Watanzania ni pamoja na wewe mkuu, mimi hata sifuatilii hizo issue za ajali na misiba ya haraiki maana inabaki tu kuwa takwimu tena hasa kwa upande wa serikali. Ndio hizo takwimu hujivunia nazo baadae, utasikia “Hapo awali walikuwa wakifa wakina mama wajawazito kadhaa ila sasa idadi imepungua na kuwa hivi…”
Msiba ukufike nyumbani ndio utajua nini naongea, utajiliza weee japokuwa nchi yako inakuwa haijashusha bendera nusu mlingoti kuomboleza na wewe.
Nadhani watanzania wengi ni wale wa ya kaizari muachie kaizari… wakristo safi kwa waislamu safi ya Mungu humuachia Mungu… nchi ina hao watu wengi kila mahali…