Watanzania kabla ya kuanza mradi wa Bandari ya Bagamoyo tafuteni Articles za 'Lesson from Sri Lanka Hambantota Port'

Watanzania kabla ya kuanza mradi wa Bandari ya Bagamoyo tafuteni Articles za 'Lesson from Sri Lanka Hambantota Port'

SGR ulikuwa uwe mradi ujengwe na mchina,na jk ndo alienda china kuweka agreement kama sikosei kwa kutumwa na Jpm,
Wachina wakaanzisha harakati za ujenzi,,kisha jpm akaona waturuki ndo wajenge,,akawatoa wachina..
Baadae kama sikosei wachina walifuatwa tena ili watoe funding,,wakagoma
Sio kwamba JK alitumwa na JPM... wakati JPM anaingia madarakani alikuta kila kitu kuhusu SGR kilikuwa tayari.

Hata kama watu tunamsema sana Mzee wa Msoga lakini ukweli ni kwamba JK alikuwa very strategic!! Yeye alitaka mradi wa SGR na Bandari ya Bagamoyo viende sambasamba ili hatimae reli na bandari vitegemeane.

Kwavile Mradi wa Bandari unahusisha na Industrial City (mainly for export), basi ilionekana wazi kwamba bidhaa zitakazozalishwa hapo Industrial City, na shehena zitakazopitia Bandari ya Bagamoyo, ni lazima zitengenezewe mazingira ya usafirishaji.

So, JK's SGR First Phase ilikuwa itoke Dar hadi Rwanda, na tawi kutoka Bagamoyo (Bandarini) litakalounganisha reli kuu. Phase ambazo zingefuata ndizo zingeelekea Mwanza ili hatime kuinganisha na Uganda. Kama kumbukumbu zangu zipo sawa, kulikuwa na phase nyingine kuelekea Southern Highland.

Phase ya kwanza ilikuwa igharamiwe na Exim Bank ya China, na walishakubali ku-finance hiyo SGR kwa gharama za USD 7.6 Billion.

That having been said, baada ya JPM kuingia madarakani ilikuwa ni kuanza tu ujenzi kwa sababu kila kitu kilikuwa kimeshakamilika! Hata hivyo, kama inavyofahamika, JPM na watu wake wakasema Mradi wa SGR umejaa ufisadi, na kwahiyo akapiga chini plan ya JK na Mchina wake, akatafuta financier mwingine, na hapo ndipo alipokuja Mturuki!!!

Lakini leo ukiangalia gharama ambazo tayari SGR imeshakula, wakati bado hatujafika kokote kule, trust me, kuna uwezekano mradi ukagharimu zaidi ya USD 7.6 ambazo JPM na watu wake walisema kuna ufisadi!!
 
So, JK's SGR First Phase ilikuwa itoke Dar hadi Rwanda, na tawi kutoka Bagamoyo (Bandarini) litakalounganisha reli kuu. Phase ambazo zingefuata ndizo zingeelekea Mwanza ili hatime kuinganisha na Uganda.

Phase ya kwanza ilikuwa igharamiwe na Exim Bank ya China, na walishakubali ku-finance hiyo SGR kwa gharama za USD 7 Billion.

Lakini leo ukiangalia gharama ambazo tayari SGR imeshakula, wakati bado hatujafika kokote kule, trust me, kuna uwezekano mradi ukagharimu zaidi ya USD 7.6 ambazo JPM na watu wake walisema kuna ufisadi!!
Huu mradi hadi Rwanda hauwezi kutumia kiasi
Kidogo kama hicho 7.6bn. Ni gharama kubwa sana zaidi ya hizo.
 
Mkuu kwani huo mkataba Usha upitia utuambia mbivu na mbichi zilizopo ndani?
Kimsingi bandari ya bagamoyo ni kutoa sehemu ya milki ya Tanzania kuwa ni sehemu ya China!! Huu si mkopo bali tunatoa/tunauza sehemu nchi ya Tanzania kwa China kwa bei che ya kutegemea ajira za chini kwa watanzania na kodi kama waki-declare faida baada ya miaka kadhaa!! Maana lazima wapewe tax holiday (likizo ya kulipa kodi wanaporejesha pesa walizowekeza) kwa miaka isiyojulikana! Zito bila aibu anasema "hii si kama nchi ambazo walikopeshwa!" Kwa hiyo waliposhindwa kulipa mradi ukachukuliwa na kuwa mali ya China! Sasa sisi hawasubiri tushindwe kulipa! Tayari tunawapa tangu day 1 na bandari ya bagamoyo kuwa yao! Wakipata hasara ni wao! Wakipata faida ni wao! Eti huo ndio ujanja! Tunatoa sehemu ya milki ya nchi yetu kuwa sehemu ya nchi nyingine! Kisa eti watanzania watapata ajira!

