Watangazaji wa kizazi hiki wanakera mpaka basi. Hivi wanaokotwa wapi hawa viumbe?

Ni kama vile hakuna mamlaka ya kupima ubora wa hivi vyombo vya habari. Mwandishi R na L zinamsumbua, anauliza maswali ya kipumbavu mara kwa mara yaani hovyo kabisa.
 
Yule dogo wa kiume Azam TV mtangazaji wa SHAJARA yupo vizuri sana kwenye kudodosa wageni. Style yake ya maswali mara nyingi unapata picha ni mtu aliefanya research kidogo kuhusu mada husika na kulazimisha watu kutoa ufafanuzi wa kina. Binafsi ndio mtangazaji pekee ninae mkubali.

Star TV miaka ya 2010 walikuwa na makala zinaitwa ‘Hoja Maridhawa’ sijui kwanini waliacha. Katika documentaries za africa sijawahi kuona bora kama zile, producer wa kile kipindi alikuwa ni neutral focusing on issue. Yule producer alikuwa special talent, yaani kipindi kikiisha shule tosha kuhusu issue aliyokuwa anaongelea.

Siku hizi vipindi vingi ujinga mtupu na watangazaji walio na bias za kisiasa au chawa wa viongozi wenye viewpoint zao tayari zinazo athiri representation ya kipindi. Matokeo yake vipindi vingi vinakuwa ovyo mwanzo mwisho.
 
Majina ya watu na vitu huwa yanaanza na herufi kubwa. Ndiyo uandishi wenyewe huu pia tunaongelea. (Usikasirike lakini 😉😉)
 
Ni kama vile hakuna mamlaka ya kupima ubora wa hivi vyombo vya habari. Mwandishi R na L zinamsumbua, anauliza maswali ya kipumbavu mara kwa mara yaani hovyo kabisa.
Chombo cha kupima maudhui ni TCRA lakini wamejikita zaidi kwenye kutoa adhabu kwa watukanaji kuliko hawa wapotoshaji.
 

Bro pole sana. Hilo ni janga la kitaifa. Hali ni mbaya kuliko tunavyodhani. Kuna siku tumejadiri hili kwenye uzi aliouanzisha pascal Mayala kuhusu umahili wa waandishi wa habari. Kwa ujumla ni changamoto, na kikubwa katika ugumu huo ni kwamba hawa watangazaji wanaongea kwa kujiamini sana, huku wakiongea vitu visivyokuwa na uthibitishoau vyenye makosa. Lalafu, kubwa kuliko, wanasikilizwa sana na vijana wa kizazi kipya.
Kufupisha mambo, ushauri ni kuboresha udhibiti wa sifa za watu wanaojiunga na fani ya uandishi. Waongeze minimum requirement au grades za kuingilia kwenye fani.

Lingine wawe na board ya kuwa regulate. Wawe wanasajiliwa ili waweze ku practice kama wahasibu, wagavi n.k.
 
Tag ENZI ZA MWALIM TULIKUA NA WATANGAZAJI KWELIKWELI DEO BURABUZA KIDUDUYE MAREHEM OSTAZI PETER OMARI HAYAT PLENCE BAINA KAMUKULU HAYATI ALEXA NGUSA HOME BOY DIWANI KILUMBA ILIKUA HATARI SANA
 
Kuna mwingine nilishangaa hajuwi hata majiji tuliyonayo hapa Tanzania, akasema eti morogoro ni Jiji, Yupo siriasi kabisa redioni kusema kuwa morogoro Ni jiji, waandishi wa siku hizi Ni wajuaji Sana na hawafanyi utafiti wa yale wanayozungumza ,pia nahisi hata hawajiandai kabla ya kuingia ofisini ndio sababu unakuta wanajiropokea tu na kufanya upotoshaji mkubwa Sana bila kujuwa kuwa wanasikilizwa na watu wengi Hadi watoto wa shule ambao wanaweza wakakalili uongo kisa tu wamesikia Redioni,

Nakala kwa: Pascal Mayalla
 
Walipokaji wanaajiriwa wwnyw taaluma hawaajiliwi juma lokole sio wa kunitangazia mm
 
Wanaendana na soko.

Vijana wanawaelewa sana...kijana ukimuwekea Godwin Gondwe anasinzia...ila muwekee mwijaku apo au babalevo uone atakavyokaa attention.

