Watangazaji wa kizazi hiki wanakera mpaka basi. Hivi wanaokotwa wapi hawa viumbe?

Cool down kijana; kumbuka hakuna kijiji kisichokuwa na wazee. Heshaima kwa wazee ni kitu bora. Hatuwezi kuona jamii inakengeuka na kuharibika tukakaa kimya. Kwa mfano, zamani hakukuwa na vitendo vya ushoga na usagaji lakini sasa hivi haya mambo yanafanyika hadharani. Tukiuliza kwanini haya mambo yanakuwa hivi mnasema wazee hatuendi na wakati. Hili sawa?

Tatizo wazee tukikemea upumbavu huu mnaona tunawaingilia mambo yenu. Kumbuka ujinga unaotangazwa na watangazaji hawa unaathiri jamii nzima; mwisho wa siku hata mtoto wako au ndugu yako ataiga mambo ya kishoga halafu utaanza kumtafuta mchawi wakati mchawi ni wewe mwenyewe unayeshabikia ukengeufu.

Tukirejea kwenye muziki ndio mnaimba upumbavu kabisa. Wanamuziki wa zamani waliimba nyimbo za mapenzi ambazo baba unaweza kusikiliza na familia yako bila wasiwasi. Siku hizi vijana wanaimba nyimbo za NGONO ambazo zikiimbwa inabidi baba na mama waondoke kwa kuwa zimejaa matusi makubwa. Hata video za muziki zinazotolewa na vijana wa siku hizi hazina maadili hata kidogo......watu wanacheza wakiwa uchi eti mnatuambia huu ndio usasa! Mmerogwa nyie sio bure.

Huwa napata taabu sana wakati ninaposafiri kwenye basi la abiria hizi nyimbo na video zinachezwa tangu mwanzo hadi mwisho wa safari. Mtu huwezi hata kusafiri na mkweo au watoto wako kwenye basi moja kwa kuwa video na nyimbo zinazoimbwa mle zimejaa matusi yenye mwelekeo wa ngono. Inasikitisha sana.

Leo nimesikitika kuna wanaume wawili wanatangaza kule Wasafi FM kwenye kipindi cha mipasho wanaongea mambo ya kimbeya kama wanawake mashangingi. Nadhani hawa wanapaswa kupimwa tuone kama kweli ni wanaume au la. Mwanaume mzima utaongeaje mambo ya umbeya na mipasho kama mwanamke? So sad!
 
Aisee wapuuzi San wakat mwingine mm nasima radio siwez kuja kumsikiliza Bab level ,zembwela ,mpoki ,doki , yaani Ni balaa siwezi kuwasikilizaa hao watu Bora Nile rege tu
Kuna wanaume wawili kule Wasafi FM wanaitwa Idriss Kitaa na Juma Lokole wanaongea umbeya kama wanaume aisee! Leo wakati nafanya utafiti wangu nime-tune Wasafi FM nimeshangaa sana jinsi wanavyoongea kishoga. Hawa wanapaswa kupimwa ili tuwatambue kama ni wanaume au la. Isije ikawa sensa inaonesha wanaume ni wengi kumbe wapo wachache. Ni shida aisee!
 
Wanaume wa dar hao
 
Sasa ulitegemea nin unakuta mtot wa kiume anaandika sms""kaandika xmx,,,,xio,xaxaivi,,,,,,,yaani unakaa unawaza unasema huyu kapote au
 
Kweli kabisa. Kiswahili kinachotumika pia ni kibovu.
Mfano:
1. Napendaga kula mihogo.
2. Alikwendaga Ujerumani kusoma
Au utasikia mtangazaji anatangaza kwa kujiamini anatamka upumbavu ufuatao:
1. Zimekasoro dakika mbili ifike saa 3.
2. Nitaendesha kipindi kwa muda wa masaa mawili.
3. Sintokubali kuondoka bila kukuchezea muziki.
4. Yamebaki mawiki kadhaa kuelekea kombe la Dunia.
5. Ni budi kufikiri kabla ya kuongea.
6. Leo nimeokota funguo ya gari iliyopotozwa na dereva wa gari iliyokuwa imebeba kontena mbili.
7. Nimemnunulia mwanangu daftari tatu.

Yaani fani ya utangazaji kwa sasa hivi imevamiwa na kenge kutoka kila kona; wanajiropokea tu kama walevi, mateja au wehu. Inasikitisha mno. Bila serikali kuingilia kati, muda mfupi ujao tutakuwa na kizazi cha ovyo sana.
 
Sasa ulitegemea nin unakuta mtot wa kiume anaandika sms""kaandika xmx,,,,xio,xaxaivi,,,,,,,yaani unakaa unawaza unasema huyu kapote au
Nawaza ifikapo 2050 nchi hii itakuwa imejaa mateja, mashoga, wasagaji na wehu tupu. Serikali inapaswa iingilie kati.
 
Ndio maana kule BBC Swahili kuna wakenya wengi kuliko watanzania kwa sababu watanzania hawako makini, mbali na ukweli kwamba tanzania ndiko Kiswahili kilikozaliwa.
 
Watangazaji makanjanja wanapomhoji mtu, hasa mwanasiasa, huwa wanamuacha atiririke tu bila kuhoji wala kuomba ufafanuzi wa majibu. Katika mahojiano na mwandishi wa habari, mtu anayehojiwa anaweza kuulizwa swali linalohusu nutrition akatoa majibu ya astronomy lakini mtangazaji akabaki amemtumbulia macho tu bila kumuongoza. Ovyo sana.

Hivi ndugu zetu waandishi akina Pascal Mayalla ndivyo mnavyofundishwa huko SJMC au mnaamua tu kutuburuza kwa makusudi? 😀 😀 😀
 
Masikini, inasikitisha sana! Huyu mpuuzi aliwapotosha wanafunzi waliokuwa wakimsikiliza maana wanafunzi wanaamini kuwa watangazaji wanaongea ukweli daima. So sad!
 
