Watanganyika msihofu bandari zenu zitarudishwa mikononi mwenu na mahakama mkataba uloridhiwa na Bunge ni Void ab initio

Utahangaika sana ndugu, Dubai sio state, kitendo cha kusaini nayo mkataba kama state party ni void ab initio
 
Utahangaika sana ndugu, Dubai sio state, kitendo cha kusaini nayo mkataba kama state party ni void ab initio
Mkataba wa IGA si lazima entity iwe state.

Inaweza kuwa non state government.

Nimekupa mfano wa Hong Kong. Hong Kong si state, lakini imeingia IGA na USA, ambayo ni state.

Same way Dubai si state, imengia IGA na Tanzania ambayo ni state.

IGA si Inter State Agreement. Ni Inter Government Agreement.

Usichanganye mambo.

As long as state entity imetoa idhini, hata serikali ya kijiji cha UAE inaweza kuingia IGA na serikali ya Tanzania.

IGA ya serikali ya Hong Kong (non state government) na USA (state government) hii hapa kama ushahidi.

 
Nijuavyo mimi Dubai ni sehemu ya The emirates, hivyo inaweza kusaini mikataba ya kimataifa kama tu itapata idhini ya The emirates

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nijuavyo mimi Dubai ni sehemu ya The emirates, hivyo inaweza kusaini mikataba ya kimataifa kama tu itapata idhini ya The emirates

Sent using Jamii Forums mobile app
Exactly.

Sasa kwa nini watu wanasema kuwa Dubai si nchi, na hivyo haiwezi kusaini mikataba ya kimataifa?

Wakati inaweza kupata idhini ya UAE na kusaini mikataba ya kimataifa.

Hapa kitu kigumu kuelewa ni kipi?

Au watu wanataka kulazimisha wanachotaka wao tu, bila kujali ukweli wa mambo?
 
Labda kwakuwa Dubai hawaweka wazi ruhusa yake toka UAE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dubai sio state na haina capacity ya kuingia mkataba wa aina yoyote.

Mahakama itatenda haki
Mafisadi wa CCM chini ya mwenyekiti wao wataaibika

Huyu Wasira na pumba zake za kumtusi Lissu ataona aibu
Lengo la hizi post zenu ni kuharibu kesi iliyopo mahakamani kwamba Mahakama itoe uamuzi unaolenga kuonesha haishinikizwi na social medias.

Mnatuharibia sana sana nyie vibaraka.

Tupambanie rasilimali zetu na heshima ya nchi.

Ambaye hajaelewa dhima ya hii post yako ataona kana kwamba nawe unapambania bandari
 
Mkuu,

Hii point ya "Dubai si nchi" itatupiliwa mbali na jaji yeyote anayejua sheria.

Kwanza hili ni suala la UAE kulalamika, kama UAE haijalalamika, sisi hatuna haki ya kulalamika. Tutalalamika kama nani wakati ikiwa Dubai imeingia mkataba kinyemela aliyevunjiwa haki ni UAE?

Yani ni hivi, serikali ya UAE ingefungua kesi dhidi ya serikali ya Dubai, katika mahakama ya Tanzania, kusema kwamba serikali ya Dubai imeingia mkataba na serikali ya Tanzania, bila ya idhini ya serikaLi ya UAE, hapo kungekuwa na kesi ya kusikilizwa.

Au kungekuwa hata na malalamiko kutoka serikali ya UAE, kuwa Dubai imeingia mkataba kinyemela na Tanzania, then hayo malalamiko yangeweza kutumiwa kuanzisha kesi, kusema kuwa Dubai imeingia mkataba kinyemela.

Sasa wewe Mtanzania unalalamikaje Dubai si nchi wakati UAE wenyewe hawajalalamika? Wakati serikali yako yenyewe imeridhika?

Unalalamika Dubai si nchi, wakati Emir wa Dubai ni Prime Minister na Vice Emir wa UAE?

Hivi kweli hapo unafikiri Dubai inaweza kuingia mkataba mkubwa kama huu bila idhini ya UAE?

Unafikiri wanasheria wapigaji wa kimataifa, economic hitmen wale wa DPW ni wajinga hivyo?

Mkataba mbaya, una mengi ya kupinga, lakini hii habari ya "Dubai si nchi" itapigwa chini tu. Na hata jaji aki entertain hili, atakachofanya ni kutaka uthibitisho kwamba UAE imeipa idhini Dubai kuingia mkataba wa IGA na Tanzania. UAE ikithibitisha hilo tu, hili dai linakuwa halina nguvu. Linatupiliwa mbali

Watu wanakuwa wamepoteza muda na nishati kwa dai la null and void ya fantasy.

Yani hamshangai UAE haijalalamika Dubai imeingia mkataba na Tanzania, wabongo wanataka kulazimisha Dubai haikupewa nguvu za kuingia mkataba?

