Watangazaji wa kizazi hiki wanakera mpaka basi. Hivi wanaokotwa wapi hawa viumbe?

Hapana mzee uli catch vibaya kusudio langu

Katika mziki kwanza huwa nafurahishwa na mambo makuu mawili ambayo ni ubunifu na content. Beat kwangu sio kipaumbele thats why hata kwenye ngoma za Joyner Lucas nilizozikubali zilizingatia contents.

Wakina Young Lunya wanapita kwenye trap beats lakini ukiangalia katika jicho la kisanaa utaona kuna makosa mengi ukiachana na contents lakini pia hata vina utaona havipo au ni vile vya magumashi

Vina vya magumashi mfano wake ni kama ile Dear God ya Kalla Jeremiah, mle hamna vina ila kwa wasiojua mziki hawawezi kuelewa. Na ndio maana nilipenda kuona hawa wagawaji tuzo wawe ni watu wanaojua mziki na sio kutoa tuzo kwaababu ya trend.

Kama wanataka kutuweka kwenye mfumo huo basi wazitafutie kipengele chao ili tuwe tunawaelewa kuliko kusema wimbo bora wakati lyrically ni zero

Ubunifu bongo umepungua au umeisha kabisa, hususani kwenye Bongo Fleva

Mfano leo hii katika kizazi cha Bongo Fleva tunao wasanii wakubwa kina Diamond nk. Hawa wasanii to be honestly they lack some creativity wameanza kufanya remake kwenye nyimbo za zamani

Na hata wakifanya nyimbo mpya walizotunga wao bado utaona wana pwaya kwenye content though wanabebwa na fame plus fan base waliyo nayo na ndio maana hata wakitoa nyimbo ya dakika 3 afu humo wawe wanajikoholesha tu bado ita trend tu.

Sasa hiyo inatengeneza mwendelezo mbovu kwa hawa chipukizi ambao wanataka kufikia malengo makubwa kupitia mziki.

Kwasababu watakuwa wanajenga dhana kichwani kuwa ili uweze kufikia level za juu za kimafanikio basi unapaswa kuimba style kama ile ile wanayoimba hawa wakubwa.
 
Mkuu, tuanze na general meaning ya kitu kuharibiwa.
Kitu tunasema kimeharibika kama pale ambapo kimeshindwa kufanya lile dhumuni la uwepo wake. Yani kama mkanda haukazi tena suruali kiunoni basi hapo tunasema mkanda umeharibika.

Lugha huharibiwa pale inaposhindwa kufanya kazi yake ambayo ni kufikisha ujumbe.
Sasa kama mtu ametumia neno 'Kwendaga' halafu watu wasimuelewe hapo ameharibu lugha. ila kama hadhira imeelewa basi hajaharibu lugha, ameikuza.
Kwani neno 'kwenda' lina kitu gani special zaidi ya 'kwendaga'?

Tena by the way, kwendaga ni bora kuliko kwenda kwasababu linaonesha mazoea. Kuliko kusema 'huwa unaenda' mtu anasema 'unaendaga' so hapo tayari amefupisha maneno na ameongeza efficiency ya lugha.
Lugha hukua kwa style nyingi tofauti tofauti, sio lazima ikue kwa style unayotaka wewe ya kuongeza misamiati migeni kabisa kwenye kamusi.
Inaweza kukua pia kupitia kubadili misamiati iliyopo.

Ngoja nikupe mfano kwenye kimalkia.
Kulikuwa na neno Awe:-likimaanisha mshangao (wonder) au hofu juu ya kitu kikubwa chenye nguvu sana kama Mungu, mfalme nk.
Sentesi: After realizing what God had done to save my wife, I was in awe.

Sasa kile kitu kinacholeta hisia za Awe kilikuwa kinaitwa Awful..yani kitu kinachomfanya mtu ashangae ukuu wake (Awful:-Full of awe)
Sentesi: God is awful.

Lakini muda ulivyoenda watu wakaanza kulibadilisha hilo awful badala ya full wakaanza kuweka some, wakazaa neno 'awesome' lenye hiyohiyo maana....na walipofanya hivyo wakabadili matumizi ya hili neno awful mpaka sasa limekuwa kinyume chake kabisa.
Sasaivi ukisema Awful unamaanisha kitu kibaya, kisichofurahisha, kisichopendeza.

