Watanganyika msihofu bandari zenu zitarudishwa mikononi mwenu na mahakama mkataba uloridhiwa na Bunge ni Void ab initio

Watanganyika msihofu bandari zenu zitarudishwa mikononi mwenu na mahakama mkataba uloridhiwa na Bunge ni Void ab initio

Taifa halisaini mikataba, wanasaini watawala wachache walafi. Ndiyo maana hata wananchi hawapewi nafasi ya kuishauri serikali kabla mikataba haijasainiwa au kupitishwa bungeni.

Na hao watawala nia yao si ustawi wa taifa, nia yao ni kujitajirisha na kuendelea kutawala.

Watu wanatafuta hela za uchaguzi wa 2025 na uhakika wa kutajirika wao na vizazi vyao.

Ukielewa hili, hutashangaa.

Najua Samia ni mjinga, lakini, si mjinga kiasi cha kusaini mkataba kama huu kwa ujinga tu.

Hapa inaonekana kuna mamia ya mamilioni ya dola za Kimarekani yametembea kirushwa.

DPW wana historia hiyo, kina Rostam wana historia hiyo, Samia anapangiwa tu cha kusaini.
Uamuzi kama Taifa tufanye nini?
 
Wanasema Dubai haina nguvu za kusaini mkataba wa kimataifa, mikataba ya kimataifa ni kazi ya UAE.

Lakini hata hapo, Dubai inaweza kusaini mikataba ya kimataifa kwa idhini ya UAE, kama Zanzibar inavyoweza kufanya mikataba ya kimataifa kwa idhini ya serikali ya muungano.
Kwa kuwa emir wa dubai ndio waziri mkuu wa uae na ndio mtendaji mkuu wa serikali ya uae yaani federal govt hivyo basi maamuzi ya dubai ni maamuzi ya uae amri ya dubai ni amri ya uae. Ni sawa na mheshimiwa Raisi Mwinyi wa Zanzibar ni makamu wenyekiti ccm maamuzi yake ni halali kama makamu mwenyekiti na ni maamuzi ya ccm na viongozi wa chini wanatii.
 
Kwa kutokuupata mkataba wote rasmi, mengine yanayobaki ni speculations tu. Ikishakuwa issue ya kisheria, ni bora tu kujihakikishia hata kama uwezekano wa hilo kutokea ni mdogo mno.
Hizo ni hoja ulizotakiwa kuzitoa kabla ya mkataba kusainiwa.

Mkataba wenyewe una kipengele cha wewe kutoupata mkataba wote rasmi, hivyo, wewe kuuona mkataba wote rasmi ingekuwa ni kuvunja mkataba. Huu uliouona umeuona kwa kuvuja tu.

Tatizo lako si mkataba, tatizo lako ni viongozi walioingia huo mkataba.

Huelewi wapi?
 
Acha kuongea ujinga. Zanzibar lili ilishasaini mikataba kwa niaba ya Muungano? Wapi Zanzibar ina ubalozozi wa kudumu?
Kwani wapi nimesema Zanzibar imesaini mkataba kwa niaba ya Muungano?

Unaelewa kusoma na kufuatilia hoja kimantiki au unajibu kishabiki tu?

Nakwambia hivi, serikali ya Zanzibar inaweza kusaini mkataba wa kimataifa kati ya serikali ya Zanzibar na nchi ya kigeni, kama mkataba huo umepata idhini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Hapo si kusaini mkataba kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Unaelewa hilo mpaka hapo?
 
Dubai sio state na haina capacity ya kuingia mkataba wa aina yoyote.

Mahakama itatenda haki
Mafisadi wa CCM chini ya mwenyekiti wao wataaibika

Huyu Wasira na pumba zake za kumtusi Lissu ataona aibu
 
Uamuzi kama Taifa tufanye nini?
Ondoeni CCM, wekeni utamaduni wa kusimamia viongozi, maana mkiondoa CM bila kusimamia viongozi yatajirudia hayahaya kwa yeyote, wekeni uwazi wa hii mikataba ili iwe inajadiliwa kwa kina kabla ya kupitishwa, pitisheni katiba mpya inayoondoa mamlaka makubwa sana ya viongozi, hususan rais, ukiweka uhuru wa rais kushitakiwa unapunguza impunity.

Zaidi ya yote, futeni ujinga wa watu wengi, ujinga huu ndio mtaji wa viongozi kufanya wanavyotaka, bila kuuondoa ujinga huu mnaweza kupata katiba mpya na sheria za kuruhusu uwazi, halafu mkashindwa kuzitumia kwa sababu wajinga wengi.
 
Dubai sio state na haina capacity ya kuingia mkataba wa aina yoyote.

Mahakama itatenda haki
Mafisadi wa CCM chini ya mwenyekiti wao wataaibika

Huyu Wasira na pumba zake za kumtusi Lissu ataona aibu
Wewe huelewi unchokiongea, hata wewe unaweza kuingia makubaliano na serikali MoU.