Faida tunayotegemea kupata watanzania inayoshadidiwa ni ajira!! Lakini kusema ukweli siyo ajira bali ni utumwa katika nchi yako mwenyewe! Haipishani na mashamba ya walowezi waliyokuwa wanamiliki wazungu huko Zimbambwe! Wazimbabwe ndio walikuwa wanafanya kazi kwenye hayo mashamba!! Kwa maneno mengine walikuwa wametatuliwa tatizo la ajira!! Ashukuriwe Mungu kwa ajili ya Mugabe aliyekataa utumwa huu (sisi tunaita fursa ya ajira). Mugabe akasema no way!

Hata kama kwa sasa hatuna uwezo wa kuyaendesha mashamba haya kwenye nchi yetu, mbele ya safari watoto wetu, wajukuu wetu, vitukuu vyetu , vilembe vyetu nk watakuja wapate uwezo na kulima mashamba kwenye nchi yetu!! Alikuwa anaangalia mbali!! Magufuli aliangalia mbali! Mbele ya Safari watoto wetu, wajukuu wetu, vitukuu vyetu, watakuja watushangae na kutulaani kwa kuuza nchi yao!! Watakuja kulazimika kuanzisha vita dhidi ya wachina ambayo itaigharimu sana nchi yetu!! Naomba kumbukumbu iwekwe sawa ili historia ije itoe hukumu yake. Majina ya viongozi watakaoruhusu jambo hili yaorodheshwe vizuri na siyo wajifiche kwenye kichaka cha SERIKALI eti "Serikali itafanya mazungumzo na China kuhusu bandari ya bagamoyo".

Hao wanao"wakilisha" serikali wajulikane wazi!! Isiwe kama ile kamati ya corona ambayo hawakubainisha majina yao tangu mwanzo na tukajua jina la mwenyekiti tu. Hata walipopiga picha ya pamoja walivalia kininja ili sura zisionekane eti ni barakoa!! Hawa viongozi wanaotazama leo tu, wanaotaka faida wapate wao tu katika muda wauhai wao bila kujali mustakabali wa watanzania watakaokuja kuishi hapa miaka 1000 ijayo hawatufai!

Kumbukeni scramble for Africa iliyotokea zaidi ya miaka 1000 iliyopita! Wakoloni walivyokuja machifu wetu walikuwa wakipewa shanga, na mavazi na wao wakawatoa watu wao wachukuliwe utumwani!! Watakaokuja kuishi Tanzania miaka 10000 ijayo hawataamini kile ambacho viongozi wetu leo wanataka kukifanya kwa ulaghai wa fursa ya ajira!!
 
Huu mradi hadi Rwanda hauwezi kutumia kiasi
Kidogo kama hicho 7.6bn. Ni gharama kubwa sana zaidi ya hizo.
Lakini unafahamu kwamba hizo 7.6 Billion ni USD?! Na kama bado unadhani ni kidogo, unadhani ni kiwango gani ndicho sahihi?!
 
Well spoken
 
Lakini unafahamu kwamba hizo 7.6 Billion ni USD?! Na kama bado unadhani ni kidogo, unadhani ni kiwango gani ndicho sahihi?!

Ooh, kumbe unaongelea 7.6 bn USD, hapo ni karibu na uhalisia pesa halisi ni double that amount hadi Rwanda.

Kwahiyo Mchina angekuwa na bandari na ku- control miundombinu ya SGR.

Najua unajua kuhusu debt trap, usustainable debt, vitu gani vimewekwa kama rehani (Bond) tusipoweza kulipa.

Kwamba ukishindwa kulipa inabidi ukabidhi assets kama Bandari, SGR, etc. Mfano Sri- Lanka ndio maana ni vizuri kujua , kupata majibu ya maswali yote labda wengi wataunga mkono hili wazo wakijua ukweli.

