Watanzania hawana imani na Waziri wa Nishati January Makamba, anapaswa kuachia ngazi, asipoachia Rais amuondoe

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Kila kona manug'uniko ya Watanzania ni juu ya dalili za wizara nyeti ya nishati na umeme kuwa na waziri ambae watu hawana imani nae. Tangu ateuliwe kuwa waziri basi taifa limekuwa na mauzauza tu juu ya upatikanaji wa umeme na hata uongozi na uendeshaji wa Tanesco.

Kitendo cha watanzania kutokuwa na imani na waziri huyu ni sababu tosha kabisa ya kujiuzulu au kuwajibishwa maana ni muda mfupi tu ameprove failure

Mtangukilizi wake Dkt Kalemani alisimamia vizuri Tanesco na kudhibiti ukatikaji hovyo wa umeme, pia aliwahakikishia watanzania kuwa mradi wa kuzalisha umeme wa JNHP utakuwa tayari ifikapo juni 2022.

Lakini tangu ateuliwe January Makamba kuwa waziri mradi wa JNHP umeanza kupata mauzauza, ujazaji maji kwenye mabwawa umechelewa kwa sababu zisizo za msingi, huku kukiwa na harufu ya ufisadi.

Nishati ya umeme ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa letu. Hii wizara haipaswi kuwa na waziri anayetiliwa shaka na umma kuwa mpiga madili.
 
Naona mnaanzisha nyuzi kibao za January Makamba kwa Nchi ya Tanzania yenye msururu wa kodi kwenye bidhaa zetu toka enzi na enzi mnamzungumzia Makamba wa leo.

Kwenye magari huko kuna kodi utadhani Wananchi wanaleta ndege bado wakileta hayo magari yaliyotumika kutoka Japan wanakutana na Ewura kuwapandishia bei kila mwezi...Zambia mafuta yapo bei nafuu kuliko Tanzania nadhani tumerogwa sio bure.
 
Naona mnaanzisha nyuzi kibao za January Makamba kwa Nchi ya Tanzania yenye msururu wa kodi kwenye bidhaa zetu toka enzi na enzi mnamzungumzia Makamba wa leo...kwenye magari huko kuna kodi utadhani Wananchi wanaleta ndege bado wakileta hayo magari yaliyotumika kutoka Japan wanakutana na Ewura kuwapandishia bei kila mwezi...Zambia mafuta yapo bei nafuu kuliko Tanzania nadhani tumerogwa sio bure.
Sahizi ishu ni kuwa fata ofisini huko huko na kuanza kuwatembezea vichapo kama wao walivyowafanya wamachinga!

Ishu ikienda viral pengine masikio yao yatasikia! Tunataka bei za vitu zishuke na usimamizi uwe mzuri! Viongozi wapuuzi waondolewe haraka sio kukumbatia mabomu
 
Hivi watu hawaoni ya kuwa January na uongozi mpya wa Wizara ya Nishati pamoja na TANESCO wapo katika nafasi walizo kuwanazo kwa muda mfupi uliopita! Katika kipindi kama hicho ni lazima tuwe wavumilivu na wapewe muda ili kuweka mambo sawa.

Unapo kabidhiwa uongozi wa wizara kubwa na nyeti kama hiyo ya nishati, ni vyema kiongozi mpya akajifunza kwanza kuhusu mambo ya "efficiency & productivity" ya mfumo alioukuta, nafikiri hiki ni kitu ambacho January amekuwa akikifanya. Pia anapaswa kufanya mabadiliko kwa tahadhari kubwa ili kuleta matokeo lengwa.

January aliukuta mfumo ambao unaendeshwa tu kwa amri tu za kisiasa bila kujali "technical environment" ili watu wapate umeme. Mfumo alioukuta haukujali kabisa kuhusu athari hasi na za muda mrefu kwa mitambo iliyolazimishwa kuendelea na uzalishaji pasipo kuzingatia tahadhari za kitaalamu.

Ni lazima kijana apewe "benefit of doubt" ili apate kutimiza yale aliyoyakusudia kuyafanya na timu yake. Hapo alipo yupo kwenye mipango ya muda mfupi, yaani STP ambayo matokeo ya ni magumu kuyaona. Isipokuwa akiingia katika MTP na hatimaye LTP watu ndipo wanaweza kumpa stahiki yake ya pongezi ama lawama.
 
Unakomaa na mtu mpaka anaku cost political capital yako na focus yako kama Makonda alivyom cost Magu.

