Uchaguzi 2020 Watanzania eleweni: Kuanza kampeni kabla ya wakati ni kanuni ndani ya CCM tu; haipo popote katika Sheria za Tanzania, wala katika Kanuni za Uchaguzi

Uchaguzi 2020 Watanzania eleweni: Kuanza kampeni kabla ya wakati ni kanuni ndani ya CCM tu; haipo popote katika Sheria za Tanzania, wala katika Kanuni za Uchaguzi

Habari wana JF,

Naomba niwaelimishe, CCM wana utaratibu wao wa siasa. Ndio walijiwekea kitu kinaitwa, "kuanza kampeni kabla ya wkt" huko kwao.

Hakuna popote hicho kitu ktk sheria za nchi ya Tanzania, wala haipo ktk kanuni za uchaguzi mkuu za nchi yetu.

Sasa kanuni za CCM nani anataka kulazimisha ziwe eti ndio za nchi?!

Hizo ni kanuni za Chama chenu, ndio hizo hizo mlitumia kumkata Lowassa huko mwaka 2015, pamoja na mambo mengine. Hizo ni za CCM, sio za nchi.

CCM ndio huwa mnatuhumiana mambo ya kampeni kabla ya muda.
Acheni kutuharibia nchi kwa kanuni zisizokuwepo.

Nashangaa watu wanashadadia tu.
Membe nae anajisemea eti katafuta wadhamini kimya kimya kuepuka kuvunja kanuni. Zipi?
Yani B. Membe bado anawaza kanuni za CCM kichwani mwake?
Kweli nimeamini ni ngumu sana mtu kusahau asili yake.

Membe, Magufuli na wenzako kajisomeeni tena, hiyo ni sheria yenu kwenye makabrasha ya CCM; haipo ktk sheria za nchi.

Full stop

Tofautisheni nchi na CCM.
Membe ametamka hiyo Kauli kimkakati kabisa kutengenezs mazingira ya Lissu kukdtwa ionekane kavunja sheria , Membe ni walewale chui ndani ya ngozi ya Kondoo be aware.
 
Pamoja na kupiga porojo miaka 5 wakati wenzie wa auguza majeraha huyu "Msema kweli mpenzi wa Mungu" hizi wiki 2 tu za Lissu jukwaani keshaanza kuwika kama kuku anayemashwa na kicheche hehhe
 
Membe ametamka hiyo Kauli kimkakati kabisa kutengenezs mazingira ya Lissu kukdtwa ionekane kavunja sheria , Membe ni walewale chui ndani ya ngozi ya Kondoo be aware.
Membe ana rangi nyingi za kijani.
 
Nyie subirini kuingia uchaguxi bila mgombea urais hamtaki , zege halilali.Mlionywa hamkuonyeka
 
Hakatwi mtu yeyote wa upinzani kwa figisu za CCM/NEC ,wakijaribu ndio utakuwa mwisho wa CCM kabla ya tar 28 OCt maana NTITI wake utakuwa mara 100 na nusu.
Speaking behind the keyboard. Baadaye tukisema tutoke hauonekani [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Speaking behind the keyboard. Baadaye tukisema tutoke hauonekani [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Kwani Tulivyojitokeza JKNIA kumpokea lissu licha ya vitisho vyote hautukuona? Subiri uje kuona SASA BASI either mtangaza matokeo ya haki au TULIE WOTE.
 
Ni kweli aisee, hizo kanuni zilitumika kumpiga marufuku kufanya siasa kwa muda usiojulikana ndugu Lazaro Komba alietaka kumng'oa Jenista Mhagama kule Peramiho.
 
Back
Top Bottom