Wote tunataka maendeleo, ajira, pesa, ila iwe kwenye win-win situation.
 
Mengi yamesemwa kuhusu sekeseke la bandari ya bagamoyo! Watatezi wa bandari ya bagamoyo ni upatikanaji wa maelfu ya ajira kwa watanzania na maendeleo ya bagamoyo kwa ujumla.

Wapinzani wa bandari ya bagamoyo ni kuwa mkataba ni mbovu kwa kuwa unaruhusu sehemu ya nchi yetu kuwa mali ya wachina na bandari hii itakuwa ni mshindani wa bandari zetu!!Maoni yangu binafsi ni kama ifuatavyo:

Kimsingi bandari ya bagamoyo ni kutoa sehemu ya milki ya Tanzania kuwa ni sehemu ya China!! Huu si mkopo bali tunatoa/tunauza sehemu nchi ya Tanzania kwa China kwa bei che ya kutegemea ajira za chini kwa watanzania na kodi kama waki-declare faida baada ya miaka kadhaa!! Maana lazima wapewe tax holiday (likizo ya kulipa kodi wanaporejesha pesa walizowekeza) kwa miaka isiyojulikana.

Zitto bila aibu anasema "hii si kama nchi ambazo walikopeshwa!" Kwa hiyo waliposhindwa kulipa mradi ukachukuliwa na kuwa mali ya China! Sasa sisi hawasubiri tushindwe kulipa.

Tayari tunawapa tangu day 1 na bandari ya bagamoyo kuwa yao! Wakipata hasara ni wao! Wakipata faida ni wao! Eti huo ndio ujanja! Tunatoa sehemu ya milki ya nchi yetu kuwa sehemu ya nchi nyingine! Kisa eti watanzania watapata ajira.

Faida tunayotegemea kupata watanzania inayoshadidiwa ni ajira!! Lakini kusema ukweli siyo ajira bali ni utumwa katika nchi yako mwenyewe! Haipishani na mashamba ya walowezi waliyokuwa wanamiliki wazungu huko Zimbambwe! Wazimbabwe ndio walikuwa wanafanya kazi kwenye hayo mashamba.

Kwa maneno mengine walikuwa wametatuliwa tatizo la ajira!! Ashukuriwe Mungu kwa ajili ya Mugabe aliyekataa utumwa huu (sisi tunaita fursa ya ajira). Mugabe akasema no way!! Hata kama kwa sasa hatuna uwezo wa kuyaendesha mashamba haya kwenye nchi yetu, mbele ya safari watoto wetu, wajukuu wetu, vitukuu vyetu , vilembe vyetu nk watakuja wapate uwezo na kulima mashamba kwenye nchi yetu!! Alikuwa anaangalia mbali!! Magufuli aliangalia mbali.

Mbele ya Safari watoto wetu, wajukuu wetu, vitukuu vyetu, watakuja watushangae na kutulaani kwa kuuza nchi yao!! Watakuja kulazimika kuanzisha vita dhidi ya wachina ambayo itaigharimu sana nchi yetu!! Naomba kumbukumbu iwekwe sawa ili historia ije itoe hukumu yake.

Majina ya viongozi watakaoruhusu jambo hili yaorodheshwe vizuri na siyo wajifiche kwenye kichaka cha SERIKALI eti "Serikali itafanya mazungumzo na China kuhusu bandari ya bagamoyo". Hao wanao"wakilisha" serikali wajulikane wazi!! Isiwe kama ile kamati ya corona ambayo hawakubainisha majina yao tangu mwanzo na tukajua jina la mwenyekiti tu.

Hata walipopiga picha ya pamoja walivalia kininja ili sura zisionekane eti ni barakoa!! Hawa viongozi wanaotazama leo tu, wanaotaka faida wapate wao tu katika muda wa uhai wao tu bila kujali mustakabali wa watanzania watakaokuja kuishi hapa miaka 1000 ijayo hawatufai.

Kumbukeni scramble for Africa iliyotokea zaidi ya miaka 1000 iliyopita! Wakoloni walivyokuja machifu wetu walikuwa wakipewa shanga, na mavazi na wao wakawatoa watu wao wachukuliwe utumwani.

Watakaokuja kuishi Tanzania miaka 1000 ijayo hawataamini kile ambacho viongozi wetu leo wanataka kukifanya kwa ulaghai wa fursa za ajira!