Asante sana mkuu. Naomba huo uzi wa Pascal Mayalla ukiupata unitag, sikuwahi kuusoma. Najua atakuwa amedadavua vizuri hii mada.
 
Nawaza ifikapo 2050 nchi hii itakuwa imejaa mateja, mashoga, wasagaji na wehu tupu. Serikali inapaswa iingilie kati.
Unajua ujinga wa ushoga unaanza na vitu vidogo vidogo mtoto wakiume unafanya vitu vyakike kike mwisho was siku unashindwa kujitofautisha wew na wanawake unaanza kufanya usodoma
 
Na wahariri ama waliowaajiri nao unaweka kundi gani?
 
Nadhani mngejua kutofautisha kwenye ukemeaji wenu kati ya maudhui na mtindo wa ufikishaji wa sanaa.
Mnapokemea maudhui kama ushoga, ngono,ulevi,umbea, uongo, uzembe katika uwasilishwaji wa sanaa kama habari, muziki, nk. Hapo ni sawa.

Lakini sasa mnapoenda mbali/kuchanganya na kuanza kukemea mtindo wa sanaa inavyowasilishwa kama matumizi ya Lugha, mandhari, mahadhi, nk. Hapo mnakosea.
Mtindo huwa unabadilika kuendana na muda.

Mfano kwenye lugha hapo, mngetakiwa kutambua sifa ya Lugha mojawapo ni kukua, lugha sio gereza kwamba lazima ujifunge kwenye kanuni na sheria za kisarufi, misamiati nk. Zilizowekwa na wataalamu kule maofisini. Kumbuka sanaa ni kioo cha jamii. Sasa kama jamii inaongea "kwendaga" basi haina budi sanaa iakisi lugha inayotumiwa na jamii.
Hata kiingereza cha leo hakikuwa hivyo miaka 500 iliyopita. Wangeng'ang'ania na wao kisibadilike ingekuwaje?
Hata lugha za matusi pia ni mojawapo wa mtindo wa ufikishwaji wa sanaa. Haya matusi yana maana na yangekuwa mabaya sana basi jamii isingeyatunga na kuyaweka kwenye kamusi.

Mfano mwingine kwenye mziki, kuna watu wanalalamika mtindo wa kisasa wa mziki haufai, unakuta mtu kama Scars anapinga mziki wa leo kwasababu mabiti ni ya Trap, yeye anataka mabiti yaleyale ya bum bap ya miaka ya 90 mpaka leo watu waimbie.
Au unakuta mzee analalamika kuwa sikuizi mnaiga wanaijeria hamna uhalisi wa kitanzania. Well, No shit Sherlock..Have you ever heard the term 'globalization'?
 
Ni sawa wangeongea tu basi kiswahili. Shida wanajifanya na kiingereza wanajua ila kila wanalochomekea wanakosea!!!! Past tense, noun, verb, adverb havibadiliki hata miaka 500!!! Lugha za watu zina misingi yake mkuu kama huwezi hata basics ni kuachana nazo tu!!!
 
Mkuu nakuelewa sana unaposema kwamba lugha yoyote hukua. Lakini sikubaliani nawe unapotetea kwamba lugha sanifu ambayo tayari ipo kwenye matumizi iharibiwe eti huko ndiko kukua kwa lugha. Big NO!

Kukua kwa lugha huhusisha kuongeza misamiati mipya sio kupindisha misamiati ambayo tayari ipo na inaeleweka kwa wazungumzaji wa lugha husika. Kwa mfano huwezi kutetea kwamba mtu akitamka "kwendaga" badala ya "kwenda" au "sintokubali" badala ya sitakuballi". Hii haimaanishi kukuwa kwa lugha bali huo ni upotoshaji wa lugha unaopaswa kukemewa kwa nguvu zote.
 
Again, inategemeana na hadhira. Kama hadhira ni waingereza wanaojali past tense, verb noun hapo atakuwa anakosea.
ila kama hadhira ni watu kama mwajuma wa mwabepande ambaye yeye kila siku anasema 'ofkozi mimi ni beuty' na jamii husika ndio inaelewa hivyo. Basi hata watangazaji wakisema hivyo sioni shida.

Kumbukeni jamani hizi lugha ni nothing but tools tu za kufikisha ujumbe.
Lugha zipo kwa ajili ya watumiaji na sio vice versa.

Kama wewe ukitumia kiswahili sanifu/fasaha kwa misamiati migumu na kuifanya majority ya jamii isikuelewe na mwingine akatumia kiswahili hiki kinachoongewa mtaani chenye mbwembwe na vikolombwezo 'shazi' halafu watu wakamuelewa. Aliyefikisha ujumbe zaidi ni yupi?

Angalieni kwanza hadhira inayokusudiwa ni ipi. Kama hadhira ni ya kimataifa kama BBC, basi wakifanya hivyo wanakosea.
Lakini kama kipindi husika kinaitwa XXL kwaajili ya vijana wa mtaani wanaondika sasa 'Xaxa'..inabidi mtindo uendane na vijana walengwa.
 
Mwijaku naye mtangazaji
Juma Lokole naye mtangazaji
Baba Levo
Orodha ni ndefu.

Hali ni shaghalabaghala
Kwakweli. Halafu kariba watangazaji wote kuna kamsemo kao wanakapenda. Utasika "Ee bana eeh" kila mtangazaji akianza kutangaza lazima aanze na neno "Ee bana eeh". Sijui ndio wanafundishwaga huko vyuoni kwao, au wanaigana. Sikapendi hako kamsemo basi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…