Watangazaji wa Azam TV wamekuwa wakirudia nguo

Watangazaji wa Azam TV wamekuwa wakirudia nguo

Mishahara sio item pekee ya gharama za uendeshaji
We unajua mtu akifanya kazi azam basi ndo ana mihela ila ukweli wanalipwa hela ya kawaida sana pale azam malipo hayaendani na brand.
 
Kama vipindi ni vizuri, unasikia vizuri wakizungumza na unaelewa inatosha.

Azam TV sio Fashionista, jukumu lake kuu ni kuwasilisha programs mbalimbali katika hadhira yake.
 
Kwahiyo mwanaume anatakiwa kuwa rafu?
Kuwa na nguo chache ndo kuwa rafu, unatakiwa kuwa nazo ngapi ndo uonekane smart........unaleta udaku JF? itabidi mods. mfanye utaratibu jukwaa tayari limeingiliwa na watoto.......
 
Acha ushamba Basi wewe mnyaturu kumbuka Ile ni media na pia vipindi wanavyofanya ni tv shows so wanatakiwa kuwa nadhifu.
Kwanza we ni jinsi gani kabla ya yote? Usiulize jinsi ni nini, najua ushazoea kusikia " jinsia" which is wrongly used kama nomino.

Nimeuliza jinsi kwa sababu kama ni mtoto wa kiume nitashangaa unapataje muda aisee mpaka wa kugundua hilo. Ila, kama ni mtoto wa kike sawa sitashangaa. I

nawezekana ukawa ni mvulana au binti.
 
Kwanza we ni jinsi gani kabla ya yote? Usiulize jinsi ni nini, najua ushazoea kusikia " jinsia" which is wrongly used kama nomino.

Nimeuliza jinsi kwa sababu kama ni mtoto wa kiume nitashangaa unapataje muda aisee mpaka wa kugundua hilo. Ila, kama ni mtoto wa kike sawa sitashangaa. Inawezekana ukawa ni mvulana au binti.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kuna kitu kinatafutwa hapa lol.
 
Sio uchawi mkuu Mimi ni mfatiliaji Sana wa vipindi vyao na Kiukweli ni vipindi vizuri sana tatizo pamba babaaa Yani pamba hzohizo daily basi Bora hata waazime sikumoja moja au wawekewe uniform Kuna mmoja analifulana la picha ya ramani basi wiki haipiti kaivaa dah shida Sana
Sisi tunaoangalia tv Imaan kila siku kanzu nyeupe peeee! Si utasema hawavai nguo kabisa?
 
Mtu ukiwa na njaa,ni lazima kila kitu utakiona, Maana muda wote unakodoa macho tu,kwa kuwa unakuwa huna cha kufanya, yaani inafikia muda unahesabu mpaka misumari ya bati ilivyogongelewa
 
Kuwa na nguo chache ndo kuwa rafu, unatakiwa kuwa nazo ngapi ndo uonekane smart........unaleta udaku JF? itabidi mods. mfanye utaratibu jukwaa tayari limeingiliwa na watoto.......
Utoto unaleta wewe sababu huna upeo jaribu kujua content ya mada husika usmart ni unadhifu na unadhifu unajumuisha usafi na ubora wa mavazi kwa maana ya kupendeza.kila sehemu inautaratibu unaoendana na sehemu husika inaweza kuwa rasmi au uliozoeleka.

Hapa hatuzungumziii mavazi kwa mtu tuuu tunazungumzia mavazi ya mtu maalum kwenye shughuli maalum ndio maana ukiwa mgodini Kuna mavazi yake na taratibu zake nasehem nyingine.Mukhtadha wa unadhifu ktk mada yetu unagusia watangazaji ambao hawajipendi hyo ndio tafssiri nyepesi hatuwezi kuwaita nadhifu katu.
 
Back
Top Bottom