Mawaziri karibia 30 mmoja ndio jamii inasema hatoshi, wewe umekomaa nae, kwa nini usisikie kilio na ushauri wa umma kwa ujumla kwamba huyu waziri mmoja hatumtaki ?

January Makamba hakuweza uwaziri chini ya JPM, bosi mfuatiliaji mwelekezi, hatakaa auweze chini ya bosi ambae haijui nchi, bosi clueless, offhanded, tone deaf and out of touch.
 
Hivi watu hawaoni ya kuwa January na uongozi mpya wa Wizara ya Nishati pamoja na TANESCO wapo katika nafasi walizo kuwanazo kwa muda mfupi uliopita! Katika kipindi kama hicho ni lazima tuwe wavumilivu na wapewe muda ili kuweka mambo sawa...
Nyerere alisema mswahili ukitaka akuone wewe Ni mtaalamu Basi ongea maneno ya kiingereza kidogo tu kwny kila baada ya maneno machache,kwahio wewe hapo kuweka maneno Kama efficiency & productivity,technical environment,benefit of doubt,hizo Short/long term plan... Umejiona bonge la expert afu sisi unatuona viaziiiiiiiiiiii.

Duh.
 
Sina uhakika kama huyu bingwa anajua anachofanya na ninaanza kuamini anahusika kutopatikana kwa umeme, atueleze ukweli sio story za magufuli alikataza maintenance au hakuna crane ya kufanyia kazi
 
Hivi watu hawaoni ya kuwa January na uongozi mpya wa Wizara ya Nishati pamoja na TANESCO wapo katika nafasi walizo kuwanazo kwa muda mfupi uliopita! Katika kipindi kama hicho ni lazima tuwe wavumilivu na wapewe muda ili kuweka mambo sawa...
Mh!
 
Nyerere alisema mswahili ukitaka akuone wewe Ni mtaalamu Basi ongea maneno ya kiingereza kidogo tu kwny kila baada ya maneno machache,kwahio wewe hapo kuweka maneno Kama efficiency & productivity,technical environment,benefit of doubt,hizo Short/long term plan... Umejiona bonge la expert afu sisi unatuona viaziiiiiiiiiiii.

Duh.
Huyo jamaa mpambe nuksi anatuona sisi machizi😅!

Watanzania million 1 washamuona yeye hatoshi katika wizara wapambe 10 wanaonunuliwa bia sinza wanataka kuleta utetezi wa kijinga! Wizarani sio sehemu ya majaribio pale...Tunahitaji impact ile ni wizara ambayo ina reflect kipawa cha mtu moja kwa moja kama kilaza utabaki uchi ndani ya muda mfupi tu!
 
Duh hapo kwny uchi umenikumbusha ule usemi wa "ukitaka kuona nyeti za Kuku subiri upepo upulize".

Nadhani sasa upepo ndio unapuliza vzr.
 
Upepo ukivuma nyeti za kuku zinabakia wazi kabisa😅 mfano halisi sasa umeme umekuwa wa shift haumalizi 24 hrs bila kukata
 
Kila kona manug'uniko ya watanzania ni juu ya dalili za wizara nyeti ya nishati na umeme kuwa na waziri ambae watu hawana imani nae. Tangu ateuliwe kuwa waziri basi taifa limekuwa na mauzauza tu juu ya upatikanaji wa umeme na hata uongozi na uendeshaji wa Tanesco...
Samaki anaozaga kuanzia kwa kichwa!
 
Nyerere alisema mswahili ukitaka akuone wewe Ni mtaalamu Basi ongea maneno ya kiingereza kidogo tu kwny kila baada ya maneno machache,kwahio...
Anachokifanya January kujenga mazingira mazuri na ya kitaalamu ili aweze kuiendesha wizara yake. Mkuu, kuhusu matumizi ya maneno ya Kiingereza ndivyo ambavyo mtu yeyote anayetumia lugha yoyote anaweza kufanya ili kutokuweza kupoteza maana aliyoikusudia.

Nenda hata katika hicho Kiingereza ambacho unakisema, kimeazima maneno mengi kutoka katika lugha nyingine hasa Kilatini ili kutopoteza maana lengwa. Maneno kama; ceteris paribus, mutatis mutandis, fait accompli, functus officio, ad hoc, n.k.

Hata Nyerere akiwa kama msomi, katika hotuba zake nyingi ndivyo ambavyo alikuwa akifanya. Pole mkuu, kama nimekuharbia siku kwa kuchanganya maneno, sina njia yoyote ile ya kukusaidia.
 
