Watanzania 38 waukana uraia wa Tanzania

Watanzania 38 waukana uraia wa Tanzania

Mkuu kila kitu kinawezekana chini ya jua
Wengine wanakula ya kubrashi
Na wengine wameambiwa wasile sana

Watu wanapita kila kukicha na kuingia/kutoka
Hata Mexico wanavuka kutwa
Dunia hii huwa sioni kinachoshindikana
Ni kweli s3hemu ambayo unahisi ni changamoto , kuna waliotangulia na waktatua hiyo changamoto
 
ukiukana kuupata ni kwikwi... sheria hairuhusu labda kama itafanyiwa marekebisho... hivyo ni bora usubiri dual ili uongeze uraia kuliko kuukana sasa ukitegemea kuurejesha pale kutakapo kuja kuwa na dual, maana ni ngumu labda kama sheria itazingatia kuwa rejeshea walio upoteza...
Mimi naishi lakini nishaukana hapa hapa sijivunii kuitwa mtanzania
 
Mimi nilipata mchongo wa kuajiriwa Benki Kuu ya Marekani. The Federal Reserve.

Jamaa waliangalia resume yangu (Tanzania tunaita C.V), wakaipenda.Tena nilikuwa hata sitafuti kazi nilikuwa nafanya kazi sehemu nyingine.

Wakasema wananitaka nifanye nao kazi, wamependa uzoefu wangu na elimu yangu.

Ila, wameona kitu kimoja tu, kwamba nimetokea Tanzania. Lakini nimefanya kazi miaka mingi Marekani

Je, nishachukua uraia wa Marekani?

Nikawaambia bado. Hapo nilikuwa na Green Card tu.

Wakasema samahani sana, tumepemda uzoefu wako sana, elimu yako nzuri, lakini hii kazi ni sensitive sana, ina sharti la kwamba mtu atakayeifanya ni lazima awe raia wa Marekani. Haijalishi kama ana uraia wa nchi nyingine, lakini awe raia wa Marekani.

Yani Tanzania ilikuwa na nafasi ya kuwa na mtu wao Benki Kuu Marekani apate uzoefu, hata aweze kusaidia mambo Tanzania.

Hapo nilikuwa nishasubiri sana dual citizenship kwa uzalendo.

Nikasema sasa basi sisubiri tena.

Ilikuwa nina uwezo wa kupata uraia wa Marekani miaka kadhaa nyuma lakini nilikuwa nangojea dual citizenship Tanzania.

Nikaenda ku apply uraia wa Marekani, nikauchukua.

Kuanzia hapo nikafungua milango ya zile kazi zote sensitive ambazo watu walikuwa wana mind uraia.

Mpaka leo sijajutia uamuzi wangu huo.

Kama Watanzania wameshindwa kujua umuhimu wa watu walio nje, wao ndio wanakosa kitu hapo.

Ilinitokea kama hii ila mimi ilikuwa army na utofauti kwa uzawa sio uraia
Nikakataliwa kwa sababu ya kutokuwa mzaliwa ingawa nina uraia wa wazungu
 
Sensa imeanza mapema hivi.😂😂
#Akili za usiku
 
Shida wabongo watamchomea utambi ipo siku ndo ataelewa bongo nyosso au atageuzwa mteja au chaka pindi maafisa wakijua.
Maana wakiingia tu kwenye data base atapewa 24hrs note aondoke nchini sio raia plus kesi juu ya kujipatia passport ya kitanzania hali si Mtanzania.
Inatakiwa aishi kwa vibali hadi miaka 7 kisha ndo aombe kujadiliwa kuwa Mtanzania, kuanzia ngazi ya mtaa hadi kwa Waziri.
Unachomewaje utambi wapo wengi waliishi hivyo kwa hiyo mtu akiishi Nje miaka mingi watasema sio Mtanzania?
 
Hivi tunaukania wapi maana mm nishachoka bora niukane hapa Tz niombe ukimbizi huko Norway au ujerumani
Hivi ukiukana watakulazisha kulipa kodi na makato mengine? Dr. Nchemba alisema tuhamie Burundi lakini siioni kwenye hiyo list
 
Uingereza washkaji kibao wana british passport na na passport ya Tanzania na wanazitumia zote.

Wahapahapa hawawezi kulijuwa hili, hizi ni siri za jandoni.
Hata Arusha, wengi Sana Wana passport za Kenya na tz
 
Sasa hao waliochukua uraia wa China na India.bora wangeendelea kuwa wabongo tu.
 
So inamaana ugumu wanaouweka kwenye kupata hizi documents ni kutengeneza mazingira ya kujipatia rushwa , na sio usiri wala usalama?????
Swadakta ww ukiona sehemu kugumu unaekewa vikwazo vikwazo penyeza rupia tuu mambo yanakuwa laini maana mtu ndo anachokihitaji.
 
Yeah,

Unaunyaka ule mtaa?

New Yorkers wenyewe wale ukiutamka ule mtaa "Hyuston" huwa wanamind sana.
Yes naunyaka, nimegundua Americans kuna baadhi ya maeneo yao wao wenyewe wanatofautiana kuyatamka kutegemeana na state.
 
Back
Top Bottom