“Watanionaje” neno hili linaweza kukufanya ukaishi maisha magumu sana

Yan afisa masoko wa jiji ajipatie experience kupitia kuuza karanga mtaani, come on man.!!
Kuuza karanga ni mfano tu, usidharau biashara ya aina yoyote kisa eti una digrii. Kama fikra zako zitakuelekeza uko utaishia kulalama kuwa hakuna ajira wakati fursa ziko nyingi ila umebaki watanionaje. Macho yako hayaoni fursa yoyote bali yanaishia kuona macho ya wengine yanavyokutazama wewe
 
Mwaka wa 6 sasa nipo kwenye biashara, siandiki apa kujifurahisha
 
Unauza Vizuri Ifanye Kwa Ubora Wa Kidigrii Hiyo Biashara
 
fo shua mkuu hapa tunadanganyana tu motivational speaker ni wengi sana siku izi waambiwe wao waache kushinda tiktok waende beba zege tuone je wanaweza thubutu
Fo shua nini mzee mnalishana matango pori, hakuna aliesema kufanya kazi ndogo ndogo ni ufahari kwa mwenye degree, hoja iliokuepo ni neno "Watanionaje" unashindwa kupita njia zako unazoamini eti unawaza watanionaje.
Simple example labda uelewe.

Degree umekosa ajira, limekujia wazo la biashara, let's say umepata wazo la kuuza Viatu, but huna mtaji.

Lakini akili inakwambia kabisa nikitengeneza unguli(competence) kwenye Viatu watu wataniamini itakuwa rahisi kuwaomba mtaji.

Lakini circle yako huna wafanyabiashara wa viatu, logic inakuja kichwani, acha nitafute machinga anifundishe kupoint nijikaze for 3Months ili niweze jua jozi za Viatu ambazo nipendwa, namba zenye wateja, brand pendwa na n.k

Akili inakwambia this will either change your life forever au kukupa ujuzi wa biashara lakini unashindwa chukuwa action kwa kuwaza "WATANIONAJE", hili ndio jambo la kipuuzi ambalo mtoa maada analipinga
 
Asante sana
 
Umesema kweli,. Lakini hizo juisi na karanga unaweza kuziandaa na kuziuza kisomi zaidi.

Hivi unajua Reginald Mengi alitajirika kwa kuuza maji ya kunywa?
 
Hii isikie kwa jirani tu ila ukweli ubaki hata amani ya moyo hakuna ni afadhali uende mbali na wanapokujua alafu jikaushe kama hujawahi kuingia hata o level alafu pambania kombe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…