Majina yao yawekwe wazi kutoka day 1, na tuiachie historia ije kutoa hukumu yake maana upepo unavyoelekea hakuna msaidizi wa karibu aliye tayari kutoa ushauri wenye maslahi ya kitaifa kwa hofu ya kupoteza mkate au kuonekana mpinzani!! Wananchi wa kawaida hatuna namna ya kufanya zaidi ya kupaza sauti zetu. Lakini jueni kuwa Mungu anawaona!!
 
Watanzania kabla ya kuanza huo mradi wa Bandari ya Bagamoyo naomba tafuteni Articles za LESSON FROM SRI LANKA Hambantota port.

Kama hizo article umezipata please tunaomba uzishare ndani ya huu uzi.

Wabongo mnataka mjidai mnawazidi akili wa Sri Lanka ninyi.

Tunataka siku mkianza kulia tulie sote.

Tafuteni Articles tuanze kusoma
Viongozi wetu watueleze wamepewa mabilioni mangapihapo na hao wachina. Tuanze na Ndungai mpaka juu. Unafikiri walimaliza bure Magufuli, kulikuwa na majambo, wanaanza na huo mradi. It is sad, it is sad kuuza nchi kwa ajili ya viongozi hao. Eti huwa ya saps mbele ya jaji. Watawekewa mabillioni huko uswiss etc.

Tumerudi enzi za Kikwete, Ona walivyosota magerazani mpaka wakazirudisha. I cannot believe wanampa huyu mchina mradi huu. Wanauza nchi, na hawajali Bali wana hali matumbo yao tu. Kuondoa utata watueleze wamepewa kiasi gani Kama hongo. Nafikiri hawa wachina walipigiwa simu in March.

Ona walivyofurahi kumwona yumo kwenye box, na wakatembeza hilo box kila mahali ili kutuonyesha ni kweli amekufa. Lini maiti ikatembezwa hivyo - ni Dharau siyo heshima.
 
Well spoken
Na yakimaliza muda wao wa kula nchi hatuwezi kuwashitaki maana wameisha pitisha sheria ya kuwakinga. Hiyo sheria ilitungwa shauri ya utopole Kama huu! Kama you are a good leader, why utunge sheria! These leaders are criminals. Majangili ya hali ya juu. RIP Magufuli
 
Well spoken
They have made a decision why a study tour. Majangili huwa hayafanyi hivyo!! These are criminals. Tabu ya viongozi wetu, wanataka uongozi ili kutuibia hela zetu. Wototo hawana madarasa, hakuna dawa. They care less maana wao watapanda bombardier kwenda kutibiwa nje.
 
Hata kama ni kweli kuwa kuna watanzania watapata "ajira", lakini ni kwa gharama ipi? Kwa gharama ya kufanya sehemu ya nchi yetu kuwa sehemu ya China ili wafanyie uwekezaji wao hapo!! Tunawapa!! Ni mali yao! Si kwamba wametukopesha ili bandari iwe yetu na sisi tuje kurejesha mkopo!! Ni yao asilimia 100!! Can you imagine?

Yetu ni macho tu, na kujisikia vizuri kuwa bagamoyo kuna bandari kubwa kuliko zote Afrika! Halafu bila aibu tunatamba! Tunatambia kuuza/kutoa kutoa zawadi sehemu ya nchi yetu!

Tuje tupate vibarua eti ajira?? Hivi kama ingekuwa inawezekana kuwauliza watanzania watakaokuja kuishi Tanzania miaka 1000 ijayo je wangekubali?? Kumbukeni viogozi wetu kuwa Hii nchi si yetu tu tunaoishi leo!! Tuna wajibu wa kuandaa mazingira rafiki kwa vizazi vijavyo pia!! Historia itawahukumu!! Ni aibu!
 
Mangungu part 2.namwomba rais wetu mpendwa kufanya kongamano la kitaifa likihusisha wabobezi wa uchumi na wasomi wote kwa kila kanda.wanasiasa tusijifiche kwenye chaka la eti tunakuza ajira.

Kiukweli tunalishwa matango pori.mkataba uweke wazi kwa nia njema na ukweli ujulikane.wakichukua bandari ya bagamoyo kiukweli tutizame KIFO cha Bandar ya dsm.
 
