Tetesi: Watangazaji wa kike TBC wagoma baada ya kutakiwa kuvua Hijabu zao wakati wa kutangaza

Tetesi: Watangazaji wa kike TBC wagoma baada ya kutakiwa kuvua Hijabu zao wakati wa kutangaza

Sidhani kama ni kweli.
Citizen TV ya Kenya iliyo bora ukanda wa East Africa wanaachia Kina Lulu Hassan siku zote wakijimwaga
Yote kwa yote ni haki yao Kugoma kama wamelazimishwa Kukaa vichwa wazi.
Naunga mkono Maamuzi yao na Mungu awazidishie kwa kujitambua na Kutaambua Maamrisho ya Allah
Mmmh Lulu hassan! Hivi kujistiri ni kuficha nywele tuu!!??? Maana hayo magauni ya huyo lulu yanaonesha mophology yoote aliyopewa na Muumba..
 
Wamesha pata sababu mbona siku zote tunawaona vichwa wazi wasidanye watu kwamba wao ndo washika dini
 
Tunapoteza muda kujadili post au vitu visivyo na tija katika maisha yetu!kwani kuvaa hijab ndo kutakufanya uonekane mtakatifu au mcha Mungu sana?tunakoelekea tutaanza kujadili masuala ya nani anahaki ya kuchinja!na nani hana haki!upuuuuzi tu!
Njoon Lindi huku muone wadada na hijabu zao wapo bar na bia zao zinashuka tartiiibu...wakati iman yake na vazi lake vinamkataza kukaa bar.
 
hiitaarifa itakua ya uongo maana hijab znavaiwa mpk mashuleni mbn...ila na wao kila cku hawavai mpk mfungo ufike!!!! kama wanajiheshimu wawe wanavaa kila cku waache unafiki
 
Na upande wa pili wavae Rozari na Misalaba shingoni?
Mi napendekeza mtangazaji asionyeshe imani yake kwenye chombo cha umma
 
Huu ndio haswa uchochezi katika ubora wake...kama ulikuwa huna uhakika hukuwa na sababu ya kutoa taarifa sensitive kama hii ..lengo lako sio zuri kabisa..unafanya watu waanze kuhemka wakati chanzo cha habari ni uzushi...Watanzania wapenda amani tuwaepuke watu kama hawa hawaitakii mema nchi yetu....
 
Islam siyo Dini ya Serikali wala ya Taifa letu. Ukiona TBC haikufai ondoka zako kwani lazima ufanye kazi TBC? Kwani wakati unaajiliwa hapo TBC uliajiliwa kwa sababu ya Dini yako au kwa sababu ya Taaluma yako? Hebu tuondoleeni ukilaza humu ndani. Taasisi za kiislam zipo nyingi sana, Kuna Radio Imani, Bakwata,Misikitini, Muslim foundation,N.k Waende huko wakaajiriwe hapo TBC hatuhitaji mavazi mengine tofauti na tuloyazoea ,Fuateni sheria za Taasisi husika hutaki sepa zako sio lazima uwepo TBC tupo wengine mtaani hatuna ajira na tunadigriiza utangazaji lakini tumekosa ajira hivyo kuondoka kwenu sisi tutapata ajira. Ondokeni haraka sana hapo ili tuje kuomba nafasi.
 
(NIMEIKUTA SEHEMU HII MWENYE UHAKIKA ATUJULISHE ZAIDI)

TAFADHALI KWA WAISLAM NA WAPENDA HAKI TUFUATILIE HILI KUJUA UHALISIA WAKE.

Kuna taarifa kua watangazaji wa kike Waislam wa TBC TV wamegoma baada ya uongozi kuwataka kuvua hijab wanapotangaza.

Ieleweke ya kuwa wengi wao hupenda kuvaa hijab hususan katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani. Taarifa zinadai kesho asubuhi kuna kikao kujua hatma yao.

TBC TV ni chombo kinachoendeshwa kwa kodi zinazotokana na wananchi wa Tanzania ambao Waislam ni sehemu ya walipa kodi.

