Mkataba uwekwe wazi wote (warts and all terms and conditions and small prints). Hakuna mkataba mzuri wenye manufaa kwa Mtanzania, utakao pingwa na Majority ya Watanzania.
Switzeland wana utaratibu wa kupiga kura kwa mambo yote makubwa, ya msingi ya taifa. Hili ni jambo kubwa, la msingi sana.
Ni muhimu kujua kama usimamizi, ukaguzi, kodi, Bandari za Dar, Tanga, Mtwara zitaathirika kufaidika vipi? Zitakufa?
Miaka mingapi wanapewa kuimiliki, ajira ngapi zitakuwa kwa Watanzania, deni (kama litakuwepo), upande mmoja ukikiuka, ukivunja masharti / makubaliano nani atakuwa msuluhishi, adhabu gani zitahusika. Who is going to enforce those penalties.
Rushwa, mikataba mibovu inazibitiwa vipi? Miradi yote mikubwa huwa kuna risks kubwa sana rushwa kukithiri.
Kukiwa na uwazi unaweza kupunguza Rushwa.
Mwanga (uwazi) hufukuza giza ( rushwa, mikataba mibovu, upigaji).
Hii issue iangaliwe kwa maslahi mapana ya Taifa, na vizazi vijavyo.