Fo shua nini mzee mnalishana matango pori, hakuna aliesema kufanya kazi ndogo ndogo ni ufahari kwa mwenye degree, hoja iliokuepo ni neno "Watanionaje" unashindwa kupita njia zako unazoamini eti unawaza watanionaje.
Simple example labda uelewe.
Degree umekosa ajira, limekujia wazo la biashara, let's say umepata wazo la kuuza Viatu, but huna mtaji.
Lakini akili inakwambia kabisa nikitengeneza unguli(competence) kwenye Viatu watu wataniamini itakuwa rahisi kuwaomba mtaji.
Lakini circle yako huna wafanyabiashara wa viatu, logic inakuja kichwani, acha nitafute machinga anifundishe kupoint nijikaze for 3Months ili niweze jua jozi za Viatu ambazo nipendwa, namba zenye wateja, brand pendwa na n.k
Akili inakwambia this will either change your life forever au kukupa ujuzi wa biashara lakini unashindwa chukuwa action kwa kuwaza "WATANIONAJE", hili ndio jambo la kipuuzi ambalo mtoa maada analipinga