Watu wanapenda sana kujifariji kwa kujipa ushindi wa mitandaoni.
 
Lakini mkataba mzima haujawekwa wazi, hata tulivyoupata tumeupata kwa ku leak tu, na mkataba una kipengele cha usiri.

Sasa UAE/ Dubai wataweka vipi wazi mambo ya mkataba wakati wao wenyewe wanataka mkataba uwe wa siri?



Kumbe hadi kwenye mkataba wamekubaliana uwe wa siri?!
Kwanini iwe Siri rasilimali yenye maslahi ya Umma ?!
Kipengele hicho tu chaweza kuonesha kuwa kuna hila mbaya na nia ovu.

Lakini wajue Mwenyezi Mungu amekataa Ndiyo mambo yamekuwa hadharani.
 
Kumbe hadi kwenye mkataba wamekubaliana uwe wa siri?!
Kwanini iwe Siri rasilimali yenye maslahi ya Umma ?!
Kipengele hicho tu chaweza kuonesha kuwa kuna hila mbaya na nia ovu.

Lakini wajue Mwenyezi Mungu amekataa Ndiyo mambo yamekuwa hadharani.
Tatizo watu wengi wanaujadili mkataba bila ya kuusoma.

Usiri ni tatizo kubwa, ni chaka la rushwa. Siku hizi mpaka World Bank wana initiative ya kuondoka kwenye mikataba ya siri.

Niliandika makala mwaka 2011 kuhusu kampeni ya kutaka mikataba iwe wazi.

Nilishaliona hili kuwa ni tstizo kubwa tangu angalau 2011.


Huwezi kuwa na mazungumzo mapana ya wananchi kukubali mikataba kama mikataba inakuwa ya siri.

Tunaona wenzetu kama Marekani wameweka IGA yao na Hong Kong wazi, unaipata kwenye tovuti rasmi za serikali.

Lakini pia, kwa bahati mbaya sana, usiri ni kipengele cha kawaida kabisa katika mikataba hii.

Kichekesho hapa ni kwamba, wanataka mkataba upitishwe bungeni, halafu hapo hapo uwe siri.
 
Tanzania ilisaini mkataba wa Montevideo, kuingia mkataba na na nchi ambazo hazina hadhi ya kuingia mikataba ya kimataifa ni makosa. Hivyo huu mkataba ni batili
 
Huu mkataba umeitambua dubai kama state, jambo ambalo ni kosa na ndio maana ni batili
 
Sasa mbona huna akili hata kidogo kuhusu Dubai? Dubai ina kiti UN? Kuna balozi wa Dubai hapa!? Hiyo haki ya kusaini mikataba umeshaiona kwamba UAE aliwapa hao Dubai? Nitajie jina la aliyesaini mkataba upande wa Dubai. Tumia kichwa kuwa sio kama dispenser ya mate nyau wewe
 
Tanzania ilisaini mkataba wa Montevideo, kuingia mkataba na na nchi ambazo hazina hadhi ya kuingia mikataba ya kimataifa ni makosa. Hivyo huu mkataba ni batili
You are so dense it is not funny.

Ni hivi, UAE ni nchi kamili. Inatambulika UN, inatambulika na Montevideo Convention.

UAE ina Emirates saba.

Nchi zote kamili zinazotambulika na Montevideo Convention zina haki ya kuzipa nguvu ya kusaini mikataba ya kimataifa serikali ndogo zilizo ndani ya nchi hizo.

China imeipa Hong Kong nguvu hii kusaini IGA na USA. Nimeweka IGA hapa. Inaonekana UAE imeipa nguvu hii Dubai kusaini IGA na Tanzania.

UAE inaweza kuzipa ruhusa Emirates zake ziingie mikataba ya kimataifa. Ndicho kilichotokea hapa.

Usichoelewa kipi hapo?

Au unataka kuishi katika fantasy ya "Dubai si nchi, mkataba batili" tu?
 

Akili ni nini?

Kwani kusaini IGA ni lazima kuwa na kiti UN?

Hong Kong imesaini IGA na USA, Hong Kong ina kiti UN?

Soma IGA hii hapa

 
Huu mkataba umeitambua dubai kama state, jambo ambalo ni kosa na ndio maana ni batili
Mkataba umeitambua Dubai kama state wapi na kwa muktadha gani?

Unajua makubalianonya delolvement of full instrumenys if national power kati ya UAE na Dubai kwenye mkataba huu?

Marekani kuna states 50, lakini hazina full instruments of national power kwa muktadha wa Montevideo Convention.
 
Soma preamble ya mkataba. Wewe ni bumunda unachanganya mambo kibao.
 
Mbona hatujaona hiyo idhini ya UAE kwenye wale signatories wala power of attorney........wamesaini wahuni wasiojulikana.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…