“Watanionaje” neno hili linaweza kukufanya ukaishi maisha magumu sana

“Watanionaje” neno hili linaweza kukufanya ukaishi maisha magumu sana

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Watu wengi hasa wasiokuwa na ajira wameshindwa kutoka ndani na kujaribu kufanya baadhi ya shughuli za kujiingizia kipato kwa kuwaza kuwa “watamuonaje”

Ukijaribu kuangalia kuna vitu vingi vya kufanya kwa waliohitimu vyuo mbalimbali huku mkiendelea kusubiri ajira.

Vitu hivyo ni kama
Kushona,Kusuka,kupika,kupamba,kuuza Juice na vitu vingine kama hivo.

Lakini watanionaje linawafanya wajifungie ndani na kuwa wanyonge huku wakiendelea kusubiri serikali iwasaidie.

ukweli ni kwamba hakuna anayekuangalia kila mtu yuko busy na mambo yake.

Amka na uanze kujituma sasa.
 
Kabisa
Sijui huwa ni aibu kuwa watanionaje me na degree yangu, au sijui huwa ni ulimbukeni/uvivu.

Ukielewa
The Art of Not Giving A F*ck
hautasumbuka kuwaza watanionaje...

Wanetu wa degree amkeni bebeni zege,sukuma toroli la machungwa, fanya 1,2,3 huku ukisikilizia dili litiki kama msemavyo...
 
Kuna degree nyingi sana katika taifa hili, lakini bahati mbaya bado ujinga na umaskini ndio umeongezeka, kiasi cha kusema elimu haijawa msaada kwa taifa licha ya kutumia gharama kubwa za vifaa majengo na muda.

Kuna namna mwenye degree na alie ishia la saba hamna tofauti katika mtazamo na uchanganuzi wa mambo na tena ukiwasikiliza kwa makini alie ishia la saba ana hoja kuliko mwenye degree.

Ni katika muktadha huo wameendela kubaki katika umaskini na ujinga na uhitaji licha ya kuwa na degree, kiasi cha kutosha kuuliza nini haswa faida ya degree?
 
Nyie ndo mnaopelekea wadada kujiuza mtaani ilimradi tu mkono uende kinywani kwa slogan uchwara zenu.

Mtu alomaliza degree kwenda kuuza juisi mtaani sijui kushona ni akili za darasa la saba sio Bachelor, haiwezekani mtu umesota miaka 14+ shule af umalize ukauze juisi au karanga mtaani. Ni rahisi sana kutamka but coming to think of it ni utopolo mtupu.
 
Back
Top Bottom