Sasa hapo huoni msamiati ambao tayari ulikuwa unaeleweka umebadilishwa muundo na maana na kuzaa misamiati mipya?
 
Unamfahamu mtu anaitwa Tundu Lissu, makamu mwenyekiti wa CHADEMA ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni Ubelgiji...?

Huyu jamaa waandishi wa habari na watangazaji wengi makanjanja humgwaya kumfanyia mahojiano kwa sababu mwandishi au mtangazaji habari husika asipokuwa makini yeye ndiye anaweza kugeuzwa kuwa mhojiwa badala ya mtangazaji au mwandishi wa habari kwa kumfundishwa mtangazaji au mwandishi wa habari yampasayo kufanya kama mwandishi/mtangazaji...!

Na wakati mwingine haoni haya kumwambia, "wewe unajua unachokifanya kweli hapa..?"

Sasa mwandishi/mtangazaji ikifikia hatua ya mhojiwa wako anakuambia hivi mbele ya TV Cameras, uelewe kabisa wewe mwandishi au mtangazaji umekosa weledi....you are a complete failure...!!
 
Uko sawa kabisa
 
Mkuu kila nikijaribu kukuelewa nashindwa. Kama ni hivi basi hakuna haja ya kuwa na fasihi ya lugha. Kwa maoni yako, kila kitu kitakachosemwa au kuandikwa kipo sahihi. Hebu angalia mifano ifuatayo labda utanielewa. Sasa itabidi nirudi darasani. Hapa naandika maneno ambayo watangazaji hupotosha lakini wewe unawatetea unasema eti wanakuza lugha:
Neno sahihi Neno wanalotamka watangazaji makanjanjaMfano katika matumizi yasiyo sahihi
SaaMasaa/LisaaNimekaa hapa kwa masaa matatu/Nitakuja baada ya lisaa limoja
MadhumuniDhumuniDhumuni la barua hii ni kukualika mkutano
Sina budiNi budiNi budi kila mtu kujali afya yake
MakontenaKontenaGari imebeba kontena tano.
WimboNyimboNyimbo hii ni nzuri sana
MadaftariDaftariDaftrari zako ziko wapi?
JumaLijumaNitakuwa nje ya ofisi kwa muda wa lijuma limoja
Ndugu yangu hivi upotoshaji wa lugha kama huu utasema ni kukua kwa lugha kweli? Upo serious kabisa au unachokoza mada tu?
 
Pascal Mayalla tuambie taaluma yenu imekumbwa na nini?
 
Hao ni ma prizenta.
 
Niliacha kusikiliza redio punde tuu nilipogundua wimbo mmoja unaitwa 'nyimbo moja'..
 
Niliacha kusikiliza redio punde tuu nilipogundua wimbo mmoja unaitwa 'nyimbo moja'..
Halafu wanaotamka hivi wanajionaje wajanja? Wanajiona kama wako juu ya dunia. πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
 
Mkuu hili jambo nimelifanyia utafiti kwa kusikiliza redio na TV mabalimbali na kwa kuwahoji wasikilizaji. Ni kweli wengi wamechelea kufuatilia taarifa za redio na TV za jamii kwa sababu ya upotoshaji na utangazaji wa ovyo.
Exactly
 
Na wewe nawe ni kama vile hujui vizuri Kiswahili. Yaani unabaki kudokoa dokoa vijimaneno ya Kiingereza alimradi tu uonekane unajua Kiingereza. Unakera kweli kweli na huo ulimbukeni wako.
 
Na wewe nawe ni kama vile hujui vizuri Kiswahili. Yaani unabaki kudokoa dokoa vijimaneno ya Kiingereza alimradi tu uonekane unajua Kiingereza. Unakera kweli kweli na huo ulimbukeni wako.
Kwahio kujua Kiswahili ni moja ya requierments za kujiunga JF ?

Ukitaka definition ya Ulimbukeni ni hicho ulichoweka hapo juu.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…