Mengi yamesemwa kuhusu sekeseke la bandari ya bagamoyo! Watatezi wa bandari ya bagamoyo ni upatikanaji wa maelfu ya ajira kwa watanzania na maendeleo ya bagamoyo kwa ujumla.
Sisi tunafanya haya kuondoa legacy ya mwendazake hasa kwa kuhakikisha watu wanamsema vibaya tu harafu ikija kugundulika mambo yanaenda ovyo itakuwa ni mwaka 2030 hapo utakuwa utawala mwingine.

Ndiyo maana tumemuondoa kakoko bandalini na mkuu wa majeshi ya navy mr makanzo.
 
Mama katangaza Rasmi kufufua majadiliano na Wachina kujenga Bandari ya Bagamoyo.
Kupitia articles mbalimbali nimeona Wachina wametenga USD 23trilion kutekeleza mradi wa BRI duniani kote zikielekezwa kwenye miundombinu Kama Bandari, airports, barabara RELI(Sgr) nishati na kadhalika . mradi huu wa BRI nchi za ulaya wameupachika jina la CHINESE DEBT TRAP DIPLOMACY.

MIKOPO YA WACHINA.
Tofauti na Nchi za kimagharibi ambazo mikopo na misaada yao hufungamanishwa na masharti ya Uhuru wa Vyombo vya habari, demokrasia na haki za kibinadamu nk... Wachina wao hawasumbuki na mambo ya ndani wao wanaangalia maslahi yao tu kiuchumu. Michakato ktk mikopo hii Mara nyingi huendeshwa kwa usiri mkubwa na Rushwa kubwakubwa. Kwa muktadha huo nchi zenye shida za ndani na madeni wameona kimbilio Ni China(mikopo hii pia hutumika na watawala kuwafanya wabaki madarakani). Hata Kama uwezo wao wa kulipa uko mashakani Wachina watakukopesha tu ilimradi mambo yakikwama wanajua watakuja kushika rasilimali gani kujilipa kwa wakati. Mifano Ni mingi.

1. Sri Lanka walikopa kujenga Bandari ya Hambanthota haikuwa na TIJA wakashindwa kutengeneza faida wakashindwa kuservice mkopo ikawalazimu kuwakabidhi Bandari waiendeshe Wachina lease ya miaka mingi Sana na wao wakiambulia 9% ya faida.

2. Nchi ya Laos(kisiwa) wameshindwa kulipa Deni kwa wakati na wamelazimika kuwapa Wachina Shirika lao la umeme(kwa Tanzania Ni sawa na kuwapa TANESCO) wakusanye hela yake wajilipe kwa miaka 25.

3.Pakistani baada ya kukwama Wachina wamechukua Bandari ya Gwadar waiendeshe (91%) na wajilipe kwa miaka 40.

4. Tajikistan wameshindwa kurudsha mkopo kwa wakati na wamewapa Wachina eneo la mlimani linaloaminika kuwa na madini mengi lenye ukubwa was miles za mraba 1158. Wafanye wanavyotaka wachimbe wanachotaka bila kuulizwa Kama wako nchini kwao
5. Kuna Orodha ya Nchi takriban 40 walionaswa ktk mtego huu.

6. Kwa Nchi za Afrika mifano Ni mingi lakini utawakuta wakenya ambao Sasa wanajadili kuwaachia Wachina Bandari ya Mombasa, Nchini Djibouti pia wamewaachia Bandari, Zambia nao hawako nyuma Wachina waliingia special economic zone kwenye copper belt wameingiza makampuni 600 lakini pia Kuna zaidi ya Wachina 100000+ achilia mbali walioingia kwa njia za panya, pamoja na yote WAZAMBIA hakuna walichofaidika nacho na Sasa madeni yameiva hawana uwezo wa kulipa na Wachina Sasa wanataka wapewe Kaunda international Airport na au Machimbo ya Copper.. Nasikia hata aliyekuwa mpinzani, Sasa Rais Satta alishinda uchaguzi baada kuahidi kushughulikia uvamizi was Wachina pale Zambia.

WACHINA WANATUDHARAU AU WANATUOGOPA!?
Najiuliza hili swali kwa sababu Moja kubwa. Maeneo mengine yote Wachina wamechukua assets/Rasilimali za mataifa husika baada ya Nchi husika kushindwa kulipa kufutia kuelemewa na Madeni. Tanzania tumeambiwa waziwazi tupeni Bandari tujenge, tuindeshe kwa miaka 33-99, turudishe gharama zetu ndio tuwaachie🤣🤣🤣.

