Watanzania hatuna shukrani Mungu atusamehe kwa huu ujinga tunaofanya

Sio kweli..hukuwa ukifatilia bunge, Nape aliwahi ongelea suala la mikopo wakati Magufuli yupo, ilipofika trillion 56 akasema serikali iwe makini kwenye kukopa maana muda si mrefu tutakuwa hatukopesheki! Kuwa makini dogo. Chuki isikufanye uwe kipofu, give the man his due..
 
Sasa kwanini alikuwa anajikopea akiwa chumbani kwake..!??

Kwani nchi ilikuwa yake peke yake!??

Acheni kutetea ujinga.
Si angekuwa wazi tuhh!!??
 
Ficha upumbavu wako, au ulishiriki kuzipiga?. Usitetee uovu kwa kulinganisha na hayo yaliyofanyika. Ililazimu afanye ndiyo kazi ya uongozi. Kwani tulimchagua kwenda ikulu kucheza Sindimba au dogoli?.
 
Hapo mtu kaomba tu uchunguzi wa matumizi ya mikopo watu wanakuja na mada kibao zilizo nje ya hoja.

Akija mwingine akaomba uchunguzi wa bei za ndege na utaratibu wa kuzinunua napo zitakuja mada kibao zilizo nje ya hoja.
 
Usilolijua ni kuwa awamu ya 5 wizi ulikuwepo tena mkubwa ila tofauti yake ulikuwa ni wa watu wachache..

Sababu kubwa ni kulikuwa na muzzling of civic space pia hakukua na checks and balances yani dikteta alizitia judiciary na legislature mfukoni .

Wapi Trillion 1.5 alizohoji Prof Assad??

Kwanini tenda kubwa walikua wanapewa Mayanga Constructions?
 
Yote haya umeyaandika kwa kutumia wakati uliopita. Tujadili wakati huu uliopo sasa. Changamoto huenda sambamba na maisha halisi pamoja na utatuzi.
 
Kashfa nyingi ziliibuka wakati wa JK kwa sababu aliruhusu uhuru wa kuongea,Magu hakuruhusu huu uhuru ndio maana unaona wanaanza kuongea sasa hivi.

Believe me,hakuna kipindi wizi umefanyika kama awamu ya Magu,awamu hii inapita awamu zote kwa wizi na ufujaji pesa.

Be a critical thinker you'll understand.
 
Kwa hiyo unamanisha Nape analenga wakuchunguzwa ni Mama na Mpango? Marehemu hahojiki.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…