Watangazaji waliokuwa wanamuhoji Ruto, Tanzania hatutowapata wa kiwango kile daima

Watangazaji waliokuwa wanamuhoji Ruto, Tanzania hatutowapata wa kiwango kile daima

Wakina nani mfano?
Mkuu hata hao waKenya wakija Tanzania hawawezi kufunguka hivyo, pale wanafunguka kwa sababu wanajua wanalindwa na wananchi na sheria.
Hapa kwetu hio kitu hamna, sikatai hakuna serikali yenye kutoa uhuru wa kuongea 100%, lakini Kenya kwenye suala la uhuru wa vyombo vya habari wametupiga miaka 100, na hilo halikutokea tu walipambania.
 
Kenya kuna Uhuru wa habari wa kutosha Sana, tujifunze huko.

Huku kwetu nadhani hatujafikia hatua hiyo bado tuko kwenye homa ya ujamaa unaweza mtangazaji ukataka kutumia akili yako vyema wamiliki wa chombo wakaona unawatafutia matatizo.
Bora ujadili mpira na udaku havina madhara Sana.
 
Mchimba Chumvi ukifatilia mahoji fulani hivi... Ni kiongozi mkubwa hapa serikali akaulizwa

""Mheshimiwa unawashauri nini vijana wanaopenda mashangingi""""

Sasa assume hawa ndo watangazaji wetu
Aisee ni media za bongo zinatia kinyaa.
Mtu kwenye interview anaongea peke yake mara serikali imefanya hiki mara kile bila evidence na mwandishi wala hashughuliki kudadisi,wezetu Kenya huko wametoka zamani sana
 
Mwandishi mmoja wa habari wa Kenya ni sawa na waandishi wa habari wa tano wa Tanzania tena walevi.

Mwandishi wa habari maarufu wa CNN kutoka Kenya Larry Madowo alipata hadi nafasi ya kumhoji bilionea wa Afrika Aliko Dangote.

Waandishi wa habari wa Tanzania kutwa kucha kusifia ccm na kuendekeza uchawa.!!

Uafrika hasa utanzania ni laana.
NI LAANA FOR SURE.
 
Uko sahihi,sekta ya habari hatuna waandishi wenye uwezo mzuri wa kuuliza maswali, binafsi nilichokigundua wengi wao hawapendi kujifunza hata kwa kuangalia wengine wanafanyaje,pia kufanya utafiti kwa jambo analotaka kuuliza na kuwa na data za kutosha kulinda hoja/swali lake.

Shida nyingine ipo kwenye waandishi wa michezo hasa wanapowahoji makocha au wachezaji wa kigeni, unaweza kupata kichefuchefu, waandishi wa michezo ni simple Zaidi kwasababu unaweza kujifunza hata you tube tu,kuna interviews kibao...........


NB: Ukiwa mwandishi kila siku lazima ujifunze na uwe mdadisi kujua vitu vipya
 
Back
Top Bottom