Lengo la hizi post zenu ni kuharibu kesi iliyopo mahakamani kwamba Mahakama itoe uamuzi unaolenga kuonesha haishinikizwi na social medias.
Mnatuharibia sana sana nyie vibaraka.
Tupambanie rasilimali zetu na heshima ya nchi.
Ambaye hajaelewa dhima ya hii post yako ataona kana kwamba nawe unapambania bandari
Mkuu,
Hii point ya "Dubai si nchi" itatupiliwa mbali na jaji yeyote anayejua sheria.
Kwanza hili ni suala la UAE kulalamika, kama UAE haijalalamika, sisi hatuna haki ya kulalamika. Tutalalamika kama nani wakati ikiwa Dubai imeingia mkataba kinyemela aliyevunjiwa haki ni UAE?
Yani ni hivi, serikali ya UAE ingefungua kesi dhidi ya serikali ya Dubai, katika mahakama ya Tanzania, kusema kwamba serikali ya Dubai imeingia mkataba na serikali ya Tanzania, bila ya idhini ya serikaLi ya UAE, hapo kungekuwa na kesi ya kusikilizwa.
Au kungekuwa hata na malalamiko kutoka serikali ya UAE, kuwa Dubai imeingia mkataba kinyemela na Tanzania, then hayo malalamiko yangeweza kutumiwa kuanzisha kesi, kusema kuwa Dubai imeingia mkataba kinyemela.
Sasa wewe Mtanzania unalalamikaje Dubai si nchi wakati UAE wenyewe hawajalalamika? Wakati serikali yako yenyewe imeridhika?
Unalalamika Dubai si nchi, wakati Emir wa Dubai ni Prime Minister na Vice Emir wa UAE?
Hivi kweli hapo unafikiri Dubai inaweza kuingia mkataba mkubwa kama huu bila idhini ya UAE?
Unafikiri wanasheria wapigaji wa kimataifa, economic hitmen wale wa DPW ni wajinga hivyo?
Mkataba mbaya, una mengi ya kupinga, lakini hii habari ya "Dubai si nchi" itapigwa chini tu. Na hata jaji aki entertain hili, atakachofanya ni kutaka uthibitisho kwamba UAE imeipa idhini Dubai kuingia mkataba wa IGA na Tanzania. UAE ikithibitisha hilo tu, hili dai linakuwa halina nguvu. Linatupiliwa mbali
Watu wanakuwa wamepoteza muda na nishati kwa dai la null and void ya fantasy.
Yani hamshangai UAE haijalalamika Dubai imeingia mkataba na Tanzania, wabongo wanataka kulazimisha Dubai haikupewa nguvu za kuingia mkataba?
Watu wanapenda sana kujifariji kwa kujipa ushindi wa mitandaoni.