 
Kwa kuwa emir wa dubai ndio waziri mkuu wa uae na ndio mtendaji mkuu wa serikali ya uae yaani federal govt hivyo basi maamuzi ya dubai ni maamuzi ya uae amri ya dubai ni amri ya uae. Ni sawa na mheshimiwa Raisi Mwinyi wa Zanzibar ni makamu wenyekiti ccm maamuzi yake ni halali kama makamu mwenyekiti na ni maamuzi ya ccm na viongozi wa chini wanatii.
Hapana,

Inategemea anafanya maamuzi kwa capacity gani.

Ujue hata Rais wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kuna vikao anaingia kama Mwenyekiti wa CCM, anafanya maamuzi kama Mwenyekiti wa CCM, na kuna vikao anaingia kama Rais, anafanya maamuzi kama rais.

Hatusemi kwamba kwa kuwa mtu mmoja huyu ni Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, basi maamuzi yake yote ni ya Rais na ya Mwenyekiti wa CCM pia.

Kwa mfano, Rais ana uwezo wa kulivunja Bunge, Mwenyekiti wa CCM hana.

Samia akitaka kulivunja Bunge, atalivunja kama Rais, hawezi kulivunja kama Mwenyekiti wa CCM.

Full Instruments of Power kwenye mkataba uliovuja zimetoka serikali ya Dubai.
 
Wavunje huo mkataba, uwe Void au laa, watamke kwamba umevunjwa..

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Hapana,

Inategemea anafanya maamuzi kwa capacity gani.

Ujue hata Rais wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kuna vikao anaingia kama Mwenyekiti wa CCM, anafanya maamuzi kama Mwenyekiti wa CCM, na kuna vikao anaingia kama Rais, anafanya maamuzi kama rais.

Hatusemi kwamba kwa kuwa mtu mmoja huyu ni Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, basi maamuzi yake yote ni ya Rais na ya Mwenyekiti wa CCM pia.

Kwa mfano, Rais ana uwezo wa kulivunja Bunge, Mwenyekiti wa CCM hana.

Samia akitaka kulivunja Bunge, atalivunja kama Rais, hawezi kulivunja kama Mwenyekiti wa CCM.

Full Instruments of Power kwenye mkataba uliovuja zimetoka serikali ya Dubai.
Simple tu kwa kuwa emir wa dubai ndio waziri mkuu wa uae na mtendaji mkuu wa serikali yaani federal govt ya uae basi maamuzi ya emir wa dubai ni maamuzi ya uae kwa kuwa always since creation ya uae dubai wao ni vice president na waziri mkuu na utendaji wa serikali uko chini yao maamuzi yao ni maamuzi ya uae .
 
Simple tu kwa kuwa emir wa dubai ndio waziri mkuu wa uae na mtendaji mkuu wa serikali yaani federal govt ya uae basi maamuzi ya emir wa dubai nia maamuzi ya uae kwa kuwa always since cteatin ya uae dubai wao ni waziri mkuu na utendaji wa serikali uko chini yao maamuzi yao ji maamuzi ya uae .
Hilo si kweli.

Lakini, hata lingekuwa kweli, issue ya "Dubai si nchi" ndiyo ingezidi kukosa nguvu.
 
Dubai sio state na haina capacity ya kuingia mkataba wa aina yoyote.

Mahakama itatenda haki
Mafisadi wa CCM chini ya mwenyekiti wao wataaibika

Huyu Wasira na pumba zake za kumtusi Lissu ataona aibu
Binafsi nauona usaliti, usaliti uliofanywa na waliofungua kesi na mawakili wanaojidai kuwatetea walalamikaji. Naita usaliti saba kesi hii haikutakiwa kufunguliwa, ilatakiwa nginja nginja hii waachiwe wanahatakati na wanasiasa. Naita wasaliti sababu ikitojea maamuzi ya mahakama ikawapa ushindi Selikari maana yake hoja hii ya kupinga mkataba itakuwa imekufa na kuua uanaharakati. Ndio maana wengine tukiwa tunapambana na mdai hatuendi mahakamani tuna ng'ang'ana na mdai wetu mpaka mwenyewe anyoshe mikono, sababu ukimpeleka mahakamani akashinda ndio mwisho wa madai yetu.😭😭
 
IGA si two state agreement, ni two governments agreement. Kuna tofauti.

Unaweza kusaini IGA hata kati ya serikali ya wilaya na serikali ya mkoa. Hizo si states.

Suala la muhimu si nani anasaini, suala la muhimu ni anasaini kwa niaba ya nani na kama ana idhini ya kusaini.

Upande uliosainiwa na kampuni ni upi? aliyesaini ni nani? je, ana full instruments of power ku saini?
What is a state?
 
