibia.
Kitu muhimu ni kwamba, lalamiko la kwamba Dubai hana nguvu ya kusaini mkataba ni lalamiko linalotakiwa kutolewa na UAE. UAE isipotoa lalamiko hili, Watanzania hamtakiwi kulilalalimikia.
Serikali yenu ishakubali kusaini mkataba na Dubai. Dubai ina serikali. Mkataba ni wa serikali ya Tanzania na serikali ya UAE.
Ni kama vile serikali ya Zanzibar isaini mkataba na serikali ya Oman, kama serikali ya Jamhuri ya Muungano haikatazi, au imeipa idhini serikali ya Zanzibar kuingia mkataba huu, watu wa Oman watakosea kuanza kuhoji kama serikali ya Zanzibar ina mamlaka ya kusaini mkataba na Oman, hilo ni jambo kati ya Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Pia, si makubaliano yote yako wazi, IGA yenyewe ian kipengele cha kuweka makubaliano siri.