Watanzania kushangilia kuangushwa kwa Makonda katika kura za maoni Jimbo la Kigamboni kunaashiria nini?

Ndiyo mlikuwa mnashirikiana nae kuteka watanzania ?
 
Media influence, unaweza mfananisha Makonda na mkuu wa mkoa yupi Tanzania, binadamu amejazwa chuki bila kuchambua mwenyewe kichwani mwake.

Nina imani na Makonda, hata kama hapo amekosa, ila kuna sehemu atapata bureee kabisa bila kupingwa.

Sometimes watanzania tumezoea kuongozwa na wapiga dili na wasanii sanii tu, watanzania wamefika sehemu hawataki kiongoz anayeleta maaendeleo, hawataki mabadiliko.

Magufuli ameingia, watu wanamtukana, wanabeza, hv tangu mtu umezaliwa kuna rais amewah kuwa namna hii kama ya Magufuli? Sasa watanzania mnataka nini? The same to Makonda, mtaona mengi sana na mtateseka sana mioyo yenu isiyotaka positive changes.. change ur mind
 
Sawa, apakatwe tu kama alivyozoea kupakatwa labda toka utotoni lakini kura za raia huru wenye akili huyo shetani hapati ng'o! Mtu mzima unapakatwa kama kitoto kichanga, hiyo ni aibu kubwa. Halafu alivyo mhuni, anaweza akawanyea waliompakata halafu kazi ya kuzoa uharo wanaachiwa akina chagu wa malunde🤣
 
Umemjibu mtoa mada kijinga na kishabiki tuu. Point yake haikuelemea kushindwa kwake bali mapokeo ya matokeo sio kwa Kigamboni tuu bali kwa nchi nzima.
Nadhani Rais Magufuli hana fikra kama zako zilizo lala hivyo anaona reaction ya Watanzania kuhusu mapokeo yao kwa kupigwa chini maoni ya awali kwa "RC bora nchini" kama alivyokuwa anamnadi.
Pengine anajiuliza jee Makonda alikuwa amenishika kwa nguvu za Giza hadi sioni asivyokubalika?
Maana sasa sio siri kama unatumia akili kujua kuwa mama Samia hamkubali, Majaliwa na Bashiru hawamuungi mkono na hata mawaziri na viongozi wenza mkoani walikuwa hawaendi sambamba naye.
Kuna somo ambalo hata yeye Rais atakuwa amejifunza, watanzania waweza kuwa wamekuchoka lakini wanakushangilia jukwaani ila ukibwagwa na kama ulikuwa na kiburi watakuzodoa hadi waweza kukonda kwa siku mbili tuu.
 
Makonda utendaji na tabia ake ni nakala halisi ya Magufuli.

Kama watu walitunza moyoni hasira dhidi ya Makonda, ina maana hata Magufuli wana fundo nae, ni suala la wakati tu
 
Mchakato wa uchaguzi ndani ya Ccm mbona mmeutolea macho sana? Waacheni Ccm wapitishe watu wao alafu msubiri kichapo Oktoba.
 
Hahaaaaaa.......... 😁 😀
 
Wewe ndio umechemka unajadili na kuongea kama mass

Wakati unajua kabisa hata mshindi wa tatu anaweza kusimamishwa


Wanasiasa wanapenda watu kama wewe,


Ndugulile ashaondoka kuwa chagua la mkuu, kumbuka hilo

"Ndugulile ashaondoka kuwa chaguo LA mkuu" kwa hiyo unatuaminisha kuwa maoni ya wanaccm hayana maana kama wewe sio "chaguo la mkuu"? Sasa hicho ni chama cha siasa au Mali ya Bwana na Bibi Magufuli! (Family party)?
 
Kuth Unadhani Kuthubutu nayo ni sifa inayojibeba?

Muongelee Pompeo kwa sentesi tatu zinazomuhusu makonda!

Alithubutu pia kuiba simu!

Alithubutu pia kumchapa makofi MZEE Warioba.

Alithubutu pia kutoa 10m kwa kuchezewa vizuri na kolikipa mmoja.
 
Alikukosea nini Msukuma wa watu yule??.
 
WEWE itakuwa ndio Bashite mwenyewe...ulichopatia kuhusu makonda ni kuwa anapenda kujaribu na kila muda huwa anajaribu
 
Hana utendaji wowote na hizi ziwe ni salaam kwa mteuzi wake kuwa wana dsm tuliishi maisha magumu kwa kulazimishwa kuongozwa na mtu tusiyo mtaka.
 
Wape salaaaaam
Ni ujumbe kuwa Makonda na Magufuli aliyemkumbatia muda mwingi tumewachoka.
Ndio maana Magufuli alihakikisha anasimama mwenyewe kwenye kura za maoni.
Angeacha kampenyo tu asingetoboa
 
Hii yote ni rushwa! Unataka kuinfluence vikao vya juu! Makonda mpaka sasa ni number 2 na wanahitajika watatu! Kwenye duru linalofuata hao watatu wanaanza moja wote na Makonda anaweza akatoboa au akashindwa kabisa. Ndungulile anaweza akatoboa au akashindwa - hiyo ndiyo demokrasi. Msifurahi mwanzoni!
 
Wala sio kampeni meneja wala sipendelei mtu. Ila nazungumzia utaratibu wa kupata jina moja bado unaendelea. Na haijulikaani nani atapitishwa huko mbele mbona nyie mnaanza kufurahia upuuzi na Makonda ameingia kwenye mchujo wa majina matatu.
Tumia akili wewe ebo! Mbona unachosha watu kukuelimisha?
Mleta mada haongelei kushindwa kuchaguliwa maana bado, lakini maoni ya wana Kigamboni (jimbo ndani ya mkoa aliokuwa kiongozi wake) kumkataa na jinsi jamii ilivyopokea habari hiyo!
Mbona wenye mamlaka wanaweza kumpa cheo chochote wakipenda?
Mfano Magufuli akibahatika kutangazwa kashinda nani anaweza kumzuia kumteua kuwa mbunge na kuanzisha cheo nje ya katiba NAIBU WAZIRI MKUU na akampa? Hakuna.
Lakini hiyo inaondoa funzo alilolipata Magufuli na Makonda kuhusu imani ya wananchi kwa wenye viburi?
Haiondoi na inabaki palepale. Ndio kiini cha mada yake.
 
Sema tu kuwa makonda hakubaliki mkoa mzima wa dsm
Siyo "ku-influence" bali nimetoa rai kwa vikao vya juu viheshimu maamuzi yaliyofanywa na kikao cha mapendekezo cha wanaccm wa jimbo la Kigamboni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…