Watano waongezewa nguvu za kiume Hospitali ya Benjamini Mkapa

Watano waongezewa nguvu za kiume Hospitali ya Benjamini Mkapa

Figo moja inauzwa kiasi gani?
Kufa na figo mbili napo ni kuchezea fursa
 
MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Kanda ya Benjamini Mkapa (BMH), Prof. Abel Makubi, amesema hadi sasa wamefanikiwa kuweka vipandikizi maalum kwenye uume kwa wanaume watano waliokuwa na changamoto za upungufu wa nguvu za kiume.

Prof. Makubi, amesema hayo jijini Dodoma, wakati alipokuwa akielezea mafanikio na mwelekeo wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema, katika kipindi hicho BMH, imefanikiwa kuweka vipandikizi kwa wanaume watano ambao walikuwa na changamoto za upungufu wa nguvu za kiume, BMH ikiwa ni hospitali ya kwanza kutoa huduma hiyo hapa nchini.

Amesema, watu hao watano tangu wafanyiwe upandikizaji huo wanaendelea vizuri na hakuna changamoto yoyote ambayo wameipata hadi sasa.

“Tumefanya upandikizaji kwa watu hao watano hii ni kutokana na gharama kubwa zilizopo ukilinganisha na mahitaji yaliyopo nchini.

“Utafiti wetu unaonyesha kuwa asilimia 40 hadi 50 ya wanaume wanachangamoto ya upungufu wa nguvu za kiume hivyo kinachofanyika hivi sasa na serikali nikuona namna ambavyo itaweza kugharamia vifaa vinavyotumika kufanya upandikizaji ili kupunguza gharama,”amesema.

Chanzo: Nipashe
 
Kwamba wamepandikizwa uume au wameongezewa homoni zinazochochea nguvu za kiume?
 
Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) imesema kati ya asilimia 40 hadi 50 ya wanaume wanakabiliwa na tatizo la nguvu za kiume, huku wengi wakifika hospitalini hapo kutafuta huduma ya upandikizaji wa uume.

Mkurugenzi Mkuu wa BMH, Prof. Mabere Makubi, akizungumza leo Machi 4, 2025 jijini Dodoma amesema tayari wanaume watano wamefanyiwa upasuaji huo, lakini changamoto kubwa ni gharama zinazofikia Sh milioni 5 hadi 6. Amesema hospitali hiyo inaendelea kushirikiana na serikali ili kupunguza gharama na kufanya huduma hiyo kupatikana kwa wengi.

Aidha, hospitali hiyo inatarajia kuanza kutumia roboti katika upasuaji ndani ya miaka mitatu ijayo ili kuongeza usahihi wa matibabu. Pia, wanawake wenye umri wa miaka 35-50 wamekuwa wakihudumiwa kwa huduma ya upandikizaji wa mimba.

Prof. Makubi amewahimiza wananchi kujiunga na bima ya afya ili kuepuka changamoto za gharama za matibabu na kusisitiza kuwa serikali inaendelea kusaidia wananchi wasio na uwezo.
Hatari sana hii aisee!
 
Screenshot_20250306-124532_Instagram Lite.jpg


Screenshot_20250306-124335_Instagram Lite.jpg
 
Back
Top Bottom