Kulikuwa na maaskofu pale?
Kulikuwa na mashekhe pale?
Ni kwanini unadhani kumsulubisha Yesu kulikuwa ni kosa?
Asante. Twende taribu mkuu.
Tatizo letu hapa ni dogo sana, nalo ni titles nilizotumia- Mashehe na Maaskofu! Labda tujiulize, Shehe ni nani, na Askofu ni nani? Katika muktadha wa kawaida, hawa ni viongozi wa kidini bila kujali ni dini gani. Tukisogea mbele kidogo ndipo tunapata kujua kuwa Askofu ni Kiongozi wa dini ya Kikristo, na Shehe ni kiongozi wa dini ya Kiislamu.
Tukisogea mbele kidogo, utaona kuwa hata baadhi ya madhehebu ya Kikristo hawatumii hii title ya Askofu na badala yake wanatumia cheo-Mwenyekiti.
Kwa nini nimetumia vyeo hivyo kuwa wao walimsulubisha? Ni kwa kuwa ni wakuu wa Makuhani ambao ni Wakuu wa dini ya Kiyahudi wa madhehebu yote- Mafarisayo na Masadukayo ndio waliomwandalia Yesu mashitaka na kupendekeza adhabu ya kifo kwa kusulubiwa kwa Pilato....
Sio ajabu kuwa hata leo Wakuu wa dini na Maaskofu wakuu wanafanya yaleyale! Wanaketi kwenye mabaraza yao na kwa uwazi, bila aibu, wanajadili namna ya kuhalalisha dhambi kama vile kuhalalisha ndoa za jinsia moja kutambuliwa na kubarikiwa Madhabahuni. Waonaje, kufanya hivyo si kumsulubisha Yesu mara ya pili?
Kuhusu kumsulubisha Yesu kuwa ni kosa au la? Naamini kuwa ilikuwa vyote-Kosa na sio kosa! Ilikuwa ni kosa kwa viongozi wa dini kumsulubisha Yesu-rejea ole ya Yesu kwa Yuda , lakini ilikuwa sio kosa Yesu kusulubiwa maana kwa njia hiyo tulipata ukombozi.
Tujifunze kuwa wafuasi na wanafunzi wa Yesu badala ya kuwa wanafunzi na wafuasi wa dini zetu
Vv