Iwe booooooooojo.
 
Unakomaa na mtu mpaka anaku cost political capital yako na focus yako kama Makonda alivyom cost Magu.

Mawaziri karibia 30 mmoja ndio jamii inasema hatoshi, wewe umekomaa nae, kwa nini usisikie kilio na ushauri wa umma kwa ujumla kwamba huyu waziri mmoja hatumtaki ?

January Makamba hakuweza uwaziri chini ya Magu, bosi mfuatiliaji na muelekezaji, haiwezekani akauweza chini ya bosi ambae haijui nchi, bosi offhanded, clueless, tone deaf and out of touch.
Haya maoni ya jamii umeyapima kivipi kuwa hayamkubali Januari? Maoni ya JF yaliyofunguliwa na wabaya wake siyo maoni ya wananchi
 
Hivi watu hawaoni ya kuwa January na uongozi mpya wa Wizara ya Nishati pamoja na TANESCO wapo katika nafasi walizo kuwanazo kwa muda mfupi uliopita! Katika kipindi kama hicho ni lazima tuwe wavumilivu na wapewe muda ili kuweka mambo sawa.

Unapo kabidhiwa uongozi wa wizara kubwa na nyeti kama hiyo ya nishati, ni vyema kiongozi mpya akajifunza kwanza kuhusu mambo ya "efficiency & productivity" ya mfumo alioukuta, nafikiri hiki ni kitu ambacho January amekuwa akikifanya. Pia anapaswa kufanya mabadiliko kwa tahadhari kubwa ili kuleta matokeo lengwa.

January aliukuta mfumo ambao unaendeshwa tu kwa amri tu za kisiasa bila kujali "technical environment" ili watu wapate umeme. Mfumo alioukuta haukujali kabisa kuhusu athari hasi na za muda mrefu kwa mitambo iliyolazimishwa kuendelea na uzalishaji pasipo kuzingatia tahadhari za kitaalamu.

Ni lazima kijana apewe "benefit of doubt" ili apate kutimiza yale aliyoyakusudia kuyafanya na timu yake. Hapo alipo yupo kwenye mipango ya muda mfupi, yaani STP ambayo matokeo ya ni magumu kuyaona. Isipokuwa akiingia katika MTP na hatimaye LTP watu ndipo wanaweza kumpa stahiki yake ya pongezi ama lawama.
Nje ya nafasi ya kisiasa wizara ya nishati makambo siyo fani yake. Yaani kwenye nchi hii kisiasa hata mwalimu wa kiswahili anaweza kupewa vifaa vya kumfanyia upasuaji mjamzito na akaua na watu mkasema bado mgeni, anasiku chache n.k. Mnacheza na roho za watu mwambieni mama amefeli pakubwa.
 
Hivi watu hawaoni ya kuwa January na uongozi mpya wa Wizara ya Nishati pamoja na TANESCO wapo katika nafasi walizo kuwanazo kwa muda mfupi uliopita! Katika kipindi kama hicho ni lazima tuwe wavumilivu na wapewe muda ili kuweka mambo sawa.

Unapo kabidhiwa uongozi wa wizara kubwa na nyeti kama hiyo ya nishati, ni vyema kiongozi mpya akajifunza kwanza kuhusu mambo ya "efficiency & productivity" ya mfumo alioukuta, nafikiri hiki ni kitu ambacho January amekuwa akikifanya. Pia anapaswa kufanya mabadiliko kwa tahadhari kubwa ili kuleta matokeo lengwa.

January aliukuta mfumo ambao unaendeshwa tu kwa amri tu za kisiasa bila kujali "technical environment" ili watu wapate umeme. Mfumo alioukuta haukujali kabisa kuhusu athari hasi na za muda mrefu kwa mitambo iliyolazimishwa kuendelea na uzalishaji pasipo kuzingatia tahadhari za kitaalamu.

Ni lazima kijana apewe "benefit of doubt" ili apate kutimiza yale aliyoyakusudia kuyafanya na timu yake. Hapo alipo yupo kwenye mipango ya muda mfupi, yaani STP ambayo matokeo ya ni magumu kuyaona. Isipokuwa akiingia katika MTP na hatimaye LTP watu ndipo wanaweza kumpa stahiki yake ya pongezi ama lawama.
Wewe ni mse*nge hatatoboa kwa ujinga huu wa sgr

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kazi iliyokuwa inamufaa ni hiyo ya kumwandikia JK hotuba na kuuza sura.
Hii wizara haihitaji ujanjaujanja.
 
Back
Top Bottom