Ikithibiti hivyo itaonesha ni namna gani nchi zetu zinakoelekea, asiyejisitiri anaheshimika na anaejisitiri anatakiwa kuvua sitara yake..
Kuvaa hijab au kujihifadhi mwanamke ni shurti, lakini hao wa hijab ya siku 30 halafu baada ya hapo wanarudi kwenye vimini na mipasua haingii akilini. Mwenyezi Mungu hajasema wanawake wajihifadhi ktk mwezi wa ramadhan tu.

Huu ni mwezi wa kuongeza bidii katika ibada lakini ucha Mungu na kujistiri ni maisha yako yote baada ya kubaleghe.
 
kwani hijabu ni vazi la kidin au vazi la stara ?ikiwa ni vazi la kidin ni mtazamo wa mtu na uelewa wa mtu ukweli hijab ni vazi la stara tena kwa mwanamke tbc waangalie upya wasikurupuke mbona huko kunapotungw a sheria wabunge wengi wa kike wanajistiri kw a mavazi hayo
 
Kama ni kweli,Jana nilimwona Asha Haji katupia hijab nyekundu.Kiukweli alikua hajapendeza kabisa, na huenda kuna watu walitoa taarifa uongozi wa TBC, kwani aliifunga ka mtu ambaye hajui inafungwaje na kuvaliwaje.

Nadhani inabidi Zuhra Yunus apewe mchongo wa kuwafundisha jinsi ya kuifunga. kwani hata tai sio kila mtu anajua kuifunga.
issue sio linafungwaje na wala sio issue ya kupendeza,kazi ya msingi ya hijab ni stara,kupendeza ni secondary function,kama ni kweli vazi hilo limekatazwa kuna hoja ya kujadili,lakini ni ngumu kidogo kujadili tetesi.
 
Walipoajiriwa TBC, Waliajiriwa kwa kigezo cha Dini yao au kwa kigezo cha Taaluma zao? Je islam ni dini ya Serikali au ya Taifa la Tanzania hadi watu wote tuitambue? Je huko Zanzibar wakristo wasiotaka kujipatiliza lundo la Manguo nao wanapewa uhuru huo? Je wamelazimishwa kufanya kazi TBC? KWANINI WASIENDE KWENYE TAASISI ZAO WAKATANGAZE IMANI YAO? Mbona wanazo taasisi nyingi tu mfano Radio koroani, Radio Imani, Muslim foundation, Bakwata, Arahamaini n.k ? Ondokeni ili sisi tusio na ajira ambao tunazihangaikia kuzipata na hatuzipati na tunadigrii zetu za utangazaji tukajipatie Ajira. Waondoke haraka sana tupate ajira sisi. Hatupo tayari kutazama miushungi yenu. Tunataka tumuone mtangazaji sura yake ili tuelewe zaidi.
 
(NIMEIKUTA SEHEMU HII MWENYE UHAKIKA ATUJULISHE ZAIDI)

TAFADHALI KWA WAISLAM NA WAPENDA HAKI TUFUATILIE HILI KUJUA UHALISIA WAKE.

Kuna taarifa kua watangazaji wa kike Waislam wa TBC TV wamegoma baada ya uongozi kuwataka kuvua hijab wanapotangaza.

Ieleweke ya kuwa wengi wao hupenda kuvaa hijab hususan katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani. Taarifa zinadai kesho asubuhi kuna kikao kujua hatma yao.

TBC TV ni chombo kinachoendeshwa kwa kodi zinazotokana na wananchi wa Tanzania ambao Waislam ni sehemu ya walipa kodi.

Ikithibiti hivyo itaonesha ni namna gani nchi zetu zinakoelekea, asiyejisitiri anaheshimika na anaejisitiri anatakiwa kuvua sitara yake..
Nani hao wasiojisitiri eneo la kazi? Sijaona anayekwenda kazini tena ofisini ya serikali mtupu.
 
Back
Top Bottom