Sio kwamba JK alitumwa na JPM... wakati JPM anaingia madarakani alikuta kila kitu kuhusu SGR kilikuwa tayari.SGR ulikuwa uwe mradi ujengwe na mchina,na jk ndo alienda china kuweka agreement kama sikosei kwa kutumwa na Jpm,
Wachina wakaanzisha harakati za ujenzi,,kisha jpm akaona waturuki ndo wajenge,,akawatoa wachina..
Baadae kama sikosei wachina walifuatwa tena ili watoe funding,,wakagoma
Hata kama watu tunamsema sana Mzee wa Msoga lakini ukweli ni kwamba JK alikuwa very strategic!! Yeye alitaka mradi wa SGR na Bandari ya Bagamoyo viende sambasamba ili hatimae reli na bandari vitegemeane.
Kwavile Mradi wa Bandari unahusisha na Industrial City (mainly for export), basi ilionekana wazi kwamba bidhaa zitakazozalishwa hapo Industrial City, na shehena zitakazopitia Bandari ya Bagamoyo, ni lazima zitengenezewe mazingira ya usafirishaji.
So, JK's SGR First Phase ilikuwa itoke Dar hadi Rwanda, na tawi kutoka Bagamoyo (Bandarini) litakalounganisha reli kuu. Phase ambazo zingefuata ndizo zingeelekea Mwanza ili hatime kuinganisha na Uganda. Kama kumbukumbu zangu zipo sawa, kulikuwa na phase nyingine kuelekea Southern Highland.
Phase ya kwanza ilikuwa igharamiwe na Exim Bank ya China, na walishakubali ku-finance hiyo SGR kwa gharama za USD 7.6 Billion.
That having been said, baada ya JPM kuingia madarakani ilikuwa ni kuanza tu ujenzi kwa sababu kila kitu kilikuwa kimeshakamilika! Hata hivyo, kama inavyofahamika, JPM na watu wake wakasema Mradi wa SGR umejaa ufisadi, na kwahiyo akapiga chini plan ya JK na Mchina wake, akatafuta financier mwingine, na hapo ndipo alipokuja Mturuki!!!
Lakini leo ukiangalia gharama ambazo tayari SGR imeshakula, wakati bado hatujafika kokote kule, trust me, kuna uwezekano mradi ukagharimu zaidi ya USD 7.6 ambazo JPM na watu wake walisema kuna ufisadi!!