Je wameona sisi Ni wajinga Sana au wajanja Sana🤔🤔🤔?
Au wameona wakitukopesha cash tujenge wenyewe tutaweza kulipa na wao washindwe kushika rasilimali zetu? Walivyo wajanja wanakutajia makampuni sijui viwanda 700 kama sehemu ya mradi ili watu tuone Kuna ajira za kumwaga.

Tujifunze Zambia ambako Wachina Wana makampuni 600 na bado tatizo la Ajira liko palepale. Bado nakumbuka kauli ya Mama kumpa Uhuru muwekezaji kuleta watu anaotaka hapo watabaki walinzi na wafagiaji tu yaani🙄🙄

SSH NDIO SMM (SULTAN MANGUNGO WA MSOWERO) KWA KARNE YA 21?
Sultan MANGUNGO wa Msowero aliingia mikataba na wazungu wakati ule kumbe anasaini kuridhia kutawaliwa na wajerumani bila kujua.

Naam naiangalia Tanzania na umahiri wake ktk mikataba ya Kimataifa, najiuliza uwezo na uzalendo wa wajumbe na wanasheria na wataalamu wetu kwenye hii mikataba. Sijasahau miktaba iliyosimamiwa na kina Chenge wazee was vijisenti. Naam Ile mikataba ya IPTL. DOWANS au Ile ya Net Group Solution walioendesha Shirika la Ttcl, wakatufilisi wakaondoka na mtaji wa celtel yao.

Aidha MFUMO wa Bandari ya Bagamoyo unanikumbusha enzi za Mkapa wakati BARRICK GOLD wanaingia.

Walidai uwekezaji wa migodi gharama yake ilikuwa sawa na bajeti ya Nchi ya wakati ule. Kwamba Ni mkopo na wanapoanza shughuli wasiulizwe mpaka warudishe ule mkopo., Kwanza walitudanganya Kuna madini mengi Sana kiasi ambacho hata watakapo maliza kulipa na kunza kutoa Kodi watachimba kwa miaka mingi Sana mbeleni. Leo hata kabla hawajatangaza kurudiaha mtaji Buzwagi madini yamekata wanataka kufunga.

Lakini hata mtaji uliowekezwa hakuna aliyethibitisha huenda Ni nusu tu ya gharama iliyotajwa. Hata walichokuwa wanapata hakuna aliyejua, mwisho wa siku wanasema mwaka huu tumepata hasara hatujalipa Deni. Katika Hali Kama hiyo naona Bandari huenda ikajengwa hata kwa 4bil USD tukaambiwa 10b. Na wakati wa makusanyo tukaambiwa labda nusu tu na kila siku wakawa wanapata hasara mpaka ifike miaka hiyo 99 halafu ikikaribia kwisha wanaitelekeza bila ukarabati labda kwa miaka 10 ya mwisho
Siku mkikabidhiwa ukarabati unagharimu nusu ya gharama ujenzi wake, mnaenda kukopa Tena.

Najiuliza huyu SAMIA ana lipi jipya la kuwashinda WACHINA wenye uzoefu wa miaka 20 ya BRI yao. Jamani hivi huyu mama hawezi kugeuka Sultan MANGUNGO WA MSOWERO?

JPM alijulikana kwa kupenda sifa na kufanya miradi mikubwa, huu Ni mradi mkubwa kuliko miradi yake yote kwa miaka yote aliyokuwa madarakani kiujumla. Kubwa zaidi Ni mradi ambao utekelezaji wake ungeendelea bila kugusa miradi mingine aliyokuwa anajenga. Ndio kusema miradi iliyopo ingekuwa inaendelea huku Bandari ya Bagamoyo ikiendelea Kujengwa kulikuwa na credit kubwa na nyingi Sana kwa ukubwa wa huu mradi, lakini aliona madhara Ni makubwa kuliko hasara zake AKAACHANA NAO.. Pamoja na MAPUNGUFU ya JPM lakini sijawahi kutilia Shaka uzalendo wake na dhamira yake kwa taifa.

Leo Mama ameona faida yake wapi?

Tusubiri tuone?
 
Weka hapa huo mkataba wa bandari tuuso e. Mkataba wa mangungo ubafahamika.
 
Back
Top Bottom