Watanzania kushangilia kuangushwa kwa Makonda katika kura za maoni Jimbo la Kigamboni kunaashiria nini?

Mwanzoni ulimquote chagu nikabaki nashangaa tu.
 
Genta naona umefurahi sana! ila weka akiba ya maneno,Makonda atapata position serikalini,wewe endelea kufurahi kwa muda.
 
Atasema vita ya madawa haijawahi kumuacha mtu salama
 
Makonda ni kimbelembele cha mafanikio ya serikali ya awamu ya 5, yeye kuangushwa na watu kufuruhi ni dalili mbaya sana kwa serikali, ni wakati sasa wa kujitathimini.
 
Mwuaji mkubwa Bashite..
Nchi yote ina furaha isipokuwa Le mutuz tu ndio amenuna..
Asante sana Kigamboni.
 
Huu ni mwanzo wa mwisho wa DAB kwenye siasa za Tanzania, huyo hata afurukute vipi system imeshamtapika.
 
Mnafeli sana. RAIS anajua kuwa kama Makonda hakubaliki na yeye hakubaliki lazima atajibu mapigo kwa kumrudisha ili KUWAKERA
 
WEWE itakuwa ndio Bashite mwenyewe...ulichopatia kuhusu makonda ni kuwa anapenda kujaribu na kila muda huwa anajaribu
Mtu yeyote hata wewe unaweza kuwa kiongozi ila kiongozi mzuri ni yule mwenye maono, mbunifu na mwenye uthubutu hasa wa mambo ambayo yamekuwa yakiwashinda wengine na hizi sifa ndizo alizonazo Makonda.
 
Makonda, sina shaka, ndiye kiongozi anayechukiwa na wananchi walio wengi kuliko mwingine yeyote. Na kwa kiasi kikubwa, hata kuchukiwa kwa Rais Magufuli na baadhi ya wananchi, kwa kiasi kikubwa kumechangiwa na Makonda.

Jina la huyu bwana kuhusishwa na watu wasiojulikana, kuna mchango mkubwa pia. Jina lake limehusishwa na mauaji ya baadhi ya watu, mashambulio, kupotea na mateso ya watu, kiasi cha hata Serikali ya Marekani kutamka wazi kuwa amekuwa akiwanyima watu haki ya kuishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu yeyote hata wewe unaweza kuwa kiongozi ila kiongozi mzuri ni yule mwenye maono, mbunifu na mwenye uthubutu hasa wa mambo ambayo yamekuwa yakiwashinda wengine na hizi sifa ndizo alizonazo Makonda.
Mbunifu na mwenye uthubutu kwenye;

1. Kuteka
2. Kuua
3. Kubamibikia watu kesi
4. Kutoheshimu mawaziri
5. Kufeli kila mishen
 
wamefanya la maana sana kumkataa, hii itamfanya atie akili kidogo maana alisha jisahau. Makonda ni mtu wa magufuli na atakuja kupewa cheo kizuri tu. Hata asipo pewa cheo kwa sasa makonda ni Tajiri sana.
 
Ni kweli alukuwa na uthubutu. Kama aluweza kumtandika kibao Mzee Warioba nn angeshindwa?

Kilichopelekea Watu kufurahishwa kwa kuangushwa kwake ni kile kiburi chake juu ya Viongozi wengine kutokana na Mamlaka za Teuzi. Makonda kabebwa sana na Mamlaka za Teuzi hali iliyompelekea yeye kujiona ni bora kuliko wengine.
 
Kama ni hivyo kwanini ameangukia pua kwenye kura za maoni? Huyo watu walikua wanamsujudu kutokana na nafasi aliyokuwepo lakini kiuhalisia wengi walikua hawakubaliani naye kabisa. Shughuli imeisha huyo.
 
Kushika namba mbili kwenye kura za maoni sio kwamba ndio kaanguka...

Muda ukifika Mh. Makonda atawashangaza wengi...
 
Pompeo alishamaliza kazi " Bashite ananyima watu haki ya kuishi' ( YAAANI NI MUUWAJI) Over and out
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…