Binafsi nauona usaliti, usaliti uliofanywa na waliofungua kesi na mawakili wanaojidai kuwatetea walalamikaji. Naita usaliti saba kesi hii haikutakiwa kufunguliwa, ilatakiwa nginja nginja hii waachiwe wanahatakati na wanasiasa. Naita wasaliti sababu ikitojea maamuzi ya mahakama ikawapa ushindi Selikari maana yake hoja hii ya kupinga mkataba itakuwa imekufa na kuua uanaharakati. Ndio maana wengine tukiwa tunapambana na mdai hatuendi mahakamani tuna ng'ang'ana na mdai wetu mpaka mwenyewe anyoshe mikono, sababu ukimpeleka mahakamani akashinda ndio mwisho wa madai yetu.😭😭
Hapana
 
Mkataba wenyewe tumeupata kwa kuvuja, hatujaupata kwa njia rasmi.

Unajuaje kwamba tumeupata wote?

Unajuaje hiyo idhini haijatolewa sema tu haijawa sehemu ya mkataba iliyovuja?

Ukiangalia mkataba niliouweka hapa utaona kuwa hata instruments of full powers za Dubai tu zimewekwa kama atachment ambayo haipo katika numbered pages za mkataba. Angalia attachment (IGA) nimeiweka post #17.

Pages zote za mkataba zina margin ya kijani, instruments of full powers ya Dubai haina margin ya kijani, ina maana imeletwa separately. Unajuaje kwamba idhini ya UAE haipo separate pia?

Sasa utajua vipi idhini ya UAE haipo, ila haijawa leaked tu, labda aliyeleak mkataba hakuwa nayo, au hakuwa na uda wa kuiscan alikuwa anaibia.

Kitu muhimu ni kwamba, lalamiko la kwamba Dubai hana nguvu ya kusaini mkataba ni lalamiko linalotakiwa kutolewa na UAE. UAE isipotoa lalamiko hili, Watanzania hamtakiwi kulilalalimikia.

Serikali yenu ishakubali kusaini mkataba na Dubai. Dubai ina serikali. Mkataba ni wa serikali ya Tanzania na serikali ya UAE.

Ni kama vile serikali ya Zanzibar isaini mkataba na serikali ya Oman, kama serikali ya Jamhuri ya Muungano haikatazi, au imeipa idhini serikali ya Zanzibar kuingia mkataba huu, watu wa Oman watakosea kuanza kuhoji kama serikali ya Zanzibar ina mamlaka ya kusaini mkataba na Oman, hilo ni jambo kati ya Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Pia, si makubaliano yote yako wazi, IGA yenyewe ian kipengele cha kuweka makubaliano siri.
Mbona unajichanganya braza, unatetea usichokijua mara imevujishwa sasa kitu kilichovujishwa uwa haina uhalisia mbona unaitetea?

Tanganyika hamko serious nyie ujinga umewatawala aise
 
Hatujauza Bandari. Tunaweza kuuvunja mkataba kwa namna mbili tu.

1. Kuwaomba DPW tuvunje makataba, wakakubali. Hapa uwezekano wa hili kutokea ni karibu na sifuri.

2. Kwenda kwenye usuluhishi wa kimataifa. Ambapo piga ua galagaza tutapigwa faini, tulipe faini kwa kuvunja mkataba. Tundu Lissu anashauri tufanye hivi, kwa sababu tutapigwa faini, lakini itakuwa ndogo tukiwahi mapema, kadiri tunavyozidi kuchelewa ndivyo faini itakavyozidi.

Pia, tunaweza kuongea na DPW tubadili vipengele vya mkataba, tuurudishe bungeni, upate ratification upya, lakini hapa tutategemea huruma za DPW kama option 1 hapo juu, na most likely watakataa na tutaishia kwenye usuluhishi kama option 2 hapo juu.

Vyovyote vile, hakuna ku nullify mkataba bila faini hapo.

Tumecheza ule mchezo wa chess ambapo viongozi wameona wanakula, wanakula, wanakula kete, mwisho wake wanajikuta wamefungwa kwa checkmate, hawana pa kucheza, mchezo umeisha.

Uroho wao umewaponza.

Mkataba huu uneshabadiki sheria za Tanzania kwa namna ambayo maliasiki za Tanzania zimepunguziwa ulinzinwa kisheria, kwa hiyo, hata tukivunja mkataba huu, madhara yake ni zaidi ya mkataba wenyewe, kwa sababu umeshabadiki npaka sheria tayari.

Madhara yake yatakuwapo kwenye mikataba yote inayofuata.

Zaidi ya mkataba, tunatakiwa pia tufute mabadiliko ya sheria yaliyoletwa na mkataba huu.

Yani hata tukiuvunja mkataba, tusi deal na DPW tena, madhara yaliyofanywa na mkataba kwenye kubadili sheria bado yapo, mpaka tuondoe mabadiliko ya sheria yaliyotokana na mkataba.
Vichwa maji CCM wameleta balaaa kubwa kabisa
 
Why is the question of "what is a state" important here?

Umesoma na kuelewa nilichoandika ukakinukuu?

Au unauliza maswali kwa kukariri tu?
Nenda kasome mkataba wa Montevideo. Sio unadandia mada wakati kichwani ni bumunda
Screenshot_20230730-071849.jpg
 
Back
Top Bottom