Watano waongezewa nguvu za kiume Hospitali ya Benjamini Mkapa

Figo moja inauzwa kiasi gani?
Kufa na figo mbili napo ni kuchezea fursa
 
MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Kanda ya Benjamini Mkapa (BMH), Prof. Abel Makubi, amesema hadi sasa wamefanikiwa kuweka vipandikizi maalum kwenye uume kwa wanaume watano waliokuwa na changamoto za upungufu wa nguvu za kiume.

Prof. Makubi, amesema hayo jijini Dodoma, wakati alipokuwa akielezea mafanikio na mwelekeo wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema, katika kipindi hicho BMH, imefanikiwa kuweka vipandikizi kwa wanaume watano ambao walikuwa na changamoto za upungufu wa nguvu za kiume, BMH ikiwa ni hospitali ya kwanza kutoa huduma hiyo hapa nchini.

Amesema, watu hao watano tangu wafanyiwe upandikizaji huo wanaendelea vizuri na hakuna changamoto yoyote ambayo wameipata hadi sasa.

β€œTumefanya upandikizaji kwa watu hao watano hii ni kutokana na gharama kubwa zilizopo ukilinganisha na mahitaji yaliyopo nchini.

β€œUtafiti wetu unaonyesha kuwa asilimia 40 hadi 50 ya wanaume wanachangamoto ya upungufu wa nguvu za kiume hivyo kinachofanyika hivi sasa na serikali nikuona namna ambavyo itaweza kugharamia vifaa vinavyotumika kufanya upandikizaji ili kupunguza gharama,”amesema.

Chanzo: Nipashe
 
Kwamba wamepandikizwa uume au wameongezewa homoni zinazochochea nguvu za kiume?
 
Hatari sana hii aisee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…