Na ukiangalia wengi mnaowalalamikia humu age ni 50+
Kwahyo kubalini tu muda umewapita. Hamuwezi kupata mlichokuwa mnakipata miaka 20 iliyopita....Times change
 
Afadhali wewe umeliona na kilianzishia mada ili tujadili...

Ni kweli kabisa. Kwa mfano pale ITV pana watangazaji fulani wawili mmoja anaitwa JUMA KAPALATU mwingine nimemsahau jina...

Lakini hawa ndio mara kwa mara huongoza kipindi kile cha kila Alhamisi kuanzia saa 3 - 5 usiku kinachoenda kwa jina la "MALUMBANO YA HOJA"..

Hawa jamaa hawana professionalism kabisa ya kuongoza na kusimamia mijadala huru...

Kwa wanaoweza kufuatilia, wafanye hivyo kesho tarehe 10/11/2022 Alhamisi watagundua makosa mengi sana ya watangazaji kiasi cha kuondoa radha ya kipindi na mjadala wote kwa ujumla...

Ni waongo na kilicho kibaya zaidi wao wenyewe kama waendesha mjadala huwa hawana taarifa za kutosha juu ya "issues" wanazoziibua ili watu wajadili...

Hili ni tatizo la waandishi na watangazaji wengi kwa zaidi ya 70%...

Tena ukienda kwenye Online Media/TV huko ndo kuna uchafu mtupu wa wanaojiita waandishi/watangaji...

Kuna watangazaji huko ambao kama ulivyosema kule kusoma taarifa kwa ufasaha tena kwa lugha yao ya kiswahili ni shida...

Mtangazaji anasoma taarifa huku anakata kata kama vile redio iliyo na betri zilizoisha nguvu yake ya kuiendesha...!
 
What exactly do you mean..?

Je, una maana kwa kuwa hawa ni 50+ kiumri, waangalie utumbo ufanywao na vijana hawa bila kuwakosoa na kuwarekebisha kwa kuwaambia kuwa ",things don't go that way...?"

Au, Je, una maana kwa kuwa wewe ni kijana na unashindwa hata kusoma "a small piece of news" ulichoandaliwa kwa kiswahili au kiingereza fasaha uachwe tu kwa sbb wazee hawa hawawezi kupata vya miaka ile...?

This is absolutely ridiculous comments from (may be) a hopeless young man...!!
 
Kupungua watu kutazama TV kusikiza radio na kusoma magazeti kunachangiwa na kukua kwa kasi matumizi ya internet taarifa watu wazipata mapema sana na hazijachujwa hili ni jambo la kawaida globally na TZ
 
Upuuzi uko kwenye fani ya habari kwa ujumla. Mfano audience ya Kenya inakubali makanjanja kama sisi?

Fananisha ushiriki wa wa Tz na wakenya kwenye Twitter na social media nyingine uone tofauti. Tatizo ni kubwa na linahusu hadhira na jamii kwa ujumla.
 
Kweli kabisa. Kiswahili kinachotumika pia ni kibovu.
Mfano:
1. Napendaga kula mihogo.
2. Alikwendaga Ujerumani kusoma
 
Both are correct.
Ni sawa na kwenye mziki mnavyolalamikaga mziki wa sikuizi this and that.
Free advice for you;
Fanyeni kuwa mnasikiliza miziki yenu ya zamani tu muache kusikiliza ya sasaivi.
Kwenye news, angalieni zile recorded za miaka 20 iliyopita youtube.
Au muende hospitali kutibiwa kwasababu Nostalgia is one hell of a disease.

Because frankly speaking, hata mlalamikeje hamuwezi kubadilisha kitu.
Law of demand and supply, ukiona kitu kipo supplied kwa wingi basi ujue demand ndio inataka hiko kitu.
And it's a free market.
Maybe anzisheni stesheni yenu ya wazee afu muone how that'll go.
Muda ni ukuta, Huwezi kupambana nao.
 
Aisee wapuuzi San wakat mwingine mm nasima radio siwez kuja kumsikiliza Bab level ,zembwela ,mpoki ,doki , yaani Ni balaa siwezi kuwasikilizaa hao watu Bora Nile rege tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…