Aisee wangeruhusu uraia pacha ,kisha wange tunga sheria kama wanahisi kutakuwa na mkanganyiko au athari wanazozihofia
Mimi nilipata mchongo wa kuajiriwa Benki Kuu ya Marekani. The Federal Reserve.
Jamaa waliangalia resume yangu (Tanzania tunaita C.V), wakaipenda.Tena nilikuwa hata sitafuti kazi nilikuwa nafanya kazi sehemu nyingine.
Wakasema wananitaka nifanye nao kazi, wamependa uzoefu wangu na elimu yangu.
Ila, wameona kitu kimoja tu, kwamba nimetokea Tanzania. Lakini nimefanya kazi miaka mingi Marekani
Je, nishachukua uraia wa Marekani?
Nikawaambia bado. Hapo nilikuwa na Green Card tu.
Wakasema samahani sana, tumepemda uzoefu wako sana, elimu yako nzuri, lakini hii kazi ni sensitive sana, ina sharti la kwamba mtu atakayeifanya ni lazima awe raia wa Marekani. Haijalishi kama ana uraia wa nchi nyingine, lakini awe raia wa Marekani.
Yani Tanzania ilikuwa na nafasi ya kuwa na mtu wao Benki Kuu Marekani apate uzoefu, hata aweze kusaidia mambo Tanzania.
Hapo nilikuwa nishasubiri sana dual citizenship kwa uzalendo.
Nikasema sasa basi sisubiri tena.
Ilikuwa nina uwezo wa kupata uraia wa Marekani miaka kadhaa nyuma lakini nilikuwa nangojea dual citizenship Tanzania.
Nikaenda ku apply uraia wa Marekani, nikauchukua.
Kuanzia hapo nikafungua milango ya zile kazi zote sensitive ambazo watu walikuwa wana mind uraia.
Mpaka leo sijajutia uamuzi wangu huo.
Kama Watanzania wameshindwa kujua umuhimu wa watu walio nje, wao ndio wanakosa kitu hapo.