Watanzania hatujachelewa; tuwekeze kwenye Cryptocurrencies!

Mkuu nakufatilia sana nyuzi zako,unajitahidi sana kuwasanua wabongo kuhusu haya mambo,wabongo wanapenda umbeya kuliko elimu
Leo hii kijana wa chuo,anapenda sana anasa,wakati ana uwezo wa kununua hata Tron 100,akaziweka tu kwa miaka 10
Tunajitahidi tunapo pata nafasi si mbaya kushare tunayo jua. Hata kama si leo basi miaka kadhaa ijayo tunacho share leo kitanufaisha watu!

BTW thanks!
 
Mkuu hold wala usikate tamaa shilingi inaweza kupinduka saa yyte, its a matter of time, tena usiishie kuhold tu fanya na staking zitie fixed ata kila baada ya mwezi utazivuuna saana mkuu

Mkuu naomba nije PM
 
Huu Uzi Kuna muda utafufuliwa na watu watakuwa wanacomment za "ningejua"...


Kuna ule Uzi wa Bitcoin wa 2010, mwamba alianzisha ,ukisoma comment za juu na za chini utagundua kuwa watu walipishana na gari la mshahara...

Watu walikuwa wagumu hivi hivi .....

Jf huwa inatunza kumbukumbu ,2030 huu Uzi utafufuliwa na Kuna watu wataumbuka trust me...

Narudia Tena 2030 huu Uzi utaumbua watu ....
 
Inakuwaje hizo coins zinapanda thamani hivo? Hakuna udaku kweli kwenye hayo mambo? Hizo coins zinazalisha nini hasa mpaka thamani yake inapanda hivyo?

Je wachina ni wajinga kukataa hizo coins na kuzipiga marufuku??
Na Wamerekani, Waingereza, Wajerumani, Wafaransa ni wajinga kuzikubali hizo coin?! Lazima tujifunze kujiuliza maswali yote.
 
Mkuu ebu naomba ushaidi kuwa China imekataa hizi coins, maana hainingii akilin kwa taifa kubwa kama China kukataa hii kitu
Sorry lkn
Nafikiri ungemquote aliyesema china wamezuia ingekuwa sahihi zaidi.
 
Nashauri watu wawekeze kwenye physical things ...bado tuna ardhi ya kutosha, ...
Physical things kutoboa ni shida, case ya 1 kwa kilimo,mvua hazieleweki,soko nalo halieleweki,tozo kibao
Case ya 2 Biashara, Mtaji huna,majungu kibao,tozo kama zote hapo utatoboa tuache siasa wakuu...
 
Unasema dunia ndo inakoelekea na kwamba mwenye degree hapaswi kuuza vitu mtaani? Kwahiyo wakati unasubiri hiyo dunia ifike huko inakoelekea ukae tu na kusubiri sio?

Ndomaana vijana wengi wasomi sikuizi mna maisha magumu tu mitaani, kujishughulisha hamtaki na mnaamini katika easy earnings (mnaishi kwenye ndoto na sio maono). Pamoja na kwamba dunia ndo inaelekea huko bado mnatakiwa mfanye kazi za kueleweka sio kukaa tu matokeo yake mnakuja kuwa vibaka.

Hapo unajinasibu kuwa mwenye degree hawezi kuuza maembe ilhali huna hata 50M benki, aiseeeh😂
 
Kwa wastani ulianzia kiasi gani?
 
Mtu angenunua MATIC tarehe uliyopost...leo angekua na faida ya zaidi ya 90%
 
Binadamu wengi hatuna pesa, sababu si kuwa hatufanyi kazi kwa bidii,...sababu kubwa ni kuwa hatuna taarifa sahihi kuhusu pesa na tukiambiwa/tukipewa taarifa kuhusu pesa tunapuuzia,tukiamini njia tunazotumia sisi tu ndio sahihi(tumekaririshwa)........na hii ndio sababu kubwa wengine ni masikini wa kutupwa wakiendelea tu kulalamika,........umasikini sio pesa,ila ni taarifa sahihi kuhusu pesa
 
Duuh mkuu haya madini acha niyasave...
 
Mkuu tupeane maujanja ya "projects" zitakazolipa hapo mbele...hao wadau tutakuja kuwauzia Shibacoin moja usd 1.2 2031 huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…