Hebu eleza ubaya wa makamba kwa ushahidi concrete sio kwa blah blah
Moja, umeme umeanza kukatika baada ya Makamba kuingia madarakani. Hiyo ni rebuttable presumption kwamba tatizo ni yeye.
Mbili, hajui, hajatulia akaisoma TANESCO, ama hasemi ukweli kuhusu kiini cha matatizo ya TANESCO. Alisema sababu za kukatika kwa umeme ni kukosekana kwa ukarabati wa mitambo, siku tatu baadae tukaambiwa tatizo ni mabadiliko ya tabia nchi. Wiki moja baadae bosi wake akasema tatizo ni ng'ombe za wasukuma na binadamu wakaidi. Wiki moja baadae tukaambiwa tabia nchi imetengemaa, mabwawa yamekaa sawa. Jana Dar es Salaam maji yamekatika kutwa. The leadership is clueless.
Tatu, hajui ama ali underestimate majukumu yake: alisema kama Waziri hataki kupelekewa matatizo ya umeme kwa sababu hataki TANESCO iingiliwe na wanasiasa. Siku hizi anazunguka kwenye mabwawa na karakana za TANESCO.
Nne, anafanya mzaha na teuzi za watendaji. Kamweka Mkurugenzi rafiki yake ambae hana background ya kumwezesha kuendesha taasisi ya kibiashara kubwa kuliko zote nchini. CEO wa Makamba, Chande Maharage, kasema kiini cha tatizo la TANESCO ni wafanyakazi kutolipwa kutokana na utendaji. Toka lini mshahara wa mtumishi wa umma ukabadilika kila mwezi based on performance ?
Tano, ni mzembe, anatupa excuses za hovyo na za kitoto kila wanaposhindwa kusimamia miradi. Makamba kasema Nyerere Hydropower haitakamilika kwa wakati kwa sababu vyuma ni vizito na crane hatuna. Atulie akasome mikataba kwanza, project planning ya contractor inasemaje, walikubaliana watatumia nini kubeba nondo za ujenzi, vichwa vya waponda zege ?
January Makamba does not know which end is up at Ministry of Energy. His boss is just as clueless, and Makamba